MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Tuesday 22 August 2017

WORLD CUP 2022: VIWANJA VYA QATAR SI MCHEZO NI KANDANDA NA VIVUTIO

 Umm Salal Stadium utakuwa ni uwanja wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 45,120. Uwanja huu umebuniwa katika mila ya ngome za kiarabu. Baada ya World Cup 2022, uwanja huu utatumika na klabu ya Umm Salal FC kama uwanja wao wa nyumbani.
 Sports City Stadium ni uwanja ambao nao utajengwa maalum kwa kombe la dunia in 2022. Utakuwa mjini Doha Qatar. Utakuwa na uwezo wa kuingiza watu wasiopungua 42,000. Uwanja huu utakuwa na teknolojia ya hali juu ya kupambana na hali ya joto kubwa liliopo katika nchi hiyo.
 Lusail Iconic Stadium, ni uwanja ambao utajengwa hapo baadae katika mji wa Lusail. Huu ndio uwanja utakaotumika kwa ajili ya mechi za ufunguzi na fainali za World Cup 2002. Uwanja utajengwa kwenye maji na utakuwa umeunganishwa na madaraja 6 ambayo yatakuwa yakielekea uwanjani. Umebuniwa na Waingereza wajiitao Foster + Partners.
 Education City Stadium, ni uwanja ambao utajengwa mjini Doha -Qatar, kwa ajili ya World Cup 2022.

 Uwanja huu unaitwa AL-Khor utakuwa unaingiza watu wapatao 45,000, pamoja na siti nyingine za ziada 1000 kwa ajili ya waandishi wa habari. Pia utakuwa na parking ya kuhimili magari 6,000, mabasi 350, pia sehemu ya kuingia na kutoka ya mabasi ya abiria yapatayo 150 kwa wakati mmoja. Pia kutakuwa na sejhemu ya kuweza kupaki taxi 1000 za kawaida na  za kupita majini (Baharini).
 Uwanja huu utaitwa Doha Port Stadium, unajengwa maalum kwa ajili ya michuano ya World Cup 2022.
 Uwanja wa Ahmed bin Ali, maarufu kama Al-Rayyan Stadium - ni uwanja ambao unatumika katika vingi. Pia ni uwanja unaotumiwa na klabu Al-Rayyan Sports Club na Al-Kharitiyath Sports Club. Uwanja huu ulijengwa 2003 na una uwezo kuingiza watu 21, 282. Lakini uwanja huu utatengenezwa upya kwa ajili ya World Cup 2022, na kuweza kuingiza watu 44,740.
Uwanja wa AL-Wakrah ni uwanja unaotumika kwa michezo mingi katika mji wa Al Wakrah, Qatar. Kwa sasa unatumika zaidi kwa ajili ya kuchezea soka. Uwanja huu unachukua watazamaji 20,000 lakini utatengenzwa na kuweza kuchukua watazamaji 43,500

No comments:

Post a Comment