*DAR ES SALAAM DERBY*
*Vita Ya Ubingwa Iliyojaa Visasi*
*Na Athuman Bemelengo*
Muda umewadia sasa. Na umefika ule wakati ambao wadau na wapenzi wote wa soka hapa ndani na nje ya nchi huelekeza fikra zao katika mchezo mkubwa sana kwa ligi kuu ya Tanzania.
Hii ni mechi ya watani wa jadi inayowakutanisha Simba dhidi ya Yanga. Mechi hii haijawahi kuwa ndogo hata ingekuwa ni mechi ya bonanza tu la kawaida. Ukubwa wake unaifanya kuwa mechi ya tatu kwa ukubwa barani Afrika.
Wakati umewadia na jumamosi hii watani hawa wa jadi watashuka tena dimbani kwa ajili ya kukipiga katika mchezo wa raundi ya pili ya ligi kuu.
Siku hii ilisubiriwa kwa hamu sana baada ya kuahirishwa kwa ile tarehe ya kwanza ambapo mchezo huu ulikuwa umepangwa kuchezwa tarehe 18 mwezi huu.
Kuelekea mchezo huu utakaochezwa siku ya jumamosi tarehe 25 mwezi huu nimekuandalia makala hii yenye mambo yatakayozidisha upinzani katika mchezo huu.
*MCHEZO WA VISASI*
Kila wakutanapo wababe hawa wa soka la Tanzania lazima hutawaliwa na dhana ya ulipaji wa kisasi kwa upande mmoja. Lakini kuelekea mchezo huu itakuwa tofauti sana na pande zote mbili zitakuwa na kiu hii ya kulipa kisasi kwa mpinzani wake kufuatia mwenendo wao kwa msimu huu.
Simba watahitaji kulipa kisasi kwa kile kilichotokea katika mchezo wa kwanza wa ligi ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare baada ya mshambuliaji wa Yanga Amisi Tambwe kuisawazishia timu yake kwa goli lililozua utata mkubwa kwa kile kilichoonekana kuwa aliushika mpira ule kabla ya kuumalizia golini.
Kwa upande wa Simba waliumizwa sana na matokeo yale hali iliyowapelekea mashabiki wake kufanya uharibifu mkubwa wa uwanja. Ni hakika wanahitaji sana kulipa kisasi juu ya hili na kuwaadhibu watani wao katika mchezo wa ligi kuu na sio katika mashindano mengine. Licha ya kufanya hivyo katika michuano ya Mapinduzi lakini bado hii haitoshi kutibu kiu yao.
Upande wa pili ambao ni Yanga wao walipoteza mchezo wao wa mwisho dhidi ya watani wao walipokutana katika mechi ya nusu fainali ya kombe la Mapinduzi. Haliwezi kuwa jambo la kawaida kwao kukubali kipigo katika mechi ya pili mfululizo. Haiwezekani kabisa hivyo Yanga watakuwa na kila sababu ya kuwafurahisha mashabiki wao kuwafuta machozi kuwasahaulisha kile kilichotokea mjini Unguja.
Dhana hii ya kulipa kisasi baina ya watani hawa wa jadi ni wazi inaongeza upinzani katika mchezo huu.
*MBIO ZA UBINGWA*
Upinzani katika mechi hii unachagizwa sana na mbio za ubingwa baina ya timu hizi mbili ukizingatia sasa hivi ligi imefika katika wakati ambao kila timu inaamini ni wakati sahihi kabisa wa kutengeneza mazingira ya kwenda kutwaa taji. Simba wana uchu sana na taji hili msimu huu ukizingatia ni msimu wa nne sasa hawajatwaa taji la ligi. Mwanzo walikuwa wakiizidi Yanga kwa pointi nyingi sana lakini mpaka sasa Simba inaongoza kwa pointi moja ikiwa imecheza mchezo mmoja zaidi ya Yanga.
Simba ikishinda mchezo huu ndio itakuwa njia sahihi na nyepesi ya kumpunguza mpinzani wao. Wanalazimika kushinda mchezo huu ili kujihakikishia kukaa kileleni.
Lakini hata kwa upande wa Yanga vivyo hivyo kwa kushinda mechi hii inawapa nafasi kubwa ya kutetea taji lao kwa sababu watakuwa wamefanikiwa kurejea kileleni kwa tofauti ya pointi mbili zaidi ya Simba wakiwa na mchezo mmoja mkononi. Hakuna njia nyingine rahisi ya kuwapa Yanga matumaini makubwa ya kutwaa ubingwa zaidi ya hii.
Kwa wastani zikiwa zimebaki mechi saba za ligi, mechi hii ni muhimu sana katika mbio hizi za ubingwa na inawezekana kabisa mechi hii ikaja kutuamulia ni nani atakuwa bingwa kwa msimu huu.
*MAKOCHA WAMEVIZOEA VIKOSI VYAO*
Katika michuano ya Mapinduzi kocha wa Yanga George Lwandamina alionekana wazi kuwa bado alikuwa hajakizoea kikosi chake pamoja na wachezaji wake hali iliyopelekea timu hiyo kuzidiwa katika mchezo dhidi ya Azam fc baada ya kukosea katika kukipanga kikosi chake.
alfachengulablogspot.com
No comments:
Post a Comment