Karibu katika kisa kitamu cha jina la MKE WA RAISI usiskose kutembelea blog ya
alfachengula.blogspot.com....... anza nayo
PART ONE
SEHEMU YA 01
Kwa jina ninaitwa Adrus Maldi, kwenye maisha yangu ndoto zangu zote zilikuwa ni kuwa askari, kama. ilivyo kuwa kwa baba yangu mzee Maldin. Baba yangu alifariki katika kifo cha kutatanisha nikiwa bado mtoto wa miaka kumi na mbili. Nilibaki na mama pekee, kwani sikuwa na kaka wala dada, au wadogo zangu, ikimaanisha nilizaliwa peke yangu kutoka tumboni mwa mama yangu Asma. Kila nikitazama mkusanyiko wa watu walio hudhuria halfa ya kufuzu mafunzo yetu ya ukomando au kwa jina jingine P.S.S(President Securty Service), moyo wangu unajisikia furaha sana kwani, ndoto zangu zimetimia japo si kwa asilimia mia moja ila kwa hapa nilipo fikia ni pakubwa sana kwenye maisha yangu. Tuliingia wengi sana katika chuo hichi cha ukomando hapa nchini Cuiba, tukitokea mataifa mbali mbali duniani, hadi leo tunamaliza tumebakia vijana mia moja, wengi wao zaidi ya mia tano waliweza kukumbwa na matatizo mbalimbali huku wengine wakifarika katikati ya mafunzo haya magumu, ambayo pasipo rehema za mwenyezi Mungu na kuwa makini nilazima ufe.
Macho yangu muda wote yakawa yakipita pita kwenye majukwaa yaliyo jaa ndugu na jamaa walio kuja katika shuhuli yetu hii ya leo, nikamuona mama akiwa ameketi kwenye moja ya jukwaa akiwa na furaha sana huku mkononi mwake ameshika kijibendera kidogo chanye rangi za bendera yetu ya nchi ya Tanzania. Furaha iliyo jaa kwenye uso wake, iliniashiria kwamba ni mzima wa afya japo tangu alipo kuja nchini hapa Cuiba, tuliwasiliana kwa simu tu. Nikiwa kama kioongozi wa gwaride, ilinibidi kukaa mbele, huku nikiwa na bundukia yangu yenye singe inayo ng’aa mbele. Baada ya amri mkuu wa jeshi la nchi hii kuingia ndani ya uwanja, sherehe zikaanza. Ngoma za bendi ya jeshi zikaanza kupigwa na wezetu walio kuwepo kwenye kitengo hicho huku nasi taratibu tukianza kutembea kwa mwendo wa kawaida kupita mbele ya amiri jeshi mkuu, pamoja na mkufunzi wa mafunzo ya chuo hichi na baadhi ya viongozi wa serikali ya hapa Cuiba walio kuja kujumuika nasi kwenye haya mahafali.
Tukazunguka mzunguko wa kwanza, kwa mwendo huo wa kawaidia, kisha milio ya ngoma ikabadilika na kuanza mwendo wa taratibu. Kama tulivyo pita awali ndivyo jinsi tulivyo pita kwa mara ya pili. Huku sote tukiwa makini kwa kile tunacho kifanya sikuu hii ambayo kila mmoja aliitamani kuifikia na pasipo kuwa na moyo wa uvumilivu nilazima ushindwe mapema. Tukapita mzunguko wa tatu, huku mwendo ukiwa umebadilika na kuwa mwendo wa kasi, ulio wafanya watu wote waliomo ndani ya uwanja huu wa chuo chetu cha ukomandoo wapige makofi kwa furaha iliyop pitiliza. Miguu yetu ilienda sawa sawa, huku ikipigiga chini kwa nguvu zote kuhakikisha kwamba tunawadhihirishia watu sisi ni makomandoo hodari tulio stahili kuwa katika siku hii ya leo.
Tukamalizia kutoa heshima kwa amiri jeshi mkuu, kilicho fwata ikawa ni kazi ya sisi kuonyesha michezo mbali mbali ya kijeshi, ikiwemo kama komando kupambana na watui ziaidi ya hamsini akiwa peke yake na kufanikiwa kuwashinda na kuwapiga vibaya. Tukazidi kuwaburudisha watu kwa kile tulicho fundishwa kukifanya katika siku nzima ya leo. Tukamaliza kufanya burudani hizo, na kupewa dakika tano kubadilisha nguo zetu, na kurudi uwanjani kwa ajili ya kutunukiwa medali, pamoja na vyeti vinavyo tuyoneyesha kwamba sisi ni makomandoo wa majeshi yetu.
