MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Thursday, 25 May 2017

PRESIDENT‘s WIFE 02. (MKE WA RAISI)


ILIPOISHIA
Nikamshika Spora mkoo na kutoka naye nje ya ukumbi, tukaelekea hadi kwenye moja ya mti mkubwa uliopo kwenye uwanja wetu wa mazoezi, tukaka chini na kuitazama bahari iliyopo mbele yetu, japo ipo mbali kidogo na tulipo sisi
“Ukitazama juu angani unaona nini?”
“Nyota na mwezi”
“Unazioona zile nyota tau juu angni?” “Ndio”
“Basi baba yangu alisha wahi kuniambia kwamba. Nyota zile zinaashiria familia yaani, ile iliyo tangulia ni baba, na ile iliyo fwatia nyuma ni mama na ile ya katikati ni mtoto” Spora akatabasamu na kunifanya niweze kuuona uzuri wake vizuri, Spora akanitazama kwa macho yenye kuhitaji kitu fulani, kwa haraka nikausogeza mdomo wangu karibu na ulipo mdomo wake, kabla mdomo wangu haujakutana na mdomo wangu, akaukwepesha mdomo wake akishiria, haitaji nimbusu mdomoni mwake.

ENDELEA
“Adrus hatuwezi kulifanya hilo jambo kwa muda huu”
Spora alizungumza kwa sauti ya chini, huku akinijiweka vizuri nguo yake.
“Kwa nini?”
”Nina mchumba wangu, ninampenda sana naye ananipenda sana. Siwezi kumsaliti katika hili”
Spora alizungumza kwa kujikaza sana, mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio, huku nikihisi hali fulani ya maumivu ikikatiza katika ya moyo wangu.  Katika miasha yangu sikuwahi kuwa na mwanamke wa aina yoyote na wala sikuwahi kushiriki swala lolote kuhusiana na mapenzi, hii ni kutokana na muda wangu mwingi niliutumia katika masomo ili malengo yangu haya niliyo kuwa nimejiwekea kuweza kuyatimiza. Haliya kumpenda Spora ilinikumba gafla huku nikiamini kwamba nitampata. Ila kwa jibu alilo nipa, limeweza kunikatisha matumaini ya kuwa naye, huku yakinipa maumivu makali moyoni mwangu.
“Adrus, natambua kwamba una hisia fulani juu yangu, ila ni vyema kuweza kuzungumza mapema kwamba ninaye mtu ninaye mpenda. Kuliko ningekukubali alafu yangetokea matatizo hapo mbeleni.”
“Isitoshe mtu huyo anacheo kikubwa kuliko wewe katika hichi chuo unacho kisoma” “Ni nani huyo?”
Spora akaka kimya huku akinitazama machoni mwangu. Akashusha pumzi nyingi na kunijibu nililo muuliza.
“Ni mkufunzi wenu wa mafunzo bwana Dismas Santos”
Nikajikuta nikistuka sana, kwani bwana Dismas Santos ni mtu mzima mwenye umri si chini ya hamsini na tano. Mbaya zaidi ni moja ya waalimu walio tokea kunichukia kutokana na mimi kupenda kutetea haki za wezangu kwa kipindi chote tukiwa mafunzoni. Siku nyingine ilinilazimu kuwasaidia wezangu azabu, wanazo pewa na mkufunzi huyo ambaye karibia asilimia tisini ya wahitimu, tunamchukia sana kwa vitendo vyake vya unyayasaji na roho mbaya hususani kwa wanaume isitoshe yeye ndio msababishaji wa wanachuo wengi kufariki kwa ajali nyingi ikiwemo kulipuliwa na mabomu ya kutega na wengine kuanguka kwenye makarongo makubwa pale tulipokuwa tunapita kwenye kamba zilizo fungwa juu ya mlima mmoja kwenda mlima mwengine na chini ni mbali sana na endapo mtu anaanguka basi biashara yake ya kuishi duniani inakwisha kabisa.
“Mbona umestuka?” “Hapana, kawaida”
“Sawa ngoja mimi niende ndani kwa maana akitukuta hapa inaweza kuwa matatizo”
“Sawa”
Spora akanyanyuka na kuondoka, nikabaki peke yangu nikiendelea kutazama, nyota angani. Hamu ya kuendelea kusherekea ukumbini ikaniishia kabisa, moja kwa moja nikanyanyuka nikaelekea chumbani kwetu ambapo, tunaishi mimi na Aron. Nikafungua mlango pasipo kubisha hodi, nikamkuta Aron akiwa anafanya tendo la ndoa na msichaa aliye kuwa amenionyesha kipindi walipo kuwa wanaingia wasichana wale ukumbini.
