MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Friday, 30 March 2018

KIFAACHA CHINA AINA YA Tiangong-1: UTAFITI UNAONESHA KITAANGUKA DUNIAN KIKIWAKA MOTO BAADA YA KUPOTEZA MAWASILIANO

Radar image of TiangongHaki miliki ya pichaFRAUNHOFER
Chombo cha anga za juu cha China kwa jina Tiangong-1 ambacho kimekuwa kikitumiwa kama maabara kinatarajiwa kuanguka duniani mwishoni mwa wiki.
Kina urefu wa mita 10 na uzani wa zaidi ya tani 8 na ni kikubwa zaidi ya vyombo vyote vilivyoundwa na binadamu ambavyo vimewahi kuanguka kutoka anga za juu.
China inasema imepoteza mawasiliano yote na chombo hicho jambo ambalo linamaanisha kwamba mwendo wake wakati kinadondoka kutoka anga za juu hauwezi kudhibitiwa.
Hata hivyo, wataalamu wanasema uwezekano wa vipande vya Tiangong ambavyo havitakuwa vimeteketea kabisa wakati vikifika ardhini kuanguka kwenye maeneo yenye watu wengi ni mdogo sana.
"Ukizingatia kwamba Tiangong-1 ina uzani wa juu sana, vipande vyao vimekazwa sana, kuliko ilivyo kwa vitu vingine ambavyo hurejea duniani kutoka anga za juu, kumekuwa na juhudi nyingi za kutumia mfumo wa rada kufuatilia mwendo wake na kukadiria ni wapi kitaanguka," anasema Richard Crowther, mhandisi mkuu katika Shirika la Anga za Juu la Uingereza.
"Sehemu kubwa ya chombo hiki inatarajiwa kuungua kikiingia ndani ya anga ya dunia kutokana na kushika kiwango cha juu cha joto. Uwezekano mkubwa ni kwamba vipande ambavyo vitasalia baada ya hapo vitaanguka mahali baharini," aliambia BBC.
Presentational grey line
Graphic
  • Ni vigumu kujua mapema ni wapi kitaanguka na ni wakati gani
  • Kawaida, wataalamu huweza kubaini ni wapi saa moja kabla ya chombo kama hicho kuanguka
  • Sehemu kubwa ya chombo hicho itaungua chombo kitakapoingia kwenye anga ya dunia
  • Njia ya mzingo ya chombo hicho ina maana kwamba vifusi sana vitaanguka katika eneo moja
  • Pengine 20-40% ya chombo hicho itafika ardhini, ambayo ni tani 1.5-3.5 hivi
  • Uwezekano mkubwa ni kwamba vifusi hivi vitaanguka baharini
  • Njia ya kuanguka kwa vifusi hivyo ardhini inaweza kuwa na umbali wa mamia ya kilomiya
  • Tiangong ndicho chombo cha 50 kwa uzani kuanguka duniani kikiwa hakiwezi kudhibitiwa
Presentational grey line
Chombo hiki ambacho kilikuwa kikitumiwa kama kituo cha anga za juu kilirushwa angani mwaka 2011 na kutembelewa na wana anga sita wa China.
Tiangong kilifaa kusitisha shughuli yake ya kuizunguka dunia kwa utaratibu na mpangilio fulani.
Lengo lilikuwa kutumia vifaa vinavyokipa msukumo kukielekeza hadi maeneo ya mbali yasiyo na watu maeneo ya Bahari ya Kusini.
Lakini kabla ya hilo kufanyika, ghafla mfumo wa kukidhibiti ulikumbwa na hitilafu na wataalamu wa China wakapoteza udhibiti.
Kwa sasa, hakuna lolote linaloweza kufanyika kuzuia chombo hicho kisianguke popote.
Mashirika 13 ya anga za juu ya mataifa mbalimbali, yakiongozwa na Shirika la Anga za Juu la Ulaya (ESA), kwa sasa yanafuatilia njia ya Tiangong na kujaribu kuiga tabia yake kadiri kinavyoingia ndani ya anga ya dunia kikiendelea kuizunguka.
Kwa pamoja, mashirika hayo yana kundi linalofahamika kama Kamati ya Mashirika ya Pamoja ya Kuangazia Taka kutoka Anga za Juu, na yanajaribu kukadiria ni wakati gani hasa chombo hicho kinaweza kuanguka na ni wapi.
RoketiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionChina ilikituma chombo cha Tiangong-1 angani mnamo 2011
Kutotabirika kwake kuna maana kwamba kwa sasa ni taarifa tu na ubashiri unaofanywa huku kila mtu akisubiri kuona chombo hicho kitaanguka wapi.
"Wataalamu wanaweza kuwa na uhakika wa mwelekeo wa chombo hiki wa saa moja hivi na hilo linaweza kufanyika saa nne tu pekee pamepa. Lakini uhakika huo wa saa moja una maana kwamba itaweza kufahamika pengine karibu mzunguko mzima wa mwisho," mkuu wa kitengo cha kuondoa taka anga za juu wa Esa Holger Krag anasema.
"Lakini hilo linatosha kutahadharisha mataifa kadha, au hata mabara."
Kinachoweza kubainishwa wazi kufikia sasa ni kwamba hakuna vifusi vyovyote vitakavyoanguka nje ya eneo la nyuzi 43 kaskazini na kusini mwa Ikweta.
Hii inajumuisha eneo kubwa la kuanzia bahari ya Mediterranean hadi Tasmania, kwa mfano.
Hilo linatokana na mwinamo wa Tiangong wakati wa kurushwa kwake angani.
China haina uwezo mkubwa wa kufuatilia vyombo vyake vinapozunguka anga za juu na kwa hivyo haikuwa na njia nyingine nzuri ila kurusha chombo hicho kiasi kwamba kingekuwa kikizunguka dunia kupitia Ikweta.
Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu kwa mfano hufika nyuzi 52 kaskazini na kusini.
Presentational grey line
Tiangong maana yake ni 'Kasri la Mbinguni'
Tiangong-1 space lectureHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMwanananga Wang Yaping alitoa mhadhara unaokumbukwa sana kwa watoto akiwa moja kwa moja kutoka chombo cha Tiangong-1 kikiwa anga za juu
  • Chombo hiki kirirushwa mwaka 2011 kufanyia majaribio utaratibu wa kutuma vyombo vingine na kuviunganisha vikiwa anga za juu
  • Makundi mawili ya wanaanga yalizuru chombo hicho wakitumia vyombo vidogo kwa jina Shenzhou - mwaka 2012 na 2013
  • Walijumuisha wanaanga wa kwanza wa kike kutoka China Liu Yang na Wang Yaping
  • China inapanga kutuma chombo cha anga za juu cha kudumu katika mwongo mmoja ujao
  • Imeunga roketi inayobeba kuinua vitu vya uzani wa juu sana kwa jina Long March 5 kwa ajili ya kazi hiyo
Presentational grey line
Maeneo ambayo kituo hicho kinatarajiwa kuanguka yanaishi watu 5.2 bilioni hivi, ingawa mengi ya maeneo hayo ni bahari.
Hii ndiyo maana uwezekano mkubwa wa chombo hicho ni kuanguka baharini.
Dkt Krag alisema: "Tunafahamu kutoka kwa matukio sawa ya awali kwamba kati ya 20% na 40% ya chombo kama hicho kwa uzani wake ndiyo hufika ardhini baada ya sehemu kubwa kuteketea.
"Tukitumia kipimo hiki kwa Tiangong, naamini, kimsingi... basi tani 1.5 hadi 3.5 zinaweza kufika ardhini."
Vipande vingi ambavyo sana hukosa kuteketea ni matanki ambayo sana huwa sehemu ya ndani ya chombo.
Na pia huwa yameundwa kwa chuma, titanium au plastiki zilizoimarishwa zaidi na kawaida huwa yanahimili joto kali.
Graphic
Tiangong ni miongoni mwa vyombo vingine vikubwa vilivyowahi kuanguka bila kudhibitiwa, lakini bado kineachwa nyuma na vyombo vingine.
Chombo cha Skylab cha Marekani kilikuwa na uzani wa tani 80 kilipoanguka, ingawa kiliweza kudhibitiwa kwa kiasi fulani, mwaka 1979.
Kilianguka Australia Magharibi ardhini lakini hakuna aliyejeruhiwa.
Chombo cha Nasa cha Columbia nacho kilikuwa na uzani wa tani 100 kilipoanguka mwaka 2003.
Tena, ardhini hakuna aliyegongwa na vifusi vyake ambavyo vilitapakaa majimbo ya Texas na Louisiana.
Mtaalamu Jonathan McDowell kutoka Kituo cha Fizikia ya Anga za Juu cha Harvard-Smithsonian anasema kwa kukadiria, 50 ni chombo cha 50 kwa ukubwa.

