Kwa niaba ya shafiiNad blog napenda kuomba radhi kwa taarifa ambayo ilitolewa kupitia website ambayo ilionekana imehakiwa na matapeli .
Maelezo kamili ni kuwa kampuni ni ya halali na mimi nawaelezea kuwa niliogopa ile website nyingine nje ya tssf.or.tz ambayo ndio naifahamu, naomba niwaelezee kuwa kampuni ina website nyingine tofauti na hii ninayo ifahamu mimi na kwa urahisi ni kuwa hata ile website nilityosema sio yao wameniambia ni yao kwa kuitangaza hadi kwenye page yao.
Naombeni samahani kwa usumbufu ulio jitokeza, niliandikwa kwa uoga wa kutapeliwa watu wengine kama mimi nilivyowahi tapeliwa kwenye vikoba ambapo walitumia hiyo hiyo weebly.com kama ndio hosting wao.
Na naomba wanachi wenzangu makala ile nimeifuta kwa sababu za kiusalama zaidi katika kampuni hii lakini pia kwa kuonesha nimakosa niliyafanya.
Lengo halikuwa kuchafua kampuni, bali lilikuwa ni kujaribu kuepusha matapeli wasitapeli watu kama ambavyo hutumiaga majina na kampuni za kuaminika katika kuibia watu.
Natanguliza ombi langu la. Msamaha kwa wana TSSF wote,
Tafadhalini sana naombeni sambazeni na huu ujumbe ili kurekebisha makosa na kuondoa hofu ambayo niliwajengea wa tanzania wenzangu
IMETOLEWA NA SHAFI MMILIKI WA SHAFIINAD BLOG
No comments:
Post a Comment