“Adrus, leo umetupelekesha kama sio wewe” Mmoja wa wezangu aliniambia tukiwa ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo.
“Weee acha hata mimi mwenyewe siamini kama tumeweza kufanya kile tulicho kifanya”
“Kweli kaka, yaani siku tukienda kwenye mission, ya mwisho MUNGU atusaidie tuweze kurudi salama”
“Kweli kaka”
Tukarudi uwanjani tukiwa tumevalia suti nyeusi huku kila mmoja akiwa katika hali ya furaha. Katika makomandoo mia moja, wanawake walio salia ni wawili tu, mmoja akitokea nchini Nigeria huku mwengine akitokea nchini Russia. Wengine wasichana tulisha wazika na wengine walipata vilema vya maisha kutokana na hatari ya mazoezi yote tuliyo yafanya.
“Haikuwa kazi ndogo wala rahisi kwetu kuweza kufikia hapa. Tumepitiwa na mambo mengi yaliyo tufanya tuweze kuingia katika matatizo mbali mbali”
Nilizungumza kama kiongozi wa wahitimu wezangu kupitia kipaza sauti, uwanja mzima ulikaa kimya watu wote wakinisikiliza kwa kile kitu nilicho kwenda kukizungumza mbele ya umati huu.
“Tuliwapoteza wezetu wengi, wakike na wakiume. Ila imani yetu ni kwamba wanaendelea kuwa nasi katika kila jambo ambalo tunalifanya katika maisha yetu ya hapa duniani. Mungu azilaze pema roho za wapendwa wetu amina” Wezangu tisini na tisa wakasimama kwenye viti vyao, sote tukaweka mikono yetu kwenye vifua na kuanza kuimba wimbo maalumu tulio utunga kwa ajili ya kuwaombea wezetu tulio kuwa nao, ila kwa sasa wametutoka duniani. Baada ya kumaliza kuuimba wimbo huo, nikapiga saluti mbele ya amirijeshi mkuu. Kwa mwendo wa hatala nikarudi kwenye kiti changu na kukaa chini kuacha mambo mengine kuendelea. Baada ya risala ya amiri jeshi mkuu, juu ya kututaka tuwe watendaji wazuri kwenye kazi zetu, tukaanza kukabidhiwa medali pomoja na vyeti vyetu, ambavyo tulikuwa tumevisubiria kwa hamu kubwa sana. Tukaanza kuitwa kwa kufwatisha alfa beti za majina yetu. Baada ya zoezi hilo tukawa huru kwa kufanya sherea na wanandugu walio kuja kututembelea
“Ohhhh Hongera sana mwanangu” Mama alizungumza huku akinikumbatia kwa furaha sana
“Asante mama, nimefanikisha mama yangu” “Kweli mwanangu ndoto huwa kweli Mungu ni mkubwa”
“Amen. Vipi Tanzania wanaendeleaje?”
“Huko ni kwema tuu, ndio watu wanajiandaa andaa na uchaguzi wa mwaka huu”
“Ahaa” Mama aliniletea zawaidi za kunipongeza, ikiwemo maua na makadi yaliyo andikwa ujumbe mzuri wa kunipongeza. Kusema kweli nifuraha kubwa sana kwenye maisha yangu. Tukapiga picha kadhaa na mama yangu, pamoja na wezangu baadhi walio pita karibu yetu ikiwa kama ukumbusho wa tukio hili, ambalo si rahisi kwa mtu kuweza kulisahau akilini mwake kwenye maisha yake yote.
