MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Tuesday, 5 May 2020

Mmepeta Bure, Toeni Bure; Vitu Vitatu Ambavyo Kama Utavitumia Kwa Umakini Wa Hali Ya Juu Vitaweza Kukufanikisha Kwa Viwango Vya Juu Sana


Rafiki yangu hongera sana kwa nafasi ya siku hii ya keipkee. Siku ya leo napenda nikushirikishe vitu vitatu ambavyo wewe hapo umepata bure na unapaswa kuvitumia sana. Ubora wa vitu hivi vitatu ambavyo nitakushirikisha hapa sio kwamba unaweza kuvitumia vikaisha. Ubora wake ni kuwa kadri unavyovitumia ndivyo vinazidi kuimarika zaidi. Hivyo usiogope kuvitumia
Vitu vyenyewe ni
1. AKILI. Hiki ni kitu ambacho unacho bure na unapaswa kukitumia kufikiri. Tatizo la watu wengi wanadhani kuwa wanafikiri kumbe hawafikiri alisema Harry Lorayne, ambaye alimalizia kwa kusema kuwa “ukiwaambiwa watu kuwa mnafikiri sana watakupenda ila ukiwaambia tumia akili watakukchukia”. Hakuna anayependa kuambiwa ukweli kwamba akili yake ni rasilimali muhimu ambayo anapaswa kuitumia. Watu wanapenda kusifiwa tu kuwa wanafiriki.
Na mimi nilivyo mchokozi leo hii napenda tu nikwambie kwamba FIKIRI. Jenga utaratibu wa kutumia akili yako kadri uwezavyo. Akili yako inaweza kuzalisha mawazo mapya ambayo yanaweza kuisaidia dunia. Akili yako inaweza kutengeneza vitu vizuri ambavyo  dunia inaweza kufurahia. Ebu itumie.

Ubora wa akili ni kama msuli. Kadri ambavyo mtu unakuwa unatumia msuli ndivyo misuli inazidi kuimarika. Vivyo hivyo kwenye akili yako. Kadri ambavyo utakuwa unatumia akili yako ndivyo ambavyo akili yako itakuwa inazidi kuimarika zaidi. Hivyvo kuanzia leo jifunze namna bora ya kuitumia akili yako kwa manufaa. Itumie, itumie.

2. NGUVU. Hii ni rasilimali nyingine muhimu ambayo unapaswa kuitumia kwa viwango vikubwa bila kuchelewa. unazo na unapaswa kuzitumia kukamilisha majukumu yako ya kila siku. Usijipe sababu za kwa nini huwezi kukamilisha baadhi ya majukuamu. Nenda tumia nguvu zako na uyatimize.

Kuna watu ambao wamezoea kulalamika na kuwaona watu wengne kama wamebarikiwa zaidi yao. Ila ukweli ni kuwa watu hawa wanazijua siri hizi mbili muhimu mpaka sasa ambazo tayari tumezipitia. Yaani kutumia akili nguvu zao na hii ya tatu hapa chini, basi watanufaika sana.

3.  KIPAJI
Hii ni rasilimali nyingine muhimu uliyonayo ambayo unapaswa kuitumia haswa.
Moja ya kitu ambacho huwa kinanishangaza miongoni mwa watu ni jinsi ambavyo wanachukulia vipaji. Kuna baadhi ya watu ambao wanadhani kwamba baadhi ya watu wamebarikiwa kwa kupewa vipaji huku wengine wakiwa wamenyimwa. Jambo hili sio kweli.
Kila mtu ana kipaji chake ambacho akiweza kukitumia vizuri kitamsaidia sana. kwenye kitabu changu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI nimeeleza kiundani jinsi ambavyo unaweza kugundua kipaji chako na kukitumia kwa uzuri. 
Kuna mtu mmoja ambaye nilikuwa naongea naye kuhusu vipaji. Nikamuuliza hivi wewe kipaji chako ni kipi?  Aliniambia hivi, YAANI WEWE BONGO HII  UNAULIZA MAMBO YA VIPAJI.  Aliendelea kusema kuwa mambo ya vipaji yapo ulaya ila sio bongo. Mwisho alimalizia kwa kusema “wewe tafua fedha tu, achana na mambo ya vipaji”.

Huyo ni mmoja kati ya wengi ambao nimewasikia wakiongelea kuhusu vipaji. Pengine na wewe ni miongoni mwa watu ambao wamekuwa hawajui umuhimu wa vipaji maishani mwao. Kuanzia leo hii nakusihi sana uanze safari yako ya kuhakikisha kwamba unatambua kipaji chako, unatumia kipaji chako na ni wazi kuwa kipaji chako kitakulipa. Mwenye kipaji halali njaa, hahah

No comments:

Post a Comment