ILIPOISHIA
Tv hiyo ikaonyesha kamera za ulinzi zinazo chukua matukio ya nje. Sote tukaona magari mengi ya wapiganaji wa Alquida, wakipambana na wanajeshi walipo kwenye mageti. Ila kadri sekunde zinavyo zidi kusonga mbele ndivyo jinsi wanajeshi wa kimarekani waliopo magetini wanavyo kufa kwa kupigwa risasi.
“Muheshimiwa inatubidi tuondoke muda huu” Jamaa huyo ambaye ni kwa haraka haraka nikagundua ni mlnzi wa balozi alizungumza, balozi akatutazama usoni mimi na Naomi, tulio baki tukitazama video hizo za mambo yanavyo endelea nje, jinsi wapiganaji wa kikundi hicho wanavyo zidi kusonga ndani jengo la ubalozi huu wa Kimarekani tulipo mleta Ally moja wa kiongozi wa kundi hilo linalo ogopwa karibia na nchi zote duniani.
ENDELEA
“Ngoja nipige simu kwenda Marekani, niombe msaada” “Muheshimiwa mitambo yote ya simu imesha haribiwa” “Yesu wangu” “Tutakulinda kadri tuwezavyo muheshimiwa” Nilizungumza na kumfanya mwana mama huyo kunitazama, akashusha pumzi. Akatembea hadi kwenye kabati lake kubwa, akaingiza namba za siri kwa kuminya batani zilizipo katika mmoja wa mlango wa kabati hilo. Lilipo funguka, akaanza kutoa bastola moja baada ya nyingine na kutupatia kila mmoja ya kwake. Nikahakikisha bastola yangu ina risasi za kutosha, nikakuta zipo zimejaa kwenye magazine. Jamaa huyo akafungua mlango wa kutokea ofisini hapo, akatazama kila sehemu, kwa ishara akatomba tutoke. Nikamtazama Naomi na kumkonyeza huku nikumyashusha macho yangu kwenye mguu wake wenye jeraha. Naye pia akayashusha macho yake hadi kwenye jeraha hilo kisha akanitazama. Akaninyooshea dole gumba na kunitaarifu kwamba yupo safi. Tukatoka huku tukiwa tumemuweka balozi katikati, mama huyo naye pia akabeba bastola yake. Kila tulivyo zidi kwenda ndivyo tulivyo zidi kuisikia milio ya risasi ikirindima huko nje.
“Njia hii” Jamaa huyo alituongoza na kuingia kwenye moja ya mlango ambapo tukakuta ngazi za kueleka chini. Tukashuka na kuingia kwenye moja ya chumba ambacho kipo chini ya ardhi. Tukakuta gari maalumu ambalo lipo katika eneo hili, na linatumika kama dharura pale kunapo tokea hali ya hatari kama hii.
“Hapana siwezi kuondoka na kumuacha huyo Ally” Balozi zlizungumza na kutufanya sote tumkazie macho.
“Muheshimiwa hilo hatuwezi kulifanya tena kuna hatari kubwa sana mbele yetu” “Nimesema siwezi kuondoka na kumuacha huyo gaidi ni lazima tumfikishe Marekani” “Naomba munielekeze mimi nitamfwata” Niluzungumza kwa kujiamini na kumfanya Naomi kunizidi kunitazama kwa macho ya mshangaa. Balozi akanitazama usoni mwangu, nikatingisha kichwa kumdhibitishia kwamba nipo tayari kwa kuifanya kazi hiyo.
Balozi akatoa kadi yake ndogo na kunikabidhi.
“Kadi hii ni yakufungulia milango, yote katika jengo hili la ubalozi. Jerry nenda naye” “Sawa mkuu” Hapo ndipo nikatambua kwamba huyu mlinzi wa balozi anaitwa Jerry. Naomi akataka kuongozana nasi ila nikamuzia.
“Adrus kuwa makini” Naomi alizungumza kwa sauti iliyo jaa hisia nzito za mapenzi. Akashindwa kujizuia kabisa akanisogelea na kunipiga busu la mdomoni na kumfanya balozi kutabasamu. Tukaondoka na Jerry na kurudi juu. Milipuko ya mabomu ikazidi kurindima huku baadhi ya jengo zikiaharibiwa kwa kiasi kikubwa. Tukaingia kwenye jukumu la kushambulia wapiganaji hao ambao tayari walisha ingia kwenye jengo. Mimi na Jerry tuakazidi kusonga mbele kuhakikisha kwamba tunaweza kufika katika chumba alicho fungiwa Ally. Hatukuchukua mud asana tunakwa tauari tumesha fika kwenye chumba hicho kilicho jengwa kwa uimara mkubwa sana. Kwa kutumia kadi ya balozi tukafungua milango minne ya chumba hicho, ambayo ni lazima kuifungua na ndio uingie ndani ya chumba hicho. Ally aliponiona akaanza kutabasamu huku akicheka kwa dharau.
