Kwenye maisha hakuna anayejua hatma yake wala nani kapangiwa jambo gani na Mungu liwe jema au baya na kwa wakati gani. |
"USIMUACHE KISA MASIKINI UTAJUTA"
Tabia ya wanawake wengi kudharau wanaume wenye kipato kidogo kwa sasa imeshamili sana, hii ni kutokana na mmong'onyoko wa maadili na kutojitambua kwa wanawake wa kileo.
UDAKU ZAIDI.
Huwa kunausemi usemao kila kwenye mafanikio ya MWANAUME kuna MWANAMKE nyuma yake, hivyo WANAWAKE wanaopenda WANAUME wenye MAISHA mazuri magari, nyumba za thamani watambue kuwa kuna WANAWAKE wenzao WALIKUWEPO au WAPO nyuma yao hao WANAUME kuwatia moyo na nguvu katika hayo mafanikio ambayo wameyapata.
Hivyo wanawake wengi huishia kusema wanaume ni wasaliti kwa sababu kwanza akumwambia kama anaMKE na watoto wakati anavyomtongoza ili ajue lakini wamesahau kwamba ule usemi usemao "Kwenye mafanikio ya Mwanaume basi kuna Mwanamke nyuma yake" hivyo mwisho wake ni maumivu yasio na kitulizo kwenye mahusiano wanayopalamia kwa baadhi ya wanaume wenye mafanikio.
USHAURI.
_________________________________________________________________________________
Ule usemi usemao "Kwenye mafanikio ya Mwanaume basi kuna Mwanamke nyuma yake" mwanamke uutumie vizuri u wanamke wako kumjenga mpenzi uliyenaye kwasasa hata kama hana kitu mtie nguvu, moyo katika kutafuta kipato chake kama ni mwanafunzi mtie moyo asome kweli kwa bidii huku ukimuombea kwa MUNGU, ili siku akifanikiwa au akitoka nje aonekane ni mwanaume mwenye mafanikio na mwenye kutamaniwa na wanawake wanaopenda kuwa na wanaume wenye mafanikio lakini ukiwa umemjengea mumeo HOFU YA MUNGU kwa kuhudhuria IBADA kwaajili ya kulinda na kuiheshimu ndoa yake siku zote.
MWANAMKE MJENGE MUMEO AWE MWANAUME MWENYE MAFANIKIO NA SIO KUTAMANI WANAUME WENYE MAFANIKIO WALIOJENGWA NA WANAWAKE MWENZAKO.
No comments:
Post a Comment