“Samahani” Nikafunga mlango na kutoka nje, nikawaacha waendeleaa na mambo yao. Ili kupoteza poteza muda nikaamu kurudi ukumbini. Kabla sijafika ukumbini nikamuona Spora akiwa ameongozana na Sir Dismas Santos kwenye moja ya ofisi ya mzee huyo. Nikaanza kuwanyatia pasipo wao kujua, wakaingia kwenye ofisi hiyo na kufunga mlango, nikazunguka upande wa pili wa ofisi kwenye dirisha, kwa kupitia uwazi mdogo wa dirisha nikamuona bwana Dismas Santos akimshuhulikia Spora kisawa sawa. Kusema ukweli mayo wangu ulizidi kujisikia vibaya, na kuanza kuzilaumu hisia zangu kwa nini, zimependa kwa mwanamke ambaye tayari amesha pendwa tena na mtu ambaye ni adui kwa upande wangu. Jambo lililo zidi kuniumiza moyo wangu, ni pale nilipo muona Sir Dismas Santos akimlazimisha Spora, kufanya naye mapenzi kinyume na maumbile. Japo kwa mara ya kwanza Spora aliweza kukataa, ila akazidiwa kwa utamu wa maneno na kujikuta akikubali kufanya kitendo hicho.
“Shitiii”
Nilizungumza kwa sauti ya juu hadi Sir Dismas Santos akageuka na kutazama dirishani. Nikakimbia na kuelekea kwenye chumba chetu kilipo, nikausukuma mlango pasipo kugonga hodi nikamkuta Aron akiwa na msiichana yuleyule niliye muacha naye humo chumbani, wakiendelea kufanya mapenzi huku wakionekana kufurahia mechi hiyo wanayo ipiga kwa juhudi zote huku jasho likiwamwagika wote wawili.
“Sorry”
Nilijisemea kwa aibu huku nikurudi kinyuma nyuma na kuufunga mlango wa chumba chetu na kuwaacha waendelee na mambo yao. Sikuwa na jinsi zaidi ya kurudi ukumbini, kuendelea na kutazama wezangu wakicheza mziki huku moyoni nikizidi kuumia kwa kumkosa Spora.
                                                                                        ***
    Kama kawaida asubuhi na mapema tukaendelea na mazoezi ya viungo ikiwemo kukimbia mchaka machaka, tukamaliza mazoezi hayo na sote tukaingia kwenye ukumbi wa jeshi kama ari ilivyo toka kwa mkuu wetu wa chuo. Tukasimama kwenye mistari iliyo nyooka, akasimama mbele yatu na kuanza kuzungumza.
“Tusikilizane kwa pamoja. Tumepata kazi ambayo inatuchukua siku tisini kuweza kuimaliza.” “Kazi hiii ni nje ya nchi hii, na inatupasa kwenda nchini Pakistani na Lebanon kuweza kuzuia vikundi vya kigaidi vinavyo endelea kutikisa katika nchi hizo”
Kusikia majina ya nchi hizo mbili nikajikuta nikishusha pumzi nyingi, kwani huko tuendapo uhakika wa kurudi salama ni mdogo kupindukia kwani ni mara nyingi huwa tunafwatilia baadhi ya taarifa za habari wanatueleza jinsi majeshi ya umoja wa mataifa yanavyo teketezwa katika na vikundi hivyo vya kigaidi, ikiwemo kundi  tishio la Al Qaida ambalo linaongozwa na kiongozi wake mpya bwana Ayman Al-Zawahir, aliye ingia madarakani mwaka 2011 baada ya kiongozi wao muanzilishi Osama bin Laden kuuawa na majeshi ya Marekani mnamo mwaka 2011.
“Mutajiunda kwenye makundi mawili ya watu hamsini hamsini, moja litakwenda Lebano jengine litakwenda Pakistan” “Hiyo kazi itafanywa na mwalimu wenu wamafunzo Sir Dismas Santos. Kumbukeni munakwenda kuongeza nguvu kwenye majeshi yaliyopo huko, ninawahitaji wote murudi mukiwa hai na sihitaji hata mmoja kati yenu kuweza kupoteza maisha” Mkuu wa chuoa alizungumza na kumpisha Sir Dismas Santos kufanya kazi aliyo kabiziwa kuifanya, akanza kutugawa kwenye makundi ya watu hamsini hamsini kwa bahati nzuri nikafanikiwa kuwa kundi A pamoja na rafiki yangu Aron, ambaye ni Mtazania mwenzangu. Kila kundi likaombwa kuweza kumchagua kiongozi wao mkuu na msaidizi, katika kundi langu hawakuwa na mtu mwengine wa kumchagua zaidi yangu. Tukapewa muda wa kuweza kuandaa vifaa vya kwenda navyo huko tunapo kwenda huku kundi letu likichaguliwa kwenda nchini  Pakistan.
