MATUMIZI SAHIHI YA GIA
Katika gari za AUTOMATIC kuna gia za *L, 2, 3 na O/D*
Kwanza ujue kabisa katika hali ya kawaida gari yako inapaswa kuwa katika ‘’D’’ kwa maana ya ‘’DRIVE’’ na hii inategemeana na mazingira ya barabara na hali yali ya hewa kama ni nzuri ila *2, 3* hutumika tu pale unapokuwa either unashuka au unapanda mlima/mteremuko mkali sana na mrefu mfano sekenke na unataka ushuke au upande kwa speed ile ile ila isizidi 40/60 basi ndo unaruhusiwa kutumia *2, 3*
Namba *2, 3 na L* inamaana kuwa ina inalock gear box ili gear zisibadilike (-/+) kama ambavyo zinabadilika ukiweka *D* na itambulike kuwa unaweza kubadili toka *D* kwenda *2 au 3* wakati wowote gari inapokuwa katika mwendo ila hakikisha usiwe speed zaidi ya 40/60 maana kinachofanyika ni kwamba *D* inasababisha sahani (disks) zilizomo ndani ya gearbox kufanya kazi na hii hupelekea ile hydrolic iliyomo kupata joto linalotoka katika zile sahani ambalo joto lile husababisha gear box kutokuwa na nguvu ile ile (constant velocity) na ndo maana ukiweka *2, 3 au L* gear box inakuwa kwenye lock na sahani hazisuguani maana inakuwa inatumika sahani/disk moja tu kwa hiyo inasaidia ile hydrolick kupoa pia na ndo maana gari huongeza nguvu kwa ghafla.
*L* inatumika pale unapokuwa either umekwama au unavuta gari jingine au tera ila inapaswa itumike kwa muda mfupi sana maana inanguvu sana na pia inaongeza ulaji wa mafuta, so kama ukiishatoka katika mkwamo na unaona bado barabara si nzuri labda utelezi au unavuta mzigo kwa mwendo mrefu basi unaweka *2 au 3* na wakati huohuo unaweza kuweka hata *D* kama hali ya njia na mzigo vinaruhusu na unaweza kuongeza walau speed 40/60 au zaidi kama utaweka *D* kwa maana rahisi zaidi kwamba *2,3,na L* inafanya kazi kama gari ya Manual na hii inakuwa rahisi kwa yeyote ambaye anafahamu kuendesha manual.
OVER DRIVE (OD) inatumika pale gari inapokuwa speed zaidi ya 60/80 kutegemeana na aina ya gari na hili hutokea bila wewe kujua maana gari yenyewe ndo inafanya ndio maana unashauriwa iwe ON muda wote kusudi gari ichague ni wakati gani iweke on au off maana ukiwa chini ya 60/80 hata kama umeweka on bado inakuwa haifanyi kazi.
OD unaweza kuitumia kama break/stop engine hasa unapokuwa zaid ya 80 na wakati huo iko ON yaan katika dashboard taa ya OD izime ikiwaka maana yake iko OFF, basi ili upunguze mwendo kwa haraka unachofanya ni kuweka OFF na wakati huo unakanyaga break taratibu utaona gari linavyopunguza mwendo taratibu na wakati mwingine si lazima ukanyage break, we iweke OFF tu halafu toa mguu katika pedal ya mafuta gari lazima li slow down na kama lilikuwa ni tuta na umeshalipita basii iweke tena ON ongeza mafuta au unaweza kuweka *2 au 3* ili gari ianze kwa kasi zaidi na ikiisha changanya basi rudi kwenye *D* na endelea kama kawaida.
*Tahadhari:* Kamwe usikate kona wakati uko speed kubwa na gear namba tano (Kwa MANUAL) au rpm iko 3000 (Kwa AUTOMATIC) hii husababisha kupitiliza maana gari inakuwa nyepesi sana.
Hakikisha ume slow down mpaka gia namba nne na break kidogo na Kwa AUTOMATIC either uweke *2* au *3* ila lazima weka OD iwe OFF na break kidogo.
No comments:
Post a Comment