ILIPOISHIA
. Ukimya ukatawala ndani ya Helcoptar yetu, huku kila mmoja akiwa ameshika bunduki yake kwa umakini mkubwa, huku sote tukiwa tumevalia majaketi ya kuzuia risasi pamoja na makombati yanayo fanana, ila yetu kidogo yana utofauti wa chata kwenye mabega yetu ya kushoto yana bendera ya kijani na nyekundu na chini kuna maandhishi madogo ya P.S.S.
“Unatumia choclate?” Binti huyo aliniuliza huku akiwa ametoa choclate mbili mfukoni mwake
“Hapana” Akairudisha moja aliyo kua amekusudia kunipa mimi, kisha akaendelea kuila aliyo itoa, tukiwa katikati ya safari gafla tukasikia mlipuko mkubwa na mtingishiko mkali, jambo lililo ifanya helcoptar yetu kuyumba huku ikanza kuzunguka hewani ikionyesha kupoteza dira.
ENDELEA
Kila mmoja akawa makini katika kushikila katika sehemu aliyo hisi kwamba anaweza kushika, tukachungulia kwakupitia kwenye kioo cha mlango, nikashuhudia moshi mwingi ukitokea nyuma ya Helcoptar yetu iliyo endelea kuzunguka, na rubani akawa na kazi ya kujitahidi kuhakikisha kwamba anaiokoa helcpotar yetu iliyo anza kwenda mrama.
Helcoptar yetu ikaanza kuelekea chini kwa kasi ya ajabu, kila mmoja akaanza kusali sala yake kwani nilipo tazama chini niliona miti mingi ikiwa kwenye eneo hilo. Helcoptar ikaanza kujipiga piga kwenye miti na kutufanya tuliopo ndani ya helcoptar kuanza kugongana gongana, wengine nikawasikia wakisali sala zao za mwisho kwani Helcoptar yetu ndio iliyo shambuliwa kwa bumu.
Tukajikuta tunaanguka chini pasipo hata mto mmoja kutoka ndani ya Helcoptar. Moshi mwingi mweusi ukaaza kutanda ndani ya helcoptar na kunifanya niaze kuhooa, kwakutumia miguu nikaanza kuugonga mlango hadi ukachavunjika na kunipa nafasi ya kutoka ndani ya helcoptar huku nikitambaa chini.
“Help me”(Nisaidie)
Nilisikia sauti ya msichana akiomba msaada ndani ya helcopter, nikasimama kutoka sehemu nilipo na kurudi kwenye helcoptar nikachangulia ndani na kumuona yule dada aliye kuwa amekaa pembeni yangu akiwa amebalaliwa na miili miwili ya wanajeshi wezetu wanao onekana kupoteza maisha kwa ajali hii mbaya tuliyo ipata. Nikajitahidi kuwasogeza wanajeshi walio mlalia na kumtoa nje nikarudi kuchunguza kama kuna mwengine anaye weza kuwa hai, haikuwa hivyo wote walipata majeha makubwa yaliyo wafanya kupoteza maisha. Moto ukaanza kuunguza baadhi ya maeneo kwenye helcoptar, ikanilazimu kuweza kuondoka kwenye helcoptar na kumnyanyua binti huyu ambaye hadi sasa hivi silifahamu jina lake anaitwa nani. Kitendo cha kutembea hatua chache mlipuko mkubwa wa Helcoptar ukaturusha na kuanguka kila mmoja upande wake.
Kwa bahati nzuri sikuweza kuumia kwani nilirusha kwenye majani mengi, kwa haraka nikanyanyu kumkimbilia msichana aliye onekana kujeruhiwa kwenye paja la mguu wa kushoto, nikakuta kipande cha chuma kikiwa kimechoma kwenye paja lake. Nikachukua kijiti kinene kilichopo pembeni, nikamuomba aweze kuking’ata ili nitakapo mtoa chuma hicho maumivu makali yasipelekee meno yake ng’ata ulimi wake.