“Puuuuuuuu” Alitoa mlio wa kulipuka kwa bomu huku akinitishia mimi. Nikamtandika ngumi na kuanza kumnyanyua kutoa sehemu alipo kaa. Tukaanza kutoka naye hapo huku Jerry akiwa ametangulia mbele Ally tuukimuweka katikati na mimi nikifwata kwa nyuma, huku bastola yangu nikiwa nimeishika kwa umakini. Tukasikia sauti za waarabu hao zikisema yupo huku.
“Wanakuja huku, tupite njia hii?” Jerry akapita kwenye moja ya kordo, mimi na Ally aliye fungwa pingu za mikononi pamoja na mnyororo mrefu kwenye miguu yake tukamfwata. Tukiwa katika kutembea mgongoni mwa Ally ambapo kuna sehemu nguo yake imechanika kidogo, nikaona mshono wa mdogo.
“Ana kifaa huyu, popote tuakapo kwenda nilazima wajue” Nilimuambia Jerry aliye simama, akapiga hatua hadi sehemu alipo simama Ally, akamgeuza na kutazama mshono huo, kwa haraka Jerry akatoa kisu chake akampiga mtama chini Allye aliyekuwa akileta ubishi ubishi. Akaanza kumpausua sehemu hiyo na kweli akatia kifaa kidogo ambacho kinatumika kumuonyesha sehemu anapo kwenda, na ndio maana ikawa raisi kwa wezake kufahamu sehemu alipo na kujipanga na kuja kushambulia machana kweupe.
Jerry alipo maliza akamnyanyua Ally na kifaa hicho akakiacha sehemu hiyo yo kisha tukuendelea na safari ya kuellekea alipo balozi pamoja na Naomi. Kutokana na uzoefu wa Jerry katika jengo hilo tukafanikiwa kufika katika eneo walipo balozi pamoja na Naomi. Hatukupoteza muda tukaingia kwenye gari na safari ikaanza kwa kasi huku Jerry akiwa dereva wa gari hili.
Tukatokea mali kabisa na sehemu lilipo jengo la ubalozi, balozi ailkaa mbele huku mimi na namoni tukiwa tumekaa nyuma pamoja na Ally tuliye muweka katikati ya siti. Jerry akakatisha kwenye mitaa hadi tukafika katika jengo jingine lililo andikwa ubalozi wa Ufaransa. Jerry Akashuka na kwenda kuzungumza na wanajeshi waliopo kwenye geti hilo. Hawakuchukua hata dakika moja wanajeshi hao wakaongozana na Jerry hadi kwenye gari. Tukashusha vioo vya gari, wakamsalimia balozi kisha wakaturuhusu kuingia ndani ya ubalozi huo ambao una ulinzi mkali kama ubalozi wa Marekani tulio toka.
Jerry akaelekea na Allye pamoja na wanajeshi wengine kwenyes ehemu ambayo hatukuelezwa mara moja. Tukaongoznaa na bolozi hadi kwenye ofisi ya bolozi wa Ufaransa. Wakasalimiana na mzee huyo mrefu mwenye mwili mwembaba kiasi. Akaanza kuututambulisha na kumuelezea kazi nzima ambayo tumeifanya hadi muda.
“Hongereni”
“Asante mkuu” “Hawa vijana wanatakiwa kuridi kambini, kwao kuchukua kila kilicho chao” “Kwa nini?” Mwana mama uyo akamueleza balozi mwenzake amri iliyo toka Marekani, basi hapakuwa na muda mwengine wa kusubiri. Tukakabidhiwa kwa marubani wawili wa helcoptar. Tukaingia kwenye helcoptar hiyo ya kijeshi iliyo tengenezwa kwa uimara mkubwa. Safari ya kuelekea kambini kwetu ikaanza. Ndani ya helcoptar hatukuzungumza chochote mimi na Naomi. Ndani ya dakika ishirini tuawa tumefanikiwa kufika kwenye kambi yetu. Tukapokelewa na kiongozi ambaye tayari alisha pewa taafira. Tukapanda magari tofauti na kuelekea kila mmoja kwenye sehemu yalipo majengo yao kutoka mimi na Naomi tunaishi kwenye majengo tofauti na yapo mbali kutoka katika uwanja wa ndege.
Nikafika katika jengo letu, ambalo hadi sasa hakuna mtu hata mmoja ambaye yupo kutokana wote wameelekea kwenye oparesheni maalumu ya kuangamiza kikosi cha wapiganaji wa Alquida. Nikachukua karatasi kubwa iliyopo kwenye begi langu. Nikatoa na kalamu ya rangi na kuanza kuandika maandishi ambayo kwa upande mmoja yanauumiza moyo wangu.
