Balozi mteule Dk Wilbroad Slaa amezungumzia uteuzi huo akisema ni mapenzi ya Mungu.
Rais John Magufuli leo Alhamis Novemba 23,2017 amemteua Dk Slaa kuwa balozi na ataapishwa baada ya utaratibu kukamilika.
Akizungumza na kituo cha televisheni cha Azam, Dkt. Slaa amesema ameona taarifa ya uteuzi kwa njia ya mtandao lakini baada ya muda alitumiwa barua rasmi.
“Ni mapenzi ya Mungu, nashukuru kwa uteuzi. Ninachoweza kusema katika hatua hii, huu ni wajibu mkubwa katika kipindi cha kulijenga taifa letu,” amesema.
Dk Slaa amesema, “Ninachoweza kusema nitakuwa tayari kutoa mchango na mwenyezi Mungu atanisaidia. Ndicho ninachosema kwa hatua hii ya sasa.”
No comments:
Post a Comment