alfachengula.blogspot.com//mke wa rais sehemu ya nne on line
ILIPOISHIA
. Nikasikia sauti ya muhudumu waduka akionekana kufurahia tukio hilo.
“Unachekelea nini?” “Mimi siwapendi hao wanaharamu, wamarekani safi sana Al-quida Mungu awazidishie” Kwa hasira nikachomoa bastola yangu na kumuelekezea muhudumu huyo wa duka, ila akaonekana kujiamini sana, nilipo geuka nikakuta watu si chini ya ishirini wakiwa wamenielekezea bunduki zao na wote ni wale ambao walikuwa wakinifwatilia tangu nilipokuwa niikiingia ndani ya duka hili
ENDELEA
Sikutaka kufanya kosa lolote zaidi ya kuendelea kumnyooshea bunduki muhudumui wa duka hili, bastola yangu ambayo imeelekea kwenye paji la uso wake na laiti akijaribu kufanya mavyongo yoyote ninamfummua kichwa chake, hata wakiniua mimi ila nami nitakuwa nimemuondoa huyu anaye oenekana ndio kiongozi wako. Gafla nikasikia vilio vya maumivu vikitokea nyuma yangu, huku watu kadhaa walio nizunguka wakianguka chini na kutoa vishindo vizito. Risasi zilizo ingia ndani ya duka hili kimya kimya na kutua kwenye miili ya watu hawa, moja kwa moja nikajua zinatokea ndani ya gari na Naomi ndio msababishaji wa maafa haya ambayo yaliwachanganya sana watu walio nizunguka.
Wakiwa bado wanashangaa shangaa kujiuliza ni wapi risasi hizo zinapo tokea, ikawa ni nafasi yangu na mimi kufanya shambulizi kwa kutumia wepesi wa miguu yangu, huku nikirusha mateke niliyo yapeleka kwenye shingo za waarabu hawa, nilio wafanya kuanguka chini, huku wakitoa vilio vya maumivu. Nikajirusha hadi sehemu alipo muuza duka na kumtandika ngumi moja ya pua iliyo mfanya kuyumba hadi akajigonga kwenye friji lililopo pembeni. Nikamshika na kumnyanyua juu, nikampika kisukusuku cha kichwa na kumfanya kilemba alicho jifunga kichwani kuanguka chini.
Watu wote walio kuwa wamenizunguka, walilala chini huku damu nyingi zikiwa zimesambaa sakafuni na wote walisha iacha dunia na kuingia kwenye ulimwengu ambao hakuna binadamu aliye hai aliweza kuufika siku hata moja.
Nikamshika muhudumu wa duka hili alio kuwa akishangilia kuuawa kwa wezetu, kwa kumtazama nikahisi kuna kitu chochote atakuwa anakijua kuhusiana na kundi la Al-qaida. Nikamchomoa hadi nje na kumkuta Naomi akiwa nje ya gari huku bunduki yake aliyo ifunga kiwambo cha kuzuia sauti ikiwa mkononi mwake.
“Vipi unampelekea wapi huyo?” “Kuna kitu anajua kuhusiana na Al-quida” Naomi akafungua mlango wa gari katika siti aliyo kuwa amekaa, akatoa pingu na kunirushia, nikamfunga muhudumu huyu anaye endelea kuvujwa na damu za pua, nikampapasa kila kona ya mwili wake nilipo gundua kwamba hana kitu chochote, nikamsukumia siti ya nyuma ya gari na kumuamrisha akae kimya la sivyo nitampasua kwa kumtwanga risasi za kichwa.
“Naomi mlinde huyo”
Nikaingia ndani ya duka na kuchukua baadhi ya vinjwaji pamoja biskuti, kabla ya kutoka nikachukua bastola nne zilizo kuwa zinatumiwa na watu hawa walio kuwa wanahitaji kunidhuru. Nikatoka na kurudi kwenye gari, Naomi akatazama kila upande na kuingia ndani nami nikaingia. Nikawasha gari na kuondoka kwa kasi nje ya duka huku tukiendelea kufwata ramani tuliyo pewa ili kutuwezesha kuweza kufika Karachi, ambapo tungepewa msaada na ubalozi wa Marekani.
