Binadamu ni viumbe ambao wana mizunguko mingi katika siku zao za kuishi hapa duniani. Binadamu hao hao hukutana na jamii za watu tofauti tofauti katika shughuli mbalimbali za kusaka mafanikio kama vile mashuleni, kwenye semina mbalimbali na sehemu nyingine mbalimbali.
Binadamu hawa pamoja na kukutana kwako, ni watu wachache hutambua thamani ya kukutana kwako. Hebu tujiulize swali dogo tu, rafiki zako ulikuwa unasoma nao hata kucheza nao leo wapo wapi? Unajua wanafanya nini? Je ni wazima bado au walishafariki siku nyingi na wewe huna taarifa? Majibu baki nayo.
Nakumbuka sana enzi za utoto hasa katika mahafali yangu ya darasa la saba moja ya nyimbo ambazo tulizimba, nakumba tuliimba ya kuwa milima hakikutani ila binadamu hukutana, niliamini sana kwa kwa miaka ya mbeleni kuwa siku moja nitakuja kukutana na watu niliosoma nao lakini mawazo yangu hadi leo sijaona yakiitimia.
Maana yangu ni kuwa huenda ningejua wale niliokuwa nasoma nao, ningejua walipo na wanafanya nini, ningesonga mbele kimafanikio, hapo najaribu kuwaza kwa sauti tu.
Tuachane na hayo maana kila nikiwaza sina majibu, lakini jambo la kuzingatia ni kwamba mimi naamini kila binadamu wakikutana sehemu yoyote ile kuna sababu, ila wengi wetu bado hatujalitambua hilo.
Kwa mfano leo hii umekutana na mtu maarafu popote pale, jambo la kwanza utakaloliwaza katika akili yako ni kupiga Picha (selfie) na mtu huyo ili uje uweke mitaandaoni huku ukiandika maneno mbalimbali, kama vile katika ubora wangu, dunia itasimama na mambo mengine kama hayo.
Ndugu msomaji wa Makala hii kila mtu unayekutana naye, kuna sababu huenda akakusaidia katika safari yako ya Mafanikio na sio kupiga naye piicha na kuzidi kuwa na Maisha Yale Yale kila siku.
Kila mtu unayekutana naye kuna sababu. Cha msingi ni kujenga mahusiano bora na mtu huyo. Inawezekana ndiye atayekuwa msaada mkubwa katika kubadilisha maisha yako kwa namna moja ama nyingine.
Kama wewe ni miongoni mwa watu ambao unajiona maisha yako yamebadilika kwa sababu ya mtu fulani ndiye alichangia kuwa hapo ulipo chukua dakika chache kumshukuru huyo aliyekusaidia. Japo wengi wetu hatuna tabia hiyo ya kuwashukuru watu waliotusaidia kufika hapa tulipo, basi ni muda muafaka wa kutoa shukrani.
Jambo la msingi la kumbukumbuka kila unayekutana naye kuna sababu hivyo jenga mahusiano bora na kila anayekutana naye

No comments:
Post a Comment