“Natamani baba yako angekuwepo, ninaamini angefurahi sana kuona dume lake limekuwa komandoo” “Hahaaa kweli mama, ninaona hata huko alipo pumzika wakati huu, ninaamini anafurahia kwa kile kilicho jitokeza katika maisha yangu” “Ila mwanangu kuwa makini, nisinge penda kukupoteza kama nilivyo mpoteza baba yako kipenzi changu”
“Mama hadi kuwa komandoo, ina maana nipo makini sana. Hata katika kale kajirisala kangu niliko kasoma, unaweza kuona jinsi nilivyo kuwa makini kutokana kuna wezetu wengi tu wamepoteza maisha yao”
“Ni kweli mwanangu, ila kuna jambo moja tu napenda kukuambia. Zingatia sana sheria, usiwe muonevu kisa wewe ni komando, mtendee kila mtu jema, awe mkubwa au mdogo kwani swawabu zako zitaandikwa mbinguni kwa mwenyezi Mungu”
“Sawa mama nimekuelewa” “Pia hakikisha unatafuta mtoto mapema” “Mamaa”
“Haaa miaka ishirini na nne sasa, inabidi uniletee kamjukuu ka kucheza nacho. Hivi unadhani kwa kazi yako hiyo ilivyo kuwa nguma. Nitakuwa na muda wa kuonana na wewe mara kwa mara?”
“Sawa mama nitalifanya hilo” “Lini?” “Mom, inahitaji muda kidogo”
“Adrus weee haya” Mama alizungumza kiutani na kutufanya sote tutabasamu kwa furaha, nikamtembeza tembeza kwenye baadhi ya maeneo ya chuo chetu. Hadi inafika mida ya jioni, nikamrudisha kwenye hoteli aliyo fikizikia kwa ajili ya kurudi kesho yake nchini Tanzania.
“Adrus ninakupenda sana mwanangu, ninakuombea kwa mwenyezi Mungu akupe rehema zake uweze kufanikiwa kwa kila kitu unacho kifanya” “Amen mama yangu hata mimi pia ninakupenda sana, bila ya wewe na baba kunileta duniani na kunilea katika mazingira na maadili mema nina imani hata leo nisingeweza kuwa hapa.”
“Tena nilitaka kusahau, nimekuja na picha ya utotoni mwako, tuliyo piga tukiwa wote watau” Mama akatoa picha iliyo onyesha sura za zetu, akiwemo na baba yangu.
“Itunze hii mwanangu, kama ukumbosho wa kumbukumbu yako kwa baba yako, nakukumbushia tena mwanangu kuwa kama baba yako, alipenda amani, haki na kumsaidia kwa kila aliye hitaji kupata msaada wake” “Sawa mama nitalifanya hilo” “Kwa hiyo unarudi lini Tanzania”
“Mmm kuna miezi mitatu mbeleni, baada ya hapo tunarudi majumbani mwetu”
“Sawa nakutakia maisha mema mwanangu” “Nawe pia mama”
Nikaagagana na mama, nikaondoka eneo la hoteli na kurudi zangu chuoni ambapo siku ya leo kumeandaliwa sherehe kubwa usiku. Kila mmoja mwenye kipaji chake alipewa nafasi ya kuonyesha uwezo wa kipaji chake. Huku uongozi wa chuo ukitupa zawadi moja kubwa ya kutuletea wasichana wazuri kutoka katika kambi ya jeshi la nchi hii, kuja kujumuika nasi, kwa maana idadi ya wasichana chuoni kwetu haifiki hata ishirini.
“Adrus cheki watoto walivyo fiti, yaani wanang’araa mbaya” Rafiki yangu Aron alizungumza huku akinoinyesha dada mmoja aliye panda hewani, akiwa na figa nene, huku nywele zake zikiwa zimelala vizuri na amezifunga kwa nyuma.
“Ebwanaa watoto hao”
“Ndio hivyo mwanangu, hapa nilipo nina ugwadu wa kama miaka miwili ” “Hahaaa kuwa makini na kibuti usije ukakichezea”
“Ahaa wapi, asikudanganye mtu, watoto wenyewe wanaonekana wana shobo”
Aron ni mmoja ya rafiki zangu nilio toka nao nchini Tanzania, huku rafiki zetu wengine watano tulio kuja nao kutoka nchini Tanzania, walipoteza maisha kwa njia tofauti tofuti sana.