(TULIKUWA PAMOJA KATIKA MAFUNZO HADI KWENYE OPARESHIENI HII, KAMA NILIVYO WAAHIDI MUNATAKIWA KURUDI MUKIWA HAI. ASIFE HATA MMOJA WENU. NIMEFANIKIWA KUMKAMATA ALLY GAIDI NA KIONGOZI WA KIKUNDI HICHO. KWA JAMBO HILO SERIKALI IMEAMUA KUNITOA KATIKA OPARESHENI NA KUNIRUDISHA NCHINI TANZANIA. NAWAPENDA NA TUTAONANA. BY ADRUS MALDIN) Nilipo maliza kuyaandika maneno hayo nikatafuna moja ya bablishi niliyo ikuta kwenye begi langu. Nilipo hakikisha imelainika nikaitoa na kuiweka katika sehemu nne za karatasi hilo na kuibandika ukutani. Karatasi hilo lilipo kaa vizuri nikalifunga begi langu na kulinyanyua na kulivaa mgongoni. Nikatoka nje na kuingia kwenye gari hili la njeshi ambalo kwa juu halijafunikwa. Safari ya kurudi kwneye uwanja wa ndege. Tukafika na kumkua Naomi akiwa tayari amesha fika akiwa na begi lake kubwa la mgongoni. Tukaingia kwenye helcoptar iliyo tuleta na safari ya kuelekea kwenye ubalozi wa Ufaransa ikaanza.
“Adrus” “Mmmm” “Nitakukumbuka sana” “Hata mimi pia nitakukumbuka pia” Naomi akatoa kalamu na karatasi ndogo akaandika namba yake ya simu pamoja na email ambayo atakuwa anaitumia Marekani. Japo tumetoka kambini ila safari hii imejaa huzuni kubwa kati yetu kwani ndio kwanza mapenzi yetu yamechipua ila kazi na utaifa zinatutengenisha kati yetu. Akanikabidhi kikaratasi hicho huku machozi takiwa yanemlenga mlenga. Nikakipokea na kukiweka kwenye mfuko wa pembeni ya begi langu. Kutokana kwenye siti tulizo kaa yumejifunga mikata maalumu, hatukuweka kukumbatiana. Tukafika katika ubalozi wa Ufaransa, tukapokelewa na balozi wa Marekani, aliye tuchukua moja kwa moja hadi kwenye moja ya chumba. Akatupa kila mmoja bahasha ndogo tukabaki tumemkodolea macho, kwa ishara akatuomba kuweza kufungua bahasha hiyo.
Kila mmoja akafungua bahasha, tukakuta hati za kusafiria pamoja na karatasi ndogo ambayo ni cheki iliyo andikwa pesa za kimarekani dola laki moja.
“Hiyo pesa itawasaidia huko muendapo, nimetoa mimi kama zawadi yangu kwangu, kwa kuweza kuyaokoa maisha yangu. Pia munaweza kuitoa kwenye nchi yoyote ila iwe na benki ya Standard Chaterd” “Asante sana muheshimiwa” “Musijali, tiketi zenu za ndege zinaletwa muda si mrefu” “Sawa mkuu” “Ila nina zawadi moja kati yenu, ngoja atakaye leta tketi za ndege nitawaambia.” “Sawa”
Tukakaa na mwana mama huyo ndani ya chumba hicho huku tukizungumza mambo mengi kubwa likiwa juu ya huyu gaidi tuliye mkamata, baada ya dakika kumi, mlango ukafunguliwa anakingia Jerry, akiwa na bahasha moja, akamkabidhi balozi kisha akatoka. Balozi akatoa bahasha hizo na kutoa tiketi mbili za ndege.
“Nimewakatia tiketi mbili. Nyote mutaelekea nchini England, kuna hoteli kule nimewachukulia. Mutakaa hapo kwa siku tatu kisha siku ya nne, mutaondoka Adrus utaelekea Tanzania. Naomi utaeleka Marekani, sawa” “Sawa mama” Tulijikuta mimi na Naomi tukizungumza kwa pamoja, huku nyuso zetu zikiwa zimejaa furaha. Tukazipokea tiketi hizo kwa furaha.
