Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imetoa orodha ya Awamu ya Tatu yenye wanafunzi 4,161 wa Mwaka wa Kwanza waliofanikiwa kupata mikopo na hivyo kufanya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo hadi sasa kufikia 32,090.
Bofya hapa kuona orodha hiyo. Aidha, orodha hii imetumwa vyuoni walipo wanafunzi husika.
Kiasi cha TZS 427.5 bilioni zimetengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wote, wa mwaka wa kwanza na wanaoendelea na masomo.
HESLB inawasisitizia waombaji wa mikopo wenye sifa ambao hawajapangiwa mikopo, hususani wale waliokamilisha udahili hivi karibuni, kuendelea kuwa na subira wakati ikikamilisha orodha inayofuata ya wanafunzi waliopata mikopo.
Taarifa zitaendelea kutolewa mara kwa mara kupitia vyombo vya habari na tovuti hii ya Bodi.
Imetolewa na:
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
DAR ES SALAAM
Ijumaa, Novemba 9, 2018
No comments:
Post a Comment