Nikachukua mkanda wa begi nilio ukata na kumfunga kwenye paja lake kuzuia damu kuendelea kumwagika
“Unaweza kutembea?”
Nilimuuliza kwa lugha ya kingereza
“Mmm nitajaribu”
Nikaokota bunduki yangu, kisha mkono wa kulia nikaupitisha kiunoni mwake, huku mko wake wa kushoto akinishika kwenye bega langu. Tukaanza kutembea kwa mwendo wa taratibu, huku tukitazama juu kama tunaweza kuweza kuona helcoptar ya wezetu ila hatukufanikiwa kuona chochote wala kusikia lolote
“Simama” Msichana huyo aliniambia kwa sauti ndogo ya kuashiria kwamba kuna kitu anahisi kinatembea, tukajibanza kwenye mti kusikilizia milio hiyo ni yawatu wanao tembea au ni miguu ya watu. Gafla tukawaona kundi kubwa la watu walio valia vilemba pamoja nguo za jeshi wakija katika eneo tulilopo huku mikononi mwao wakia na bunduki
“Shit Al quaida”
Msichana huyo ambaye hadi sasa hivi hatujuani majina alizungumza huku akiichomoa bastola yake kiunoni. Nikaikoki bunduki yangu haraka na kupiga goti moja chini.
“Moja, mbili, tatu piga”
Msichana huyo alininiambia, hapakuwa na jinsi yoyote zaidi ya kuanza kuwashambulia wanajeshi hao wanao onekana kuja sehemu helcoptar ilipo angukia. Wanajeshi hao baadhi wakatawanyika na kujibanza kwenye miti kujibu mashambulizi yetu huku wengine tukiwa tumewaangusha chini kwa risasi zetu
“Jina lalo nani?”
“Adrus” “Mimi ni Naomi”
Ilitubidi tutambulishane majina yetu kila tulipo kuwa tunajificha kwenye mti huu mkubwa kupokezana kusikilizia mashambulizi ya kundi hilo la kigaidi. Kusema kweli si kazi rahisi kushambuliana na watu wengi ambao hata idadi yao sikujua kwamba wapo wangapi kwani niliwaona wakija tu. Nikazidi kupiga risasi kwa uwezo wangu nilio barikiwa na Mungu
“Lete grenade” Naomi akaniomba bomu lakurusha kwa mkono, nakalivua begi langu nikamuambia afungue zipu atayakuta mabomu hayo. Akafanya kama nilivyo muambia mimi nikawa na kazi moja ya kuendelea kuwashambulia, Naomi akaanza kurusha mabomu hayo sehemu walipo wanajeshi hao ambao sipati picha pindi watakapo tutia nguvuni ninahisi itakuwa ni kilio cha kusaga meno
Tukazidi kupambana na kadri muda ulivyo zidi kuwenda ndivyo jinsi tulivyo zidi kuwashinda nguvu hadi wakaanza kukimbia.
Ikatulazimu na sisi kuweza kuondka katika eneo hilo kwani tukiendelea kukaa inaweza kuwa tatizo jengine kwetu. Tukatembea kama dakika tano na kufanikiwa kufika kwenye kijiji kimoja amacho kina nyumba zilizo jengwa kwa mawe na kusakafiwa kwa chokaa, watu wa sehemu hiyo wengi wanaasili ya kiarabu ila wanaonekana ni masikini sana, kwani mavazi yao ina ya mabaibui na kanzu yamachakaa, niwachache sana walio valia vizuri. Wakaonekana kutushangaa, kwani kilicho tusinda ni lugha zatu kugongana, wao wanzaungumza kiarabu na sisi tunazungumza kingereza.
“Nyinyi ni kina nani?”
