MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Monday 12 June 2017

RAIS MAGUFULI ATOA AGIZO KWA KWA BUNGE LA TANZANIA

Raisi Magufuli leo amepokea ripoti ya awamu ya pili iliyounda kwa ajili ya kufanya uchunguziya mchanga wa madini ikifahamika kama Makinikia,ambapo Rais ameahidi kuwa sheria zote za madini zinapaswa kupitiwa tena na kurekebishwa na bunge ili ziweze kuleta tija kwa Watanzania.
‘Mhe. Spika Job Ndugai nitakuletea mizigo hii bungeni, lakini kwa wale wanaoropoka bungeni naona unaenda vizuri nenda na mwendo huo huo, maana wakiwa kule wanaweza kutukana wanalindwa na kinga ya bunge, ila ukiwatimua mwezi mzima wataropoka nje ya bunge, mimi nitadili nao vizuri. Siwatishi bali nawaambia ukweli huwezi kuwa unamrudisha watu nyuma kwenye vita hii, kama huna la kusema ni bora ukae kimya” alisema Rais Magufuli
Mbali na hilo Rais Magufuli alikubaliana na mapendekezo yote 20 ambayo yameletwa na Kamati hiyo maalum chini Mwenyekiti Prof. Nehemiah Eliachim Osoro ikiwa ni pamoja na baadhi ya Mawaziri pamoja na viongozi wote waliohusika katika kusaini mikataba hiyo kutafutwa popote walipo na kuhojiwa na vyombo vya dola.
“Wahusika wote waliotajwa kwenye ripoti hii vyombo vya dola viwahoji na kujua ukweli juu ya jambo hili, hata kama wapo serikalini au wapo wanafanya biashara zao wahijiwe tu, maana wengine wamekuwa wafanyabiashara wakubwa kumbe wanatumia pesa zetu Watanzania ili kama hizo pesa zetu tuzichukue tu” alisisitiza Magufuli

No comments:

Post a Comment