MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Sunday, 21 May 2017

FATILIA NAMNA CHELSEA ALIVOPATA UBINGWA WA EPL MWAKA HUU

alfachengula.blogspot.com/chelsea alivopata ubingwa wa epl msimu huuSafari ni safari,iwe masika au kiangazi na kutangulia sio kufika walisema wahenga,maneno haya huja baada ya kutangulia kufika katika safari yako na kumzidi yule aliyekutangulia.

Antonio Conte aliteuliwa kuwa meneja wa Chelsea mnamo juni 2016 wakati akiwa kwenye Euro 16 pale Ufaransa na kikosi cha timu ya taifa ya Italy ambayo alifanikiwa kuifikisha  katika hatua ya robo finali ambapo walitolewa na Germany katika mikwaju ya penati.

Safari ni safari tu,Antonio Conte akawashukuru mashabiki na wanamichezo wa Italy na kufungasha virago vyake na kuelekea Chelsea akiwa na mdogo wake Gialunca Conte.



Antonio Conte alipokuwa anatambulishwa Chelsea

Safari yake ndani ya Chelsea ilianza kwa kumsajili Ngolo Kante,Marcos Alonso na mwishowe kumsajili David Luiz kutoka PSG,Antonio Conte hakuishia hapo aliwarudisha Victor Moses na Juan Cuadrado na kwenda nao Marekani kwa ajili ya pre season.

Katika pre season Conte akiwa na Chelsea walicheza michezo mingi ikiwemo ule wa Real Madrid,Ac milan na Liverpool,maandalizi ya msimu mpya 2016/17 yalienda vizuri kiasi kwamba akaweza kupata kiasi cha wachezaji ambao aliwatumia katika msimu huu.

Moja kati ya wachezaji ambao  waling'aa katika maandalizi hayo ni Victor Moses ,ambaye alikua sio chaguo la makocha waliopita Chelsea kabla ya Conte kiasi cha kufikia kuwa mchezaji aliekua anatolewa kwa mkopo kila msimu.

Mwisho wa Pre season Conte alipata kikosi chake kwa ajili ya msimu mpya huku akimtoa Juan Cuadrado kwa mkopo wa miaka mitatu Juventus.

Wiki na siku zikasogea Antonio Conte akiwa ameshapanda basi aliloamini ni la mafanikio kwake Chelsea na kuendelea kutembea sentimita kwa kilometa hadi pale pazia la ligi kuu lilipofunguliwa mnano mwezi August,2016.


Antonio Conte akishangilia moja ya magoli ya Chelsea.

Conte alikishuhudia kituo chake cha kwanza katika safari yake pale Stamford bridge alipocheza na Westham na kupata ushindi wa mabao mawili kwa bila,ambao uliashiria mwanzo mzuri kwake magoli mawili ya Hazard na Costa yalitosha kumkaribisha katika Epl kwa furaha.

Siku saba baadae akasafiri kuelekea Vicarage Road akacheza mchezo wake wa pili dhidi ya wenyeji Watford fc na kupata ushindi mwingine wa 2-1 mabao ya jioni ya Diego costa na Michy(Batshuayi) yalimwinua Antonio,mashabiki wa Epl duniani kote walishuhudia aina mpya ya ushangiliaji kutoka kwa meneja huyu,aliendelea na ushindi wiki ilofata kwa burnley alipowachapa 3-0,Stamford bridge.

VIKWAZO,kama zilivyosafari nyingine Antonio katika safari yake vikwazo vilianza alipokutana na Swansea na kutoa sare ya 2-2,akacheza nyumbani na Liverpool akafungwa 2-1 kaenda Emirates akachapwa 3-0 na Arsenal fc mabao ya Sanchez,Özil na Walcott yaliutetemesha usafiri wa Conte na kumfanya aone safari ni ngumu kiasi chake.



Sanchez akiifungia Arsenal moja ya magoli dhidi ya Chelsea
 
Huu ulikua mwezi Septemba,ndio mwezi ambao msafiri mwenzake Pep Guardiola alitamba na kusema Epl ni ligi nyepesi kwa Manchester city na yeye,hapa ndipo mashabiki mbalimbali duniani kote wa Chelsea wakaanza kukata tamaa na dereva Antonio Conte,ikatabiliwa hatomaliza msimu na kutimuliwa kama mwenzake Andre Villas Boas na Roberto Di Matteo.

ANTONIO,alionekana mwenye huzuni mbele ya waandishi akasema "Chelsea ni timu bora kwenyekaratasi ila sio chochote ikiwa uwanjani,tunatakiwa tufanye kazi kwa bidii",pia akawapa maneno ya kuwafariji "tutashinda pamoja,tunafungwa pamoja,nashukuru wa sapoti yenu mashabiki".Tunaweza sema Conte amshukuru Wenger kwa kumwamsha usingizini.