“Hivi Aron unajua kwamba yule mzee ni muovu sana?” “Mzee gani?” “HuyoDead Men Dismas”
Nilitanguliza jina la utani ambalo tumezoea kumita Sir Disma, linalo maanisha mtu mfu. “Amefanyaje?” “Jana, nimemkuta akimla kiboga yule demu Sporah” “Spora…..ndio yupi huyo” “Kati ya wale mademu walio kuja jana, si kuna demu fulani hivi, kama uliniona nimekaa naye” “Mmmm hapana mimi niliwahi kuondoka na yule demu, eheee ikawaj……” Sote tukajikuta kukiaa kinya na kumtazama Sir Dismas, akija katika sehemu yetu tulipo, simama tukiendelea kusafisha safisha bunduki zetu kwa ajili ya safari inayo anza usiku.
“Nifwate ofisini kwangu” Sir Dismas Santos alizungumza kwa sauti nzito, huku akionekana kuwa kama mtu aliye kasirishwa na jambo fulani. Akatangulia na mimi nikamfwata nyuma, tukafika ofisini kwake moja kwa moja akaenda kukaa kwenye kiti chake na mimi nikasimama huku mikono yangu nikiwa nimeiweka nyuma kama kanuni ya jeshi inavyo agiza mtu unapokuwa unazungumza na mkuu wako, ni lazima kusimama mguu sawa huku mikono yako ikiwa nyuma au umeibananisha kwenye mbavu.
“Jana ulifwata nini dirishani kwangu?” Swali la Sir Dismas Sanstos lilinistua ila nikajikaza kuweza kuupoteza mstuko huo ambao ili asiweze kugundua haraka
“Sio mimi, Sir” Nilijibu kwa sauti ya juu na ya ukakamavu
“Unataka kunifanya mimi ni mtoto mdogo si ndio?” “Hapana, Sir”
“Sauti yaki Adrus ninaijua, hata nikiwa nimelala ninaitambua kwa nini unabisa?”
Sir Dismas alizungumza kwa hasira kali huku akinitazama na macho yake makubwa ambayo ni mekundu muda wote hii ni kutokana na pombe kali anazo kunywa pamoja na bangi anazo vuta kisirisiri ila ni baadhi ya wahitimu ndio tunafahamu uvutaji wake wa bangi.
“Sio mimi Sir”
“Sasa nitahakikisha haurudi hapa, utakwenda kufia huko huko Pakistani, pumbavu sana. Toka ofisini kwangu kabla sijakupasua ubongo wako” “Asante, Sir”
Nikapiga sauluti kama heshima na kugeuka nyuma na kuondoka, maneno ya Sir Santos yakaanza kuniumiza kichwa changu na kujikuta nikipoteza furaha yangu yote.
“Vipi mbona umekua mnyonge gafla?” Aron aliniuliza mara baada ya kurudi sehemu nilipo muacha
“Jamaa ameniambia lazima nife huko Pakistani” “Mmmm, ila unajua nini Adrus, wewe potezea hawezi kufanya kitu kama hicho”
“Ahaa simuamini huyu dead men, ni mtu ambaye maneno yake hayapindi. Si una ona amewaambia watu wengi watakufa, na wamekufa kweli”
“Kufa kupo kama kazi yetu inavyo sema. Ila kama kuna mpango anataka kuufanya ili ufe ni lazima kuuzuia” “Mbaya amegundua sauti yangu na anadai hata akiwa amelala akiisikia ni lazima aijue?” “Hahaa anakutisha tu, ila si umekana?”
“Ndio” “Kabla hatujaondoka nitakuwa nimefanya upelelezi wa kujua ni kitu gani ambacho anahitaji kukifanya juu yako” Aron alinifariji, tukaendelea kuchagua bunduki na risasi ambazo zitatutosha huko tunapo elekea, kila mtu akaviweka vifaa vyake kwenye mabagi makubwa ya mgongoni huku tukisubiria muda wa saa nne usiku kufika tuweze kuondoka.
Masaa yalikwenda kasi sana, kwani saa nne usiku ikawadia, na kutukuta tukiwa kwenye uwanja wa ndege wa chuo chetu, tukaagana na wezetu ambao wanaelekea Lebanon, kisha kila watu wakaingia kwenye ndege yao na safari ikaanza. Katikati ya safari nikasimama katikati ya nafasi iliyo tengenisha siti za kulia na kushoto za ndege hii ya kivita tuliyo panda.
