MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Sunday 10 September 2017

ALFA BLOG KUWALETEA ELIMU MBALIMBALI KUHUSU MAGARI NA VYOMBO MBALIMBALI VYA USAFIRI KWA WATANZANIA

[​IMG] [​IMG] 
 [​IMG] [​IMG] [​IMG]
 
HIZI NI PICHA ZA MAGARI MBALIMBALI.  PIA MAANDISHI HAYA SI SHERIA HIVO YANAWEZA BADILIKA KILA SIKU KUTOKANA NA MAENDELEO YA TEKNOLJIA YA KILA SIKU 
 HIVO tunachangiana mimi pamoja na jamiii nzima yale ninayopata kupitia mitandao yani internet sources na elimu ninayo ipata darasani kupitia fani yangu ya automobile engineering maoni yako na nyongeza yako kwangu na jamii yote ni tunu muhimmu sana ili tuweze kufika mbali kwenye upande wa magari na vyombo vingine vya usafiri kwote nchini hassa kwenye ulimwengu wa sayansi na teknolojia
kwa maoni 
alfachengula94@gmail.com 
au
0754220454
facebook ALFA BLOG



UUNDWAJI WA MAGARI TARATIBU, HATUA NA MAKAMPUNI SHIRIKISHI


Mada hii ni kwa ajili ya kusahihisha wanaosema kuna magari ambayo yameundwa tokana na rejected material, hii ni kwa sababu ya kukosa elimu na uelewa wa uundwaji magari unavyofanyika. Hakuna gari inayoundwa kutokana na rejected parts or material, bali huundwa kwa mtiririko wa kila gari kadiri ya 
engineer walivyobuni magari ghali na ya gharama nafuu kadiri ya hitaji la watumiaji.

Mamia ya makampuni hushiriki uundwaji wa gari
Gari haiundwi na kampuni moja ya uundwaji magari, kampuni yenye hati miliki ya gari ndio wanaobuni, design body, engine, na parts zote za kila aina ya gari litakaloundwa na kampuni yao.

Tenda hutangwazwa kwa car manufacturing agents toka makampuni mbalimbali, yanayotengeneza car seat, belts, tires, transmission, mirrow, radios, DVDs, locks, ignition, lights, metal or plastic tubes, electronic units, filters, engine, radiators, etc.

Mfano wa sehemu za uundwajiwa gari naleta huu wa car seat assembling.


Car seat manufacturing processing
Parts hizo haziundwi na makampuni hayo pekee, kwani ni kazi inayohitajika umakini na haraka, hivyo kuna makampuni kadhaa yanayoshirikiana mfano kuunda car seat yapo utitiri.
  • Kampuni ya kuchimba madini ya chuma.
  • Kampuni kuyeyusha chuma na kufanya iwe katika muundo wa steel slit sheet coils, flat slit sheets and solid iron (nondo).
  • Kampuni ya tube forming, tube parts forming, trimming, end finishing and shaping.
  • Kampuni ya seat foam maker.
  • Kampuni ya kushona mifuko ya vitambaa, plastic au ngozi kwa ajili ya kufunika seat.
  • Kampuni ya kutengeneza coil springs kwa baadhi ya car seats.
  • Kampuni ya kutengeneza vipande vya car seat, left, right, bottom and back of the seat.
  • Kampuni ya kuunganisha car seat, kupiga pasi na kukagua kwa computer ubora wake kisha kusafirisha kwenda car manufacturing plant.

Haya hufanyika kwa car seat hatua hizo, na hivyo kila aina ya parts na sehemu za gari hufanywa kwa utaratibu huo, hivyo unaona ni hatua nyingi na makampuni mengi sana yanayohusika katika uungwaji wa magari.

Hakuna share kwa makampuni ila kuuziana zana
Utaratibu wa makampuni yanayohusika katika uundaji zana za magari hayana share kwenye kampuni inayounda magari, bali huuza parts zao kwa kampuni husika. Utaona kampuni nyingine zinafanya shughuli zao za uzalishaji wa zana za magari kwa makampuni tofauti tofauti za magari. Mfano watengenezaji wa Car seat utaona kuna kampuni ambayo inafanya kazi zao kwa ajili ya Toyota, Honda, IBM, nk ndio maana tunaona wakati wingine kuna kufanana kwa car seat. Watenenezaji wa radio, DVD, nk huzalisha zana zao kwa makampuni mbalimbali iwe magari, meli, ndege, bodaboda, nk.

Car manufacturing plant
Plant ya kuunda magari shughuli zao ni kuunganisha gari tokana na parts ambazo zimekuwa supplied toka makampuni mbalimbali kadiri ya maelekezo ya kampuni yao ya engineering production assembly unit. Huwa wanakuwa na agents wao wambao huhakiki ubora wa part na zana mbalimbali kwenye makampuni yanayotengeneza zana za magari yao.

Chases na body za magari huundwa kwenye main car manufacturing plant. Kwa ajili ya perfect parts fit hufanywa kwa robotical interface processing system. Kwa utaratibu huo kama kuna part ambayo haifai na inakuwa rejected hupelekwa re-circling company ambao huyeyusha na kuwa chuma ghafi tayari kuundwa part nyingine. 

Part ikishakuwa rejected haiwezi kufaa kwa aina yo yote katika gari maana kila aina ya gari hata tuyaonayo ya bei nafuu yamekuwa computerized na yameundwa kwa utaratibu huo.

Chase ya gari hutembea kwenye reli huku waunganishaji wamejipanga pamoja na robot kuunganisha kwa kasi sana. Mfano kuna plant kubwa ambazo ndani ya 24 hr huunda magari mapya wastani wa 1000.

Katika line za kuunganisha magari kuna kila aina za magari zimechanganyika, mfano kama ni Toyota, litakuja Vitz, litafuata Corolla, litafuata Mark II nk. Kuna line ya truck, yaani magari kama yale makubwa ya Land cruiser, Highlander, Pic ups nk. Huwa kuna line production mbili moja ya car (tumezoea kuita salon) na line ya trucks.

Baada ya gari kutengenezwa hupitia kitengo cha ukaguzi ambao hutumia eye vision, caliper, vifaa vingine na kuhitiishwa kwenye compartment ya computer cage kuhakiki gari kama limekamilika na kama hakuna kasoro. Kisha anakabishiwa drive stadi to test kabla ya kuwekwa kwenye yard tayari kupelekwa kwa car dealers.

Huu ndio utaratibu wa uundwaji wa magari

HIZI BAADHI YA MAMBO AMBAYO HUZINGATIWA WAKATI WA KUTENGENEZA GARI
[​IMG]

[​IMG]
 FIKIRIA
Utilize free thinking and
the ability of young employees to
create future visions.

[​IMG]
Reviewing of car design concepts.
[​IMG]

[​IMG]
KIWE VIPI
Highly refined exterior and interior design.

[​IMG]
Accurate three-dimensional design images.
[​IMG]

[​IMG]
BODI YA GARI IWE VIPI
Resolve technical issues and

create drawings for each part.
[​IMG]

[​IMG]
TADHIMINI YA ULIVO FIKIRIA HAPO AWALI

Manufacture highly-accurate prototype cars
and confirm completeness.

[​IMG]
Evaluation of performance through simulations and experiments
SOURCES  kutoka katika mitandao mbalimbali 

No comments:

Post a Comment