Wasiwasi ndo akili wahenga walinena,mtaalamu huyu wa mifumo ya kiitaliano catenaccio(door-bolt),mfumo ambao timu uanza kuboreshwa kwenye safu ya ulinzi,akakaa mezani na benchi lake la ufundi na kuleta 3-4-3,akiwatumia Luiz,Cahill na Azpilicueta kwenye safu la ulinzi huku Matic na Kante wakicheza kama box-to-box midfielders  katika eneo la kiungo,Moses na Alonso wakicheza kama wingbacks(beki za pembeni za kupanda na kushuka),Hazard,Costa na Pedro wakiongoza mashambulizi.

Msemo wa mababu zetu, mchumia juani,kulia kivulini ulithibitika mwanzoni mwa mwezi Octoba akifungua kwa kuwachapa Hull city pale KCOM stadium na baada ya hapo alishinda mechi zote nne nakuendeleza wimbi la ushindi wa mechi 13 mfululizo kati ya mechi hizo aliweza kuzichapa timu kama Tottenham,Manchester city,Everton,Leicester na kudondosha kichapo kikali kwa meneja wa zamani wa klabuni hapo Jose Mourinho,kichapo cha mabao 4-0 katika uwanja wa stamford bridge alipokua akilejea kwa mara ya kwanza tangu kutimuliwa kwake.


Conte,akiwa na tuzo ya kocha bora wa mwezi December.

KOCHA BORA,Antonio Conte katika safari yake aliweza kuweka record ya kuwa kocha wa kwanza katika historia kuchukua tuzo ya kocha bora wa mwezi mara tatu mfululizo(October,November na December) akiwapiku makocha wengine kama Wenger,Alladyse,Mourinho,Guardiola na mtaalamu Jurgen klopp wa Liverpool.

FA cup,safari ya muitaliano Conte haikua kwenye ligi kuu tu bali aliweza kuitoa Peterborough katika raundi ya tatu,Brentford raundi ya nne,Wolverhampton katika raundi ya tano,Manchester United(robo fainali),Tottenham Hotspurs katika hatua nusu fainali na kufanikiwa kutinga fainali ambapo watacheza na Arsenal fc tarehe 27 may katika uwanja wa Wembley.

Vita ya panzifuraha ya kunguru,lakini pia fahari wawili hawakai zizi moja Tottenham walitudhihilishia misemo hii pale walipokubali kichapo kutoka kwa vijana wa  Slaven Bilić,Westham united  kichapo cha bao moja bila,Tottenham walijiengua katika mbio za ubingwa siku hio na kumfanya fahari mmoja Antonio Conte kubaki pekeake kwenye zizi.Antonio aliwachapa Middlesbrough mabao matatu na kuwashusha daraja huku akijihakikishia nafasi ya ubingwa kwa kuongeza tofauti ya point saba dhidi ya Tottenham.


Wachezaji wa Chelsea wakishangilia baada ya mechi ilowapa ubingwa.

CHELSEA BINGWA,Hauchi hauchi unakucha. Hayawi hayawi huwa,baada ya msoto wa msimu mzima tabu na kero walizokumbana nazo Chelsea msimu wa 2015/16 chini ya Jose Mourinho na kumaliza ligi wakiwa nafasi ya 10 huku wakimwacha Leicester city anachukua ubingwa,hatimaye shida zimemalizwa na mtaalamu Antonio Conte ambaye kwa sasa mashabiki mbalimbali duniani wamempa jina la Master plan baada ya kuibadilisha Chelsea kwa kipindi kifupi alichokaa darajani(stamford bridge).

CHELSEA,sasa ni bingwa rasmi wa ligi kuu England baada ya kuwachapa Westbrom bao moja kwa bila,goli la Mbergiji Michy Batshuayi limeipa ubingwa wa tano Chelsea.

Records zilizowekwa Antonio Conte.

Antonio conte,anakua kocha wa nne kuchukua Epl katika msimu wake wa kwanza anaungana na makocha Jose Mourinho(2004/05),Ancelotti(2009/10) na Pellegrin(2013/14).

Conte,anakua muitaliano wa nne kuchukua ligi kuu England,baada ya Carlo Ancelotti(2009/10),Roberto Mancini(2011/12) na Claudio Ranieri(2015/16).

Conte,ni bingwa wa michuano ya vilabu kwa misimu minne mfululizo,ameshinda Serie A akiwa Juventus mara tatu mfululizo (2011/12,2012/13,2013/14) na Epl akiwa Chelsea msimu huu (2016/17)

No comments:

Post a Comment