Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma bora na nafuu za matangazo ya dijitali nchini, StarTimes, inawatangazia wateja wake na watanzania kwa ujumla kutembelea banda lao kwenye maonyesho ya 41 ya Sabasaba.
StarTimes inawapa wateja ving’amuzi vya bei rahisi vilivyounganishwa na kifurushi cha bure kwa mwezi moja kwa shilingi 78,000 kwa dishi na 47000 kwa antena.
Pia wateja wataweza kununua televisheni ya kidigitali kwa bei nafuu zaidi na kupewa punguzo la asilimia 8% ambapo kutakuwa na inchi 40,32 na 24 yenye kingamuzi ndani yake na kukupa chaneli zaidi ya 100 za kitaifa na kimataifa ili kufurahia ulimwengu wa kidigitali .
Mbali na hayo,kutakuwa na bidhaa nyingine kama simu za kisasa na projekta ambazo zinapatikana kwa bei nafuu ambayo kila mtanzania anaweza kumudu.
Lengo la kufanya hivi ni kumuwezesha kila mtanzania aweze kumudu gharama za matangazo na kufurahia ulimwengu wa kidijitali.
Pia tungependa kuwahamasisha wateja wetu kulipia vifurushi tulivyonavyo ili kuweza kutazama chaneli na vipindi vingi zaidi tulivyonavyo vya kitaifa na kimataifa.
Hata hivyo, wateja wa StarTimes wanafurahia matangazo ya moja kwa moja ya kombe la mabara, Mwezi ujao tutaanza kuonyesha kombe la mabingwa kimataifa (ICC), ligi kuu ya ujerumani (Bundersliga),ligi kuu Italia (Serie A), ligi kuu Ufaransa (League 1) na mwakani kombe la dunia litakalofanyika nchini Urusi.
Tunazo tamthiliya, filamu za kiafrika na ulaya, kichina kihindi, vipindi vya watoto na kadhalika.Vilevile utaweza kuangalia chaneli zaidi ya 37 mubashara na Bure kupitia APP yetu inayopatikana kupitia Google store, App store auwww.startimestv.com.
Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania, David Kisaka akifafanua utendaji kazi wa bidhaa zilizopo kwenye banda la kampuni hiyo kwa wateja waliofika kujionea, kununua na kupata ofa zao.
Mfanyakazi wa Kampuni ya StarTimes Pauline Kaka akimwandaliwa mteja TV ya Kisasa baada kuinunua katika banda lao kwenye maonesho yanayoendelea ya 41 Sabasaba Dar es Salaam leo
No comments:
Post a Comment