Lakini je vifusi vya vyombo vyote vya anga za mbali huanguka duniani?

Wakati vifusi vya vyombo vya anga za mabali huanguka mara kwa mara, vingi " huungua na kuishia katikati ya bahari na mbali na wanapoishi watu," anasema Bw Aboutanios.
Kwa kawaida huwa yanakuwepo bado mawasiliani na chombo au setilaiti. Hii inamaanisha kuwa udhibiti wa wataalam kutoka ardhini bado unaweza kukiongoza chombo na kukipeleka mahala ambapo wanataka kiangukie.
Kifusi huwa kinaongozwa kuangukia kwenye kile kinachoitwa ncha ya bahari ambayo haifikiwi na watu - mbali kabisa na ardhi kavu. Ni eneo lililopo Kusini mwa Pacific, baina ya Australia, New Zealand na Amerika Kusini.
Ni eneo lenye ukubwa wa kilomita za duara, 500 eneo hili ni eneo la makaburi ya vyombo vya anga za mbali pamoja na setilaiti, ambako masalia ya vyombo vya anga za mbali vipatavyo 260 yanadhaniwa kuzikwa kwenye sakafu ya bahari.
Watu wakishikilia magazeti yenye picha ya mChina wa kwanza kwenda katika anga za mbali kwenye ukurasa wa mbeleHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMchina wa kwanza aliyefanya safari ya anga za mbali 2003 alikuwa shujaa wa taifa

Je Tiangong-ni nini?

Uchina ilichelewa kuanza uvumbuzi wake wa anga za juu.
Mnamo 2001, Uchina ilizindua vyombo vyake vya anga kwa kujaribu kuwatuma wanyama mwaka 2003 kwenye chombo cha anga za mbali kwenye mzingo wa dunia, na hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa ni ya tatu kufanya hivyobaada ya Muungano wa Usovieti na Marekani.
Mpango wa vituo vya safari za anga za mbali ulianza kwa kukituma chombo cha Tiangong-1 ama "Kasri la Mbinguni", mwaka 2011.
Kituo hicho kidogo kiliweza kuwahifadhi wataalam wa masuala ya anga za mbali lakini kwa muda mfupi wa siku kadhaa. Mchina wa kwanza mwanamke mtaalamu wa anga za juu Liu Yang alitembelea kituo hicho mwaka 2012.
Kilikamilisha huduma zake mwezi Machi 2016, miaka miwili zaidi ya muda kiliopangiwa

No comments:

Post a Comment