Mzee mmoja aliyejazia ndevu nyingi alizungumza huku akitufwata sehemu tuliyo zungukwa na wananchi hao
“Sisi ni wanajeshi wakulinda usalama, tumepata ajali na helcoptar yetu ndio mana tumejikuta hapa” “Munatokea wap?” “Kwenye jeshi ya Pakistani” Mzee huyo akatutizama kwa macho makali, haswa macho yake akamtazama Naomi mwenye beji ndogo ya bendera ya Marekani
“Nifwateni”
Alizungumza na kuanza kutembea kuelekea kwenye nyumba yake, iliyo jengwa vizuri kidogo na anaonekana yeye ndio mkuu wa mji huu. Tukaingia ndani kwake na kushuka kwenye chumba kilicho jengwa chini ya ardhi, akatukaribusha kwa kutupa maji kwenye vikombe vya bati, kisha akamuita mke wake na kumuomba atuandalie chakula tule. Ukarimu wa mzee huyu ukatufanya tuanze kumuamini kidogo kwani, kila alilo tufanyia ni tofauuti snaa kama tungekutana na mwanajeshi wa kundi la Al-quida.
“Kwa jina ninaitwa Abdalah Salehe, nyinyi wezangu munaitwa nani?”
“Mimi naitwa Adrus”
“Mimi ni Naomi”
“Mbona niwadogo sana munaonekana, ila mumeingia kwenye vita ya dunia inayo washinda watu wengi” “Hatujakuelewa ndugu”
Nilizungumza huku nikiwa ninamtazama mzee huyo
“Ina maana kwamba munapambana na kikundi cha Al-quida ambacho si rahisi kuweza kukikamata kirahisi ikitegemea kingozi wao mulimuu” Mimi na Naomi tukajikuta tukikaa kimya kwani hatukuwa na utetezi wowote wakuzungumza
“Tuachane na hayo, ila tuliziona helcoptar zenu zikipita hapa majira ya asubuhi, sasa na uelekeao ambao mulikuwa munaelekea ni ule ambao kuna kambi ya kukundi hicho, na kina kila aina ya silaha mbaya hadi mabumu ya nyuklia, sasa hamkufanya uchunguzi kabla ya kwenda?” Maswali ya Mzee Abdulah Salehe, yakatufanya tuzidi kupata vigugumizi” “Adeus wewe ni muislam” “Ndio” “Ahaa, nilipo kuangalia tu, nilitambua kwamba wewe upo kwenye hiyo dini. Huko mulipo toka msituni ilikuwaje?”
Ikabidi nimsimulie Mzee Abdalah kila kitu kilicho tokea, hadi tukajitoa mikononi mwa watu hao
“Nilazima watafwata ulekeo wenu, na laiti kama watajua mupo hapa nilazima watakuja kukiangamiza kijiji hichi, watu hao hawana huruma hata kidogo”
“Inabidi mufanya kuondoka katika hichi kijiji la sivyo wananchi wangu wote watauliwa” Mzee Abdulah aliendelea kusisitizia na kutufanya tuzidi kupata wasiwasi mwingi kwenye mioyo yetu.
“Nitakacho wasaidia ni kuwapa usafiri wa gari litakalo wafikisha hadi Karachi, huko munaweza kutafuta njia ya kujiokoa”
“Tutashukuru sana”
“Laiti ingekuwa si wewe kuwa dini moja na mimi, nisinge wasaidia kabisa. Dini yako imekusaidia bwana Adrus”
“Asante sana”
Ilinibidi kujinyenyekeza ili kuendelea kupata nafasi ya kuyaokoa maisha yangu mimi na Naomi ambaye ninatambua kwamba yeye ni mkristo japo wapo Manaomi ambao nao ni waislam. Chakula chetu kilicho andaliwa kikafungwa kwenye mfuko wa lailon, tukazunguka nyuma ya nyumba ya Mzee Abdulah na kukuta gari mbili aina ya picup. Akanipa funguo ya gari Toyota hardbod, ambayo bado ni mpya kabisa, nyuma ya bodi ya gari hilo kuna madungu mawili yamafuta ya petrol, akatupa na ramani ambayo ingetuwezesha kufika kwenye mji wa Karachi pasipo matatizo ya aina yoyote. Hatukuwa na muda wakupoteza zaidi ya kumshukuru Mzee Abdulah, tukaondoka na kushika njia ambayo mzee huyo alituonyesha tuweze kuondokea
Saa yangu ya mkononi inanionyesha ni saa kumi na mbili jioni, na bado safari yetu inachukua masaa mengi, sana hadi kufika kwenye mji huo. Njia nzima moyoni mwangu nikawa ninamshukuru Mzee huyo kwani pasipo yeye sijui hadi muda huu tungekuwa wapi.
