MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Tuesday 5 September 2017

Jumla ya watahiniwa 917,072 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi unaotarajiwa kuanza kesho

NECTA
Jumla ya watahiniwa 917,072 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi unaotarajiwa kuanza kesho katika shule 16,583 za Tanzania bara idadi ambayo imeongezeka ikilinganishwa na mwaka jana ambapo watahiniwa 795,761 walisajiliwa.
Katibu Mtendaji wa baraza la mitihani Tanzania – NECTA Dk Charles Msonde amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa mtihani huo utakaofanyika kwa siku mbili mfululizo ni muhimu kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla kwa kuwa unapima uwezo na uelewa wa mwanafunzi katika yale aliyojifunza kwa kipindi cha miaka saba.
Aidha Dk Msonde amebainisha kuwa maandalizi yote ya mitihani yamekamilika ikiwemo kusambazwa kwa karatasi za mitihani na fomu maalum za OMR za kujibia katika halmashauri/manispaa zote na kutumia fursa hiyo kutoa wito kwa kamati za mitihani mikoa na manispaa kuhakikisha taratibu zote zinazingatiwa na wasimamizi na wanafunzi kujiepusha na vitendo vya udanganyifu hatua ambayo itasabaisha kufutiwa mitihani hiyo.
Akijibu maswali kutoka kwa waandishi juu hatma ya shule zilizofungiwa hususan manispaa ya Ilala pamoja na zile zilizofungiwa miaka mitatu iliyopita ikiwemo Little Flower na St.Getrude juu ushiriki wake katika kipindi hiki cha mitihani amesema shule hizo mbili bado zimeendelea kufungiwa kutokana na suala la kiusalama.

KUPATA RATIBA BONYEZA LINK HAPO CHINI
⇛⇛ http://www.necta.go.tz/files/PSLE%202017%20TIMETABLE.pdf

No comments:

Post a Comment