“Haya mwaya kazi ni kwako”
Aron akaondoka na kuniacha nikiwa ninamtazama jinsi anavyo tembea kwa mwendo wa madoido kana kwamba si komandoo, ila uzuri ninao upendea kutoka kwa Aron ni jinsi alivyo makini katika swala zima la utendaji wake wa kazi na siku hata moja hakubali kushindwa kwa kitu chochote anacho hisi anaweza kukimudu. Nikaendelea kunywa mvinyo wangu taratibu huku nikiwatazama watu wakionyesha vipaji vyao kwenye jukwaa, kabla ya mziki kufunguliwa na watu kujiachia hadi asubuhi.
“Katika shindano letu la kuimba leo, tunamleta kwenu Captain Adrus Maldin, na akishindwa kuimba atatupa dola elfu kumi hapa hapa” Muendesha matukio(MC), alizungumza huku akinitazama na kunifanya nistuke kwani sikutegemea kwamba anaweza kunihusisha katika tukio hilo. Watu wakaanza kushangilia wakinitaka niende mbele. Aron kwa haraka akanifwata na kunishika mkono. Akanipeleka mbele ya jukwaa kisha yeye akanikimbia na kubaki mwenyewe.
“Una dola elfu kumi ya kuitoa au unaweza kutuimbia?”
“Sina ngoja niimbe” Nikakabidhiwa kipaza sauti(Maiki). Nikachukua moja ya gita, kisha nikasimama katikati ya jukwaa.
“Munataka kusikia wimbo gani?”
“Wowote” Walijibu kwa nguvu huku wengine wakisema wanahitaji wimbo wa wasanii wanao wahitaji wao.
“Ok basi nitaimba wimbo Adele uitwao Hello” Nilizungumza huku nikizivuta vuta nyuzi za gitaa hili la umeeme, lenye kutoa sauti kubwa ya kila mtu kuweza kuisikia kwa umakini.
(Hello, it's me I was wondering if after all these years you'd like to meet To go over everything They say that time's supposed to heal ya But I ain't done much healing Hello, can you hear me? I'm in California dreaming about who we used to be When we were younger and free I've forgotten how it felt before the world fell at our feet There's such a difference between us And a million miles Hello from the other side I must have called a thousand times To tell you I'm sorry for everything that I've done But when I call you never seem to be home Hello from the outside At least I can say that I've tried To tell you I'm sorry for breaking your heart But it don't matter. It clearly doesn't tear you apart anymore Hello, how are you? It's so typical of me to talk about myself. I'm sorry I hope that you're well Did you ever make it out of that town where nothing ever happened? And it's no secret that the both of us Are running out of time So hello from the other side (other side) I must have called a thousand times (thousand times) To tell you I'm sorry for everything that I've done But when I call you never seem to be home Hello from the outside (outside) At least I can say that I've tried (I've tried) To tell you I'm sorry for breaking your heart But it don't matter. It clearly doesn't tear you apart anymore [4x:] (Highs, highs, highs, highs, Lows, lows, lows, lows) Anymore Hello from the other side (other side) I must have called a thousand times (thousand times) To tell you I'm sorry for everything that I've done But when I call you never seem to be home Hello from the outside (outside) At least I can say that I've tried (I've tried) To tell you I'm sorry for breaking your heart But it don't matter. It clearly doesn't tear you apart anymore)
Nikiwa nina malizia kuuimba wimbo huo ulio vuta hisia za watu wote ukumbini walio kaa kimya kunitazama na kunisikiliza kwa umakini. Macho yangu yakaangukia kwa dada mmoja aliye nivutia sana baada ya kumuona akiwa katikati ya wezake walio kaa kwenye meza iliyo jaa vinjwaji. Dada huyo ambaye macho yetu yaligongana akanyanyuka kwenye kiti alicho kalia na kuanza kapiga makofi, watu wote ukumbini nao wakapiga makofi na wengine wakishangilia kwa shagwe. Kila mmoja hakuamini kwamba ninaweza kuimba kwa uwezo mkubw sana na sauti nzuri ya kuvuti, kwa maana hapakuwa na mtu aliye weza kugundua kwamba mimi nina kipaji cha uimbaji. Nikashuka kwenye jukwaa na kila mtu akawa ananipongeza kwa uwezo wangu mzuri wa kuimba, nikarudi kukaa kwenye kiti nilicho kuwa nimekaa, huku macho yangu kwa wakati wote nikimtazama tazama msichana ambaye nilikuwa ninatazamana naye nikiwa jukwaani.
