MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Saturday, 4 November 2017

WANAFUNZI 7,901 WAPANGIWA MIKOPO KATIKA AWAMU YA TATU KWA 2017/2018

WANAFUNZI 7,901 WAPANGIWA MIKOPO KATIKA AWAMU YA TATU KWA 2017/2018

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imetoa orodha ya Awamu ya Tatu ya wanafunzi 7,901 wa Mwaka wa Kwanzawaliofanikiwa kupata mikopo na hivyo kufanya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo hadi sasa kufikia 29,578. Katika Awamu ya Kwanza, wanafunzi 10,196 wa mwaka wa kwanza walipangiwa mikopo na Awamu ya Pili wanafunzi 11,481.
Orodha hiyo ya Awamu ya Tatu inapatikana hapa.  Aidha, orodha hii inapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz) na itatumwa kwa vyuo husika.
Kiasi cha shilingi 427.54 bilioni zimetengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka 2017/2018 na tayari Serikali imeshatoa shilingi 147.06 bilioni kwa ajili ya robo ya kwanza ya mwaka huu wa 2017/2018.

No comments:

Post a Comment