Tukakatiza kwenye vijiji mbalimbali, milima na mabonde, Naomi alilala akaamka ila akanikuta nikiwa bado ninaendesha gari. Kila nilivyo zidi kwenda ndivyo nilivyo zidi kupata matumaini ya kuyaokoa maisha yatu, Kwani tuliweza kukutana na magari mengine ya watu binafsi kwenye barabara niliyokuwa ninakwenda kwa kufwata ramani niliyo iweka pambeni yangu
“Adrus haujachoka?”
Naomi aliniuliza huku akipiga miayo, saa ya mkononi ikawa inanionyesha ni saa tano usiku,
“Hapo mbele ramani inanionyesha kwamba kuna mji mkubwa itabidi tulale hapo”
“Sawa, ila mguu wangu sasa hivi unazidi kuvuta”
“Pole sana”
“Asante”
Kweli ndani ya dakika kumi na tano tukakuta mji mkubwa ulio changamka kwa wingi wa watu pamoja na maduka makubwa, nikasimamisha gari nje ya duka moja kubwa linalo onyesha linauza vinjwaji baridi, Kutokana mfukoni ninanoti mbili za dola mia mia, nikaona zitanisaidia. Kabla ya kushuka kwenye gari nikavua jaketi lakuzudia risasi pamoja na kombati la juu na kubakiwa na tisheti ya ndani pamoja na suruali
“Vipi mbona unavua nguo hizo?” “Nahofia kama kuna maadui isiwe rahsi kunivamia” “Ahaa kuwa makini”
“Poa nilinde”
Nikashuka kwenye garni huku bastola zungu tatu nikiwa nimezichomeka sehemu tofauti tofauti za mwili wangu, kuanzia kwenye kiuno kwenye mguu nilio vaa viatu virefu vya jeshi. Haikuwa nirahisi kwa mtu kuweza kuziona bastola zungu, nikaingia ndani ya duka huku nikiwa ninamtizama kwa kuiba kila aliye nitazama. Nikafika kwa muhudumu, hapakuwa na kinywaji kingine zaidi ya cocacola, ambavcho ndio nilikijua mimi, nikaagiza soda hizo zilizomo kwenye ijazo wa machupa makubwa kisha nikampa muhudumu dola mia
“Hapa hatutumii dola” Alizungumza kwa lugha ya kingereza, taarifa iliyo kuwa ikionyeshwa kwenye tv ikanifanya nisimjibu muhudumu hoyo na kubaki nikiwa niitazama kwa umakini, Ilionyesha kwamba helcoptar zaidi ya kumi na nane za jeshi, zimeweza kushambuliwa na kikundi cha Al-quida, Wanajeshi wote walio kuwa kwenye helcoptar hizo inasemekana wamekufa. Nikasikia sauti ya muhudumu waduka akionekana kufurahia tukio hilo.
“Unachekelea nini?” “Mimi siwapendi hao wanaharamu, wamarekani safi sana Al-quida Mungu awazidishie” Kwa hasira nikachomoa bastola yangu na kumuelekezea muhudumu huyo wa duka, ila akaonekana kujiamini sana, nilipo geuka nikakuta watu si chini ya ishirini wakiwa wamenielekezea bunduki zao na wote ni wale ambao walikuwa wakinifwatilia tangu nilipokuwa niikiingia ndani ya duka hili
ITAENDELEA SEHEMU YA NNE USIKOSE Tembelea www.alfachengula.blogspot.com
No comments:
Post a Comment