MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Thursday, 6 July 2017

MAONESHO YA SABASABA 2017; BABA AMSAJILI MWANAE WA MIAKA 18 NA MPANGO WA "WOTE SCHEME" WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF

 NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
BWANA Sukulu Mageta akiwa na mkewe Diana wote wajasiriamali wakiwa na watoto wao, Msuya S Mageta (18) na Ng'washi S Mageta, aliamua kutumia muda wake mchache kutembelea banda la Mfuko wa Pensheni wa PPF, ili kujua nini hasa anachoweza kufaidika nacho endapo atajiunga na Mfuko huo.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bi. Jannet Ezekiel ndiye aliyekuwa na jukumu la kutoa "darasa" kuhusu faida za kujiunga na PPF kupitia mpango wa WOTE SCHEME, ambao ni maalum kwa wanachama wanaojiunga kwa uchangiaji wa hiari, mpango unaowahusu wajasiriamali, mama lishe, bodaboda na mgtu yeyote anayefanya kazi ya kumuingizia kipato na uwezo wa kuchangia kila mwezi angalau shilingi elfu 20.
Bi Jannet aliieleza familia hiyo kuwa mwanachama wa mpango wa wote scheme, atafaidi Mafao mbalimbali yakiwemo, Mafao ya afya, ambapo sifa ni mwanachama kuchangia kwenye Mfuko kiasi kisichopungua shilingi elfu 60,000/=kwa kigezo hicho mwanachama atapatiwa kadi kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), ili kuweza kupata huduma ya afya sawasawa na wanachama wengine wa NHIF kutoka hospitali zilizoanishwa. Lakini pia Mkopo wa Elimu, ambapo sifa kubwa ni Mwanachama kuchangia katika Mfuko kwa kipindi kisichopungua miezi sita na marejesho ya Mkopo huu yatafanyika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja au katika kipindi kisichopungua miaka mitano (5). Alisema Bi Jannet. Baada ya kupatiwa elimu hiyo, Bw. Sukulu aliamua kumuandikisha kijana wake wa mika 18 Msuya S. Mageta kujiunga na mpango huo wa WOTE SCHEME, kwa lengo la kujiwekea akiba ili afaidike na Mkopo wa elimu.
 Bi Jannet Ezekiel akimkabidhi fomu ya kujiunga na Mpango wa Wote Scheme kijana Msuya S. Mageta. Katikati ni baba mzazi wa Msuya, Sukulu Mageta
Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa PPF, Bi. Pauline Msanga, akichapa kazi.
 Afisa Msaidizi Huduma kwa Wateja, Mohammed Siaga, akifanya kazi.

 Afisa Mtafiti wa PPF, Elaine Maro (kulia), akimpokea kwa bashasha mwanachama huyu aliyefika kupatiwa taarifa za michango yake
 Baada ya muda mchache mwanachama huyo anapata taarifa yake na ufafanuzi pia
 Afisa Mafao wa PPF, Bi. Tulla Mwigune, (kushoto), akimpatia maelezo mwanachama huyu aliyefika kwenye banda la Mfuko huo
 Meneja wa elimu kwa wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kwame Temu, (kushoto), akimkabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko huo kupitia WOTE SCHEME, Nuru Luvinga
 Meneja wa elimu kwa wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kwame Temu, (kushoto), akimkabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko huo kupitia WOTE SCHEME, Martin Mtenga.

No comments:

Post a Comment