MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Tuesday, 15 January 2019

CHENGULA BLOG TUNAKUPA DONDOO KALI KUHUSU KUTAMBUA AINA MBALIMBALI YA VIBAO KWENYE KWENYE MAGARI


Hivi hizi herufi kwenye "licence plates" za magari zinamaana gani?

STK
STJ
STH
ST A
ST
DFP
SU - (hii nimesikia ni Shirika la Umma, ila sijui kama ni kweli)
TP - (magari ya polisi yana herufi hizi, ila sijui zinamaanisha nini)
E - (hii naona kwenye msafara wa rais, so nahisi E inasimama kwa neno Escort)
CD - (hii nadhani maana yake inatokana na neno la kifaransa Cors Diplomatique, na inakuwa kwenye yale magari ya maembasy)

Naomba kuwasilisha



------
Ukiona mtaani gari zimeandikwa ktk plate number kama ifuatavyo usiumize kichwa jua ni hivi:

1. Namba za Magari Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu 
Namba za magari yanayitumika kumbeba Rais au Makamu wa Rais na Waziri Mkuu haziandikwi namba wale herufi katika kibao chake, bali huwa na nembo ya taifa ya Bwana na Bibi. Kwa Kiingereza magari haya hufahamika kama State Cars,

ikulu-jpg.836477

2. Spika wa Bunge la Tanzania na Naibu wake
Spika wa Bunge pia gari lake huwa halina namba kwenye kibao chake bali huwa na herufi S pekee. Gari la Naibu Spika nalo huwa na herufi NS pekee. Maana ya herufi S ni Spika na NS ni Naibu Spika

naibu-spika-jpg.836478

3. Katibu Mkuu Kiongozi
Katibu Mkuu Kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatumia gari ambalo lina kibandiko chenye herufi CS pekee. Ikiwa maana ya CS ni Chief secretary

katibu-mkuu-kiongozi-jpg.836479

4. Jaji Mkuu wa Tanzania
Gari la Jaji Mkuu wa Tanzania huwa na herufi JM kwenye kibao chake

jaji-mkuu-jpg.836480

5. Mkuu wa Majeshi (CDF)
Gari la Mkuu wa Majeshi wa Tanzania katika kibao chake huwa hakuna namba wala herufi zozote bali kunakuwepo na Nyota nne kwenye kibao cha gari lake

cdf-jpg.836481

6. Waziri na Naibu Waziri wa Wizara mbalimbali
Magari ya Waziri na Manaibu wao huwa na herufi zinazoonyesha cheo (kama ni waziri au Naibu waziri) halafu hufuatia ana vifupisho vya majina ya Wizara zao. Gari la Waziri huwa na herufi W ikifuatia na kifupisho cha jina la Wizara yake. Gari la Naibu waziri huwa na herufi NW ikifuatiwa na kifupisho cha jina la Wizara yake

waziri-jpg.836483

naibu-waziri-jpg.836484

7. Gari za Serikali za Mitaa
Magari ya Serikali za Mitaa, yanayotumiwa kwenye Serikali hizo. Magari hayo kuwa na kibao chenye Herufi SM zikifuatiwa na namba tofauti tofauti.

serikali-mtaa-jpg.836487

8. Magari ya Shirika la Umoja wa Mataifa
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na moja ya shirika la umoja wa mataifa. Mfano shirika la Afya Duniani (WHO). Kibao chenye namba inayoanza na herufi T kufuatiwa na namba na herufi CD kisha namba tena.

umoja-mataifa-jpg.836488

9. Magari ya balozini Mbalimbali nchi Tanzania
Magari ya Ubalozi nchini Tanzania huanziwa na herufi T kufuatiwa na namba na kisha herufi CD kisha namba. Pia namba hizi hutumiwa na wafanyakazi wa ubalozi husika hata kama ni watanzania. Mfano wa Ubalozi ni Marekani

balozi-jpg.836489

10. Shirika la Umma. Mfano; TANESCO, EWURA
Magari yanayotumiwa na mashirika ya Umma huwa na kibao (Plate Number) ambazo huanziwa na herufi SU na kufuatiwa na namba tofauti tofauti kwenye vibao hivyo

shirika-umma-jpg.836491

11. Magari kwa ajili ya matumizi ya Miradi inayofadhiliwa na watu to nje ya nchi
Magari yanayotumika kwenye miradi inayofadhiliwa kutoka nje ya nchi kuwa na kibao chenye herufi DFP (Donor's Fund Project) ikifuatiwa na namba tofauti tofauti. Pia tofauti na DFP utakuta mengine yana DFPA

