MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Saturday 23 May 2020

MADIWANI WA CUF CHADEMA WAENDELEA KUTIMUKIA CCM


Wakati tukienda kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba, mwaka huu wa 2020. Madiwani sita wa vyama vya CUF- Chama Cha Wananchi(CUF) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Nachingwea, mkoa wa Lindi wamevihama vyao na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

 Jana wakizungumza baada ya kutangaza kuhama vyama vyao nakujiunga na CCM baadhi ya madiwani hao walisema wamejiunga na CCM kwa hiyari yao kutokana kuvutiwa na utendaji wa Rais Dkt John Magufuli na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2015.

Omari Lingumbende ambae alikuwa diwani wa kata ya Namapwia na katibu wa wilaya wa CUF alisema hakuona haja ya kuendelea kubaki CUF wakati serikali inafanya yale ambayo alikuwa anataka yafanyike.

Alisema serikali ambayo imeundwa na CCM imepeleka miradi mingi katika vijiji vya kata ya Namapwia. Ikiwamo ujenzi wa shule, zahanati na zimepelekwa fedha nyingi zitakazo tumika katika utekelezaji wa miradi hiyo na mingine.

Nae Asha Mdam ambae alikuwa diwani wa viti maalumu wa kata ya ugawaji( CHADEMA) na katibu wa umoja wa madiwani wa kanda ya Kusini alisema ameamua kwa hiyari yake kujiunga na CCM baada ya kuridhishwa na utendaji wa Rais Dkt John Magufuli na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015.

Nae aliyekuwa diwani wa kata ya Kiegei, Hemed Madogo alisema baada ya kukihenyesha CCM kwa takribani miaka 15 ameamua kujiunga nacho baada ya kufurahishwa na utendaji wa serikali ya awamu ya tano.

Akizungumza baada ya kuwapokea makada hao wa vyama vya upinzani, katibu wa CCM wa wilaya ya Nachingwea, Hakim Jackson alisema chama hicho hakina ubaguzi. Kwahiyo kitaendelea kuwapokea wanaojiunga na kitawapa haki zote bila ubaguzi.

Katibu huyo aliweka wazi kwamba chama hicho hakina fedha za kununulia wanachama. Kwahiyo hakinunui na hakitaraji kununua wanachama.¥ Waliohama vyama vyao nakujiunga na CCM ni Omari Lingumbende(CUF, kata ya Namapwia), Hemed Madogo(CUF, kata ya Kiegei), Catherine Kapanda(CUF,viti maalum).

Wengine ni Asha Mdam(CHADEMA, vitimaalum), Gabriel Matuta( CHADEMA, kata ya Naipanga) na Jamal Tamba( CHADEMA, kata ya Mpiruka).

No comments:

Post a Comment