“Kingine mutapokelewa na balozi wa Marekani huko Uingereza, Naomi si unamfahamu?” “Ndio namfahamu” “Sawa yeye ndo atakaye wapokea na atawapeleka kwenye hiyo hoteli, na yeye ndio atakaye shuhulika na swala la kuwakatia tiketi za kuelekea nchini mwenu” “Shukrani sana” “Ila jitahidini kutafuta mtoto” Maneno ya mwana mama huyo yakatufanya sote kucheka huku tukiwa tumejawa na aibu kwneye nyuso zatu. Tukatoka kwenye chumba hicho tukiwa na mabegi yutu. Akatukabidhi kwa Jerry, tukaagana naye kisha tukaongozana naye Jerry hadi nje, ambapo tukakuta gari moja aina ya Range Rover ikiwa inatusubiri na ndani yake kuna dereva. Mabegi yetu yakawekwa nyuma ya gari hilo kisha tukapanda siti za nyuma na kuondoka kwenye ubalozi huo. Safari ikaanza huku ndani ya gari muda wote tukiwa tumeshikana mikono na Naomi. Tukafika uwanja wa ndege moja kwa moja tukaelekea sehemu ya kukaguliwa. Bastola zetu hazikuwa kikwazo kwetu kutonana sisi ni wanajeshi, tukakabidhiwa bastola hizo tulipo pita katika upande wa pili wa kukaguliwa.
Tukabeba mabegi yetu, tukaongozana na muhudumu wa hapa uwanja wa ndege akatupeleka moja kwa moja kwenye ndege ambayo ndio tunayo safiria.
Muhudumu huyo akatukabidhi kwa muhudumu mwengine anaye shuhulika na ndege hiyo, akatupeleka kwenye siti zetu ambazo zipo sehemu moja. Naomi akaka dirishani na mimi nikaka pembeni yake.
“Asante Mungu” Naomi alizungumza huku akishusha pumzi nyingi sana. Nikamshika mkono taratibu nikamsogelea na kumpiga busu la shavuni, akanigeukia na kuanza kuninyonya lipsi zangu.
“Samahani, naomba mufunge mikanda” “Ohoo sawa, hakuna tatizo” Tukafunga mikanda kama muhudumu huyo wa ndege alivyo zungumza. Taratibu ndege ikaanza kuondoka, huku ndani ya ndege kukiwa na abiria wengi sana. Taratibu ndege ikaanza kuacha ardhi na kuwa hewani Safari sasa ikaanza rasmi kueleka Uingereza, moyo wangu ukaanza kusali sala huku nikimkumbuka marehu baba yangu, ambaye naye alikuwa ni askari.
‘Baba nimefanikiwa’
Nilijisemea kimoyo moyo pasipo Naomi kusikia chochote. Masaa yakazidi kukatika taratibu Naomi akapitiwa na usingizi. Akakilaza kichwa chake kwenye bega langu kitendo kilicho nifurahisha sana.
“Baby” Nilimuita Naomi aliye lala muda mrefu ulio pita.
“Kumepambazuka” “Kweli?”
“Ndio” Dirisha la pembeni la ndege liliweza kuingiza mwanga, kwani safari ilianza usiku. Safari ya kutoka bara moja kwenda bara jengine inachukua masaa mengi kiasi. Ila kwa uvumilivu tukafanikiwa kufika nchini Uingreza alfajiri na mapema. Kama alivyo tueleza balozi wa marekani nchini Pakistani, ndivyo jinsi inavyo kuwa. Tukapokelewa na balozi wa Marekani nchini Uingereza.
“Naitwa David Rutha” Alijitambulisha na sisi tukajitambulisha, tukaingia kwenye gari alilo kuja kutupokea pamoja na walinzi wake. Gari tatu zikaongozana huku sisi tukiwa tumepanda gari la nyuma, na balozi huyo upo gari la katikati. Tukafika katika mji wa London, akatupeleka kwenye moja ya hoteli.
“Hapa ndipo mutakapo kaa kwa siku tatu vijana” “Shukrani muheshimiwa” “Mukiwa na tatizo lolote muwasiliane nami”
Akatukabidhi kadi moja ndogo yenye namba zake za simu. Tulipo kabidhiwa funguo ya chumbani. Tukaagana naye na yeye akaondoka. Tukasaidiwa na muhudumu wa hoteli kubebe mabegi yetu. Tukaingia kwenye lifti na kuelekea gorofani kilipo chumba chetu. Nikafungua mlango wa chumba chetu na muhudumu akatangulia akaingiaza mabegi yetu kisha akatoka. Nikaufunga mlango wa ndani kisha nikamsogelea Naomi sehemu alipo simama, tukakumbatiana na kuanza kunyonyana midomo yetu.
“Kazi yetu iliyo tuleta hapa ni nini?” Naomi aliniuliza huku akiendelea kunivua nguvo zangu na mimi nikifanya kama anavyo fanya.
“Ni kutafuta mtoto” “Yeahaa nipe mtoto Adrus” Naomi alizungumza huku akinisukumiza kitandani kisha akapanda na kunikalia kiunoni mwangu na kuendela kunyonyana lipsi zetu tukiwa tumejawa na furaha sana.
No comments:
Post a Comment