MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Wednesday, 28 November 2018

ZITTO KABWE AKARIBISHWA CHAMA CHA MAPINDUZI(CCM)

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe amefunguka kuwa kuhamia kwake CCM hakutomaliza changamoto za Watanzania.
Zitto ametoa kauli hiyo baada ya kukaribishwa na Katibu Mkuu wa CCMDkt. Bashiru Ally  kujiunga na chama hicho, ambapo alimpongeza kwa kuibua mijadala yenye maslahi ya kiuchumi.

"Mimi kujiunga CCM sio jawabu la shida za Watanzania na changamoto zinazoikabili nchi kama vile watu kukosa Uhuru wa mawazo, kukosoa, kupashana Habari na ukandamizwaji mkubwa wa vyama vya upinzani, Wananchi wanyonge kama Wakulima, Wavuvi, Wafugaji na uporaji wa Mali za watu wakiwemo Wafanyabiashara", amesema Zitto na kuongeza;

"Namwomba Bashiru,  CCM ni kundi la wasaka vyeo na walinda vyeo. Chama pekee cha Kijamaa nchini ni ACT Wazalendo kupitia Azimio la Tabora. Namtaka Mjamaa Bashiru Ally aachane na CCM iliyofilisika kiitikadi na ajiunge na ACT Wazalendo, Chama pekee cha Kijamaa Nchini na Afrika Mashariki".

Mapema leo akizungumza na wanachama wa CCM mkoani Iringa, Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Bashiru Ally ikiwa ni ziara yake ya kikazi mkoani humo amesema kuwa Zitto Kabwe anatakiwa kujiunga na chama hicho, kwani busara zake zinafaa kukitumikia chama hicho chenye Itikadi ya Kijamaa

No comments:

Post a Comment