“Habari, sote tunatambua ni wapi tunapo elekea, si sehemu salama ila kwa umoja na ushirikiano wetu tunaimani tutarudi tukiwa wazima na hakuna mmoja wetu ambaye anaweza kupotea kwenye mikono ya hao magaidi.” “Tutafikia kwenye uwanja wa Shamsi Airfield, ambapo tutapokelewa na mkuu wa kikosi cha anga cha jeshi la Marekani pamoja na mkuu wa kambi hiyo ya jeshi” “Kikibwa ni upendo, umoja, ushirikiano, na kulindana. Nilinde mimi nami nitakulinda wewe” Maneno yangu, yaliwapa moyo  wa matumaini wezangu na kuwafanya washangilie kwa furaha kwani kabla ya kuzungumza hayo maneno ukimya ulitawala ndani ya ndege na kila mmoja alikuwa kimya akiwazia hatima ya maisha yake itakuwaje, japo mimi ni mdogo kiumri kupita wahitimu wote, ila wananipenda sana na kuniheshimu. Nikarudi kukaa kwenye siti yangu ambayo pembeni yake yupo Aron. 
Ndani ya masaa, nane, rubani akatutangazia kwamba tufunge mikanda kwani tunakaribia kutua kwenye kiwanja tunacho paswa kutua. Kila mmoja akafanya hivyo, ndani ya dakika kadhaa ndege ukiaanza kushuka chini taratibu, kwa kupitia kioo cha pembeni yangu nikashuhudia magari mengi ya kijeshi yakiwa katika kambi hii inayo onekana kuwa ni kubwa sana na ina vifaa vingi vya kijeshi. Ndege ikatua kwenye ardhi, ilipo simama sote tukashuka huku mimi kama kiongozi nikiwa nimetangulia mbele, begi langu kubwa likiwa nimelivaa mgongoni mwangu. 
Tukawakuta viongozi wa jeshi pamoja na wanajeshi wengien wakitusubiria, wakatupokea, huku nikiwa na kazi ya kumtambulisha mmoja baada ya mwengine, nao pia wakafanya kazi ya kujitambulisha kwetu.
Tukapelekwa kwenye moja ya holi ambalo linavitanda vingi, tukaambiwa hapo ndipo sehemu ambayo tutapumzikia, na kesho asubuhi tutaingia kazini rasmi.
Kila mmoja akaendelea kufanya anacho jisikia ili mradi kuweza kujiandaa kwa ajili ya kazi iliyopo kesho asubuhi. Sikutaka kujisumbua sana zaidi ya kulala kwenye kitanda changu, huku tumbo langu likiwa limeshiba kutokana na chakula nilicho kula ndani ya ndege.
                                                                                            ***
    Alfajiri na mapema tukaamka, kila mmoja akajiandaa. Mwenyeji wetu akaja kutuchukua nakutupeleka kwenye uwanja  mkubwa ndege ambapo tukakuta Helcoptar si chini ya ishirini zikitusubiria, huku kukiwa na wanajeshi wengine wa Marekani pamoja na Pakistani. Sote tukaingia kwenye helcoptar hizi, tukichanganyikana na wenyeji wetu, na taratibu zikaicha ardhi. Nilipo kaa mimi pembeni yangu kuna msichana mrembo, aliye changanyia kati ya mzungu na mufrika huku kwenye nguo yake ya jeshi aliyo ivaa kuna bendera ndogo ya marekani. Ukimya ukatawala ndani ya Helcoptar yetu, huku kila mmoja akiwa ameshika bunduki yake kwa umakini mkubwa, huku sote tukiwa tumevalia majaketi ya kuzuia risasi pamoja na makombati yanayo fanana, ila yetu kidogo yana utofauti wa chata kwenye mabega yetu ya kushoto yana bendera ya kijani na nyekundu na chini kuna maandhishi madogo ya P.S.S.
“Unatumia choclate?” Binti huyo aliniuliza huku akiwa ametoa choclate mbili mfukoni mwake
“Hapana” Akairudisha moja aliyo kua amekusudia kunipa mimi, kisha akaendelea kuila aliyo itoa, tukiwa katikati ya safari gafla tukasikia mlipuko mkubwa na mtingishiko mkali, jambo lililo ifanya helcoptar yetu kuyumba huku ikanza kuzunguka hewani ikionyesha kupoteza dira.
                                                                                              ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 3 YA STORI HII YA KUSISIMUA

No comments:

Post a Comment