Nikamuona msichana huyo akinyanyuka akieelekea kwenye moja ya kaunta za vinywaji zilizomo ndani ya huu ukumbi, taratibu nikachukua chupa yangu ya mvinyo na kuanza kupiga hatua kwenda aliopo simama.
“Mambo” Nilianza kumsalimia, akageuka na kunitazama
“Safi tuu za kwako” “Salama, ninaitwa Adrus wewe je?” “Sporah”
“Ahaa, unajina zuri. Sijui niaweza kupata muda wa kuzungumza na wewe japo kidogo” “Mmmm kidogo nipo na rafiki zangu, ila ngoja niwapelekee vinywaji vyao kisha nitakuja kuzungumza na wewe”
“Sawa mimi nipo kwenye kaunta ile pale” “Ahaaa sawa”
Nikarudi kwenye kaunta niliyo kuwa mara ya kwanza, moyo wangu ukawa umejawa na furaha sana kwani kila nilipo mtazama binti huyu mwili wangu ulisisimka sana. Nikaendelea kushusha mvinyo taratibu, nikamshuhudia binti yule akiwaaga wezake na kuja katika sehemu nilipo mimi, akiwa ameshika kinywaji chake mkononi. Nikamuwekea kiti kilicho kuwa pembeni na akakaa huku akinitazam usoni mwangu akiachia tabasamu pana.
“Unamejitahidi kuimba, una sauti nzuri”
“Asante sana, ila na wewe umependeza sana”
“Asante” Nikabaki nikimtazama Spora jinsi alivyo barikiwa macho makubwa kiasi yaliyo pambwa na kope ndefu kiasi, huku nyusi zake zikiwa nyingi kiasi na nyeusi tii. Midomo yake midogo na minene kiasi aliyo ipaka rangi nyekundu, ikazidi kunipandisha hisia za kimapenzi. Kifua chake kilicho jazia chuchu nene kiasi, amabazo nimeweza kushuhudia mstari ulio zigawanya chuchu hizo kwa kupitia kanguo kake alicho kavaa juu, chenye kola ya duara.
“Hei…mbona upo kimya?” Spora alinistua mara baada ya kuniona nikiwa ninamshangaa kwa muda mrefu. Sauti yake ilizidi kuniua kabisa kihisia, kwani ilibarikiwa kuwa nyembamba na yakubembeleza, unaweza kusema kwamba si mwanajeshi.
“Eeheee!!!” Nilibaki nikiwa nimebabaika nisijua ni nini niweze kumjibu Spora aliye kaa mbele yangu. Spora akauleta mkono wake wa kulia na kuukutanisha na mkono wangu wa kulia, hapa ndipo hali ya msisimko ilivyo zidi kuongezeka hadi sehemu zangu za siri nikaanza kujihisi ugumu fulani wa mpingo wangu ulio taka kusimama kidedea.
“Adrus vipi mbona hivyo” “Haa….haaa kun..a” “Basi ngoja mimi niondoke”
“Ehee usiondoke”
“Sasa nimekuja kuyasikiliza hayo mazungumzo, ninaona upo kumya”
“Nataka nikakuonyeshe kitu nje” Nikamshika Spora mkoo na kutoka naye nje ya ukumbi, tukaelekea hadi kwenye moja ya mti mkubwa uliopo kwenye uwanja wetu wa mazoezi, tukaka chini na kuitazama bahari iliyopo mbele yetu, japo ipo mbali kidogo na tulipo sisi
“Ukitazama juu angani unaona nini?”
“Nyota na mwezi”
“Unazioona zile nyota tau juu angni?” “Ndio”
“Basi baba yangu alisha wahi kuniambia kwamba. Nyota zile zinaashiria familia yaani, ile iliyo tangulia ni baba, na ile iliyo fwatia nyuma ni mama na ile ya katikati ni mtoto” Spora akatabasamu na kunifanya niweze kuuona uzuri wake vizuri, Spora akanitazama kwa macho yenye kuhitaji kitu fulani, kwa haraka nikausogeza mdomo wangu karibu na ulipo mdomo wake, kabla mdomo wangu haujakutana na mdomo wangu, akaukwepesha mdomo wake akishiria, haitaji nimbusu mdomoni mwake.
ITAENDELE
No comments:
Post a Comment