Ndani ya dakika kumi na tano tukiwa njiani, nikaona gari zipatazo sita zikija nyuma yetu kwa kasi, jambo lililo anza kunipa wasiwasi mkubwa kwani sikujua ni kina nani. Nikamuona muhudumu wa duka akitabasamu, hapo ndipo nikafahamu kwamba wanao tufwata wanaweza kuwa niwezao.
“Naomi endesha” Nilimuamrisha Naomi kuweza kufanya hivyo kutokana yeye bado anajeraha la mguuni, tukapishana kwenye siti ya dereva kwa ustadi mkubwa bila ya gari kuweza kuyumba, nikajirusha kwenye siti ya nyuma alipo kaa muhudumu wa duka, nikampiga kwenye shingo kwa kutumia ubapa wa kiganja changu na kumfanya apoteze fahamu. Gari hizo zikazidi kutufwata kwa kasi sana huku zikiwa zinawasha taa, Naomi hakuwa mzembe katika kuendesha gari, kwani aliweza kuifanya gari yetu kutembea kwa kasi kubwa sana, huku kila kona anayo kutana nayo anaweza kuikunja vizuri pasipo shida ya aiana yoyote.
Nikatizama bastola zangu, zote nikazikuta zimejaa risasi kwenye magazine zake. Risasi zikaanza kurushwa zikitokea kwenye magari yanayo tukimbizia nakupiga kioo cha nyuma kwenye gari yetu aina ya ‘pickup’ na kikapasuka.
“Shitii”
Nilizungumza huku nikijificha kwenye siti, nikashusha pumzi kisha nikajinyanyua na kuanza kujibu mashambulizi ya watu hao, ambao kwetu wamesha kuwa watu wabaya kwani nia yao kubwa ni kuweza kutudhuru sisi. Nikazidi kufyatua risasi kwenye moja ya gari ambalo linakaribia kutufikia, kwa bahari nzuri dereva wa gari hilo nilihisi nimempiga risasi kwani, gari hilo liliyumba gafla na kuifanya gari ya nyuma yao kuwagonga na zote zikaanza kubingiria kwenye barabara huku wezao wa nyuma wakijitahidi kuwakwepa. Mlipuko mkubwa ukatokea kwenye gari mbili hizo zilizo anguka, kidogo ikwa ni nafuu kwetu kwani tuliweza kuyaacha magari hayo kwa umbali mrefu kidogo.
“Adrus upo vizuri”
“Asante”
Madereva wa magari wanayo endesha hawakukata tamaa ya kuendelea kutufukuzia kwa nyuma, huku wakiendelea kutushambulia kwa risasi zao. Sikukuhitaji waweze kufika karibu nasi kwani inaweza kuwa ni tatizo kubwa, nilicho zidi kukifanya ni kuzidi kuwashambulia kwa risasi ambazo nilizieelekezea kwenye matairi ya magari yao. Mpango wangu uliweza kufanikiwa kwa asilimia mia moja, kwani gari zao zote ziliweza kusimama njiani na kutuacha sisi kuweza kupotea machoni mwao na tukiwaacha wakipiga risasi pasipo mafanikio ya aina yoyote.
Alfajiri majira ya saa kumi na moja na nusu tukawa tumeingia kwenye mji wa Karachi, tukafika kwenye kizuizi cha jeshi, ambacho gari zote zinazo ingia ndani ya jiji hilo nilazima kuweza kukaguliwa pamoja na watu waliomo ndani ya gari hizo. Naomi akawa wakwanza kushuka ndani ya gari huku akinyoosha mikono juu, kwani mitutu ya bunduki ya wanajeshi hao walio kuwemo kwenye kizuizi hichi waliielekezea kwetu, hii nikutokana na gari yetu kajaa matobo mengi yarisasi. Nikabaki ndani ya gari ili kuendelea kuusoma machezo mzima, kwani sikuweza kumuamini mtu yoyote japo hawa ni wanajeshi wa serikali ya hapa Pakistani.