miradi1-jpg.836492

miradi2-jpg.836493

12. Magari ya Police wa Tanzania
Magari ya Polisi nchini Tanzania huwa na kibao chenye kuanziwa na herufi PT (Polisi of Tanzania) halafu hufuatiwa na namba tofauti tofauti mbele yake

pt-jpg.836494

13. Magari ya Jeshi la Wananchi Tanzania
Magari ya Jeshi la Tanzania huwa na kibao chenye kuanziwa na namba kadhaa kisha hufuatiwa na herufi JW kisha hufuatiwa na namba tena.

jeshi-jpg.836495

14. Magereza Tanzania
Magari ya Magereza ya Tanzania huwa na kibao chenye kuanziwa na herufi MT kisha hufuatiwa na namba kadhaa mbele yakekwenye kibao cha magari hayo

magereza-jpg.836496

15. Serikali ya Tanzania 
Serikali ya Tanzania ina gari zake tofauti tofauti ambzo hutumika kwa mfano Wilayani au hata kwenye halmashauri. Magari haya huwa na kibandiko chenye Herufi za mwanzo STK au STJ au STL na baada ya hapo hufuatiwa na namba kadhaa mbele

stj-jpg.836498

stk-jpg.836499

stl-jpg.836500

16. Magari ya Wakuu wa Mikoa
Wakuu wa mikoa wote nchi huwa na magari ambayo huwana plate number ka tofauti. Gari la mkuu wa mkoa huwa na kibandiko ambacho kuanza na herufi RC na kisha hufuatiwa na herufi ambazo ni kifupi cha mkoa wake. Herufi RC humaanisha Regional Commisioner. Mfano; RC NJB- Mkuu wa Mkoa Njombe


 

17. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Serikali ya mapinduzi Zanzibar hutumia magari yenye kibao chenye kuanziwa na herufi SMZ kisha kufuatwa na tarakimu kadhaa. Magari haya hutumika kwenye shuguli za kiserikali hivyo hupewa viongozi wa serikali katika ngazi fulani

smz-jpg.836501

18. JR- Jaji wa Mahakama ya Rufaa

19. JK- Jaji Kiongozi

20. J- Jaji wa Mahakama Kuu

21. CGP-Commissioner General of Prison(Mkuu wa Magereza)

22. CAG - Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali

23. Magari ya watu binafsi
Magari ya watu binafsi nchini Tanzania huwa na kibao chenye kuanza na herufi T kisha tarakimu tatu hufuata na baada ya hapo herufi tatu hufuata. Magari haya ya binafsi yanaweza kuwa ya biashara au la.

Pia kwenye magari ya binafsi ambayo sio ya biashara kunauwezekano kuwa na kibandiko ambacho kina jina mtu binafsi.




NYONGEZA:
Magari yote haya huwa pia na tofauti katika rangi za plate number hizo, rangi hizo zinaingiliana sehemu na sehemu;

1. Magari yenye plate number za Rangi ya Njano
  • Namba za Magari Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu
  • Spika wa Bunge la Tanzania na Naibu wake
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Jaji Mkuu wa Tanzania
  • Waziri na Naibu Waziri wa Wizara mbalimbali
  • Gari za Serikali za Mitaa
  • Shirika la Umma. Mfano; TANESCO, EWURA
  • Serikali ya Tanzania
  • Magari ya Wakuu wa Mikoa
2. Magari yenye plate number za rangi ya Kijani
  • Magari ya balozini Mbalimbali nchi Tanzania
  • Magereza Tanzania
3. Magari yenye plate number za rangi nyeusi
  • Magari ya Police wa Tanzania (Maandishi ya rangi ya njano)
  • Magari ya Jeshi la Wananchi Tanzania (Maandishi ya rangi nyeupe)
4. Magari yenye plate number za rangi nyekundu
  • Mkuu wa Majeshi (CDF) (Nyota zilizopo huwa na rangi ya dhahabu)
  • Magari kwa ajili ya matumizi ya Miradi inayofadhiliwa na watu toka nje ya nchi
5. Magari yenye plate number za rangi nyeupe
  • Magari kwa ajili ya biashara (Commercial Use)
  • Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
6. Magari yenye plate number za rangi ya bluu
  • Magari ya Shirika la Umoja wa Mataifa

No comments:

Post a Comment