MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Saturday, 3 February 2018

MAKAMU WA RAIS AWAPA POLE FAMILIA YA RUBANI WA SERIKALI KAPTENI BOMANI

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amehudhuria msiba wa Rubani wa Ndege za Serikali, Marehemu Kapteni Dominic Bomani aliyefariki jana kwa ajali ya ndege ndogo  ya mafunzo pamoja na mwanafunzi wake kutoka chuo cha taifa cha usafirishaji NIT  sekunde  chache  baada ya kupaa kwenye uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume  zanzibari Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha kumbukumbu cha maombelezo ya Rubani wa Ndege za Serikali Marehemu Kapteni Dominic Bomani nyumbani kwa marehemu Kinyerezi Kanisani.  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa pole Rosemary Bomani mjane wa aliyekuwa Rubani wa Ndege za Serikali Marehemu Kapteni Dominic Bomani nyumbani kwa marehemu Kinyerezi Kanisani. makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rosemary Bomani mjane wa aliyekuwa Rubani wa Ndege za Serikali Marehemu Kapteni Dominic Bomani, wengine pichani ni mtoto wa marehemu Joanitha Bomani (kulia) na Dada wa marehemu Stella Bomani(kushoto) wakati alipoenda kuwapa pole nyumbani kwa marehemu Kinyerezi Kanisani.

    Eneo ambalo ajali ilitokea huko zanzibar

No comments:

Post a Comment