Askari mmoja akamfwata Naomi alipo kiona kitambulisho alicho kishika Naomi, akawaamuru wezake kuweza kushasha silaha zao chini, kwa ishara Naomi akaniomba na mimi kuweza kushuka ndani ya gari na kumfwata sehemu alipo simama, akanitambulisha kwa askari huyo, nami nikatoa kitambulisho changu na kuwaonyesha, wakaridhika na sisi. Wanajeshi baadhi wakawa wanalikagua gari letu, na kumuona muhudumu wa duka akiwa ndani ya amelela na pingu zikiwa mikononi mwake
“Kuna mtu ndani ya gari?” Mmoja wa mwanajeshi alizungumza kwa sauti ya juu, na kuwafanya wanajeshi wengine wawili kulisogelea gari. Wakataka kumshusha ila nikawahi kuwafwata
“Musimshushe huyo ni muhalifu”
“Hamuwezi kupita na muhalifu, tutaamini vipi kwamba ni mualifu?” Mwanajeshi mmoja alinijibu kwa sauti ya ukali, huku aking’ang’ania kitasa cha mlango kuweza kumtoa muhudumu wa duka. Ikanilazimu kumsukuma mwajeshi huyo na kuwafanya wezake wawili kuninyooshea bunduki zao, kwa haraka na mimi nikatoa bastola yangu na kumuelekezea askari niliye msukuma na kupepepesuka.
“Mukifungua humo ndani, nitamwaga ubongo mwezenu” Nilizungumza kwa sauti ya kukoroma, iliyo jaa besi kubwa lililo mtisha hata mwanajeshi niliye msukuma. Akawaa mrisha wezake kushusha silaha zao chini, huku Naomi na wanajeshi wengine wakibaki wakitutizama. Wanajeshi hao wakasogea pembeni ya gari, nikafungua mlango na kutazamana na muhudumu ambaye fahamu zake zikiwa zimemrejea.
“What is your name”(Unaitwa nani?)
Nilimuuliza muhudumu wa duka, hakunijubu zaidi ya kunitemea mate ya uso. Nikajifuta mate yake hayo kwa kustukiza nikamtandika ngumi ya pua na kumfanya atoe ukelele mwengine wa maumivu.
“What is your fuc.. name?”
“Ally….Ally”
Alijibu huku machozi yakimwagika, nikaufunga mlango wa gari kwa kuubamiza na kumuacha ndani ya gari na mimi kurudi sehemu alipo simama Naomi na mwanajeshi mmoja anaye onekana ndio kiongozi kwenye kundi hili.
“Mumefikia wapi?” “Wamefanya mawasiliano na kule kambini, watakuja kutuchukua, hapa unaweza kulisogeza gari pembeni?” “Kuna usalama kweli hapa?” “Unaweza kuliigiza huku kwenye uzio wa geti”
Mwanajeshi huyo alizungumza, nikarudi kwenye gari nikaliwasha na kweda kulisimamisha kwenye moja ya maegesho ya magari ya jeshi. Kabla sijashuka nikamgeukia Ally, nikamtazama jinsi anavyo nitazama kwa macho ya hasira.
“UTAKUFAAAAAA” Ally aliniambia kwa lugha ya kiarabu, huku akihisi kwamba siielewi lugha hiyo, ambayo ni baadhi ya maneno ndio nilikuwa ninayasikia. Sikutaka azidi kuniletea dharau nikamtandika kofi la shavu huku nikizishika ndavu zake nfefu zilizopo kwenye kidevu na kuaanza kuzivuta kwa nguvu na kumfanya atoe ukelele umkubwa
“Eheee nitakufa si ndioo” Nilimjibu kwa kiarabu, kelele za Ally zikamfanya Naomi kuja sehemu tulipo huku akikimbia
“Adrus achana naye bwana”
Naomi alizungumza huku akinishika mkono nimuache Ally, kabla sijamuachia tukasikia milio ya risasi pamoja na milipuko ya mabomu yakitokea nje ya geti
“Hahaaaa mutakufaaa”
Ally alizungumza huku akicheka, hapo ndipo nilipo zidi kupandwa na hasira, nikamtandika ngumi ya shingo na kumfanya apoteze fahamu tena, kabla hatuka fanya chochote, gari ya tatu kutoka gari letu lilipo, likalipuka na kutufanya mimi na Naomi kuanguka chini.
ITAENDELEA
No comments:
Post a Comment