Katibu Mwenezi wa ccm Wa Mkoa Njombe Ndugu Erasto ngole siku ya jumanne alikuwa mgeni rasmi katika sherehe ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya wazazi wilayani ludewa katika sherehe hizo zilizo fanywa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimabli akiwemo mkurugenzi na katibu wa jumuiya ya wazazi ccm mkoa wa njombe ambaye kwa nafasi yake aliweza kukutana na mkurugenzi na wakateta faragha namna ya kuinusulu shule sekondari ya wazazi iliyoko wilayani ludewa mkoani Njombe. Ndugu Erasto ngole Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi amesikitishwa na mazingira mabovu yasiyo rafiki kwa wanafunzi ambayo wazi yanapelekea kushuka kwa taaluma kwa kupungua kwa ufaulu kwa wanafunzi wengi wanao soma katika shule hiyo. mazingira hayo hafifu yamepelekea kuwepo na uamuzi wa kuifunga shule hiyo ambayo ilikuwa msaada mkubwa kwa vijana waliotambua na kuelewa dhamani ya elimu kama urithi pekee ambao utaweza kuwasidia vijana wetu kwa siku za usomi kwa ajili kuandaa wataalamu mbalimbli ambao watakuwa chachu ya kuchochea maendeleo katika nyanja mbali za maisha ya mwanadanu.hatimae ndugu ngole akaondoa dhana na fikra za kutaka kuifunga shule hiyo kwa kuwa ilikuwa na mzingira hafifu ya kujifunzia. Hata hivo wamekubaliana na mkurugenzi Wa wilaya ya ludewa ndugu Deogratias kuhakikisha shule hiyo inakuwa mfano wakuigwa. Hata hivo amemwagiza Mkuu Wa wilaya kuhakikisha watoto wote walio andikishwa kusoma shuleni hapo wote kufika bila kukosa hata mmoja kwani kidato cha kwanza amewakuta wanafunzi 19 baadala ya 250 kitu hicho kimemshangaza sana Katibu Mwenezi CCM Mkoa Wa Njombe kwa kuona utoro uliokidhiri katika shule hiyo . licha ya hilo Wazazi wengi waliokuwepo katika sherehe hiyo walifurahishwa sana na maongezi ya katibu mwenezi juu ya nia yake dhabiti ya kutaka kuifufua shule hiyo kwani walienda mbali zaidi na wamemuomba Ndugu Erasto ngole kusimamia shule hiyo kwani mchango wake umeonyesha kuikonga mioyo ya wazazi hii yote ni baada ya kutoa pesa kiasi cha tsh milion moja na laki tano(1,500,000).hata hivo kawazawadia walimu kiasi cha tsh 100,000/ kama vocha ili kuhakisha wanapata mawasiliano kila wakati ambayo yataboresha ufanisi wa kazi za uwalimu kwa kuwatafutia aina mbalimbali za stadi za kufundishia shule hiyo
katibu mwenezi wa ccm mkoa wa njombe akiwa anawasili na akipokewa kwa ukakamavu na vijana wa scourt shuleni hapo akiwa ameongozana katibu wa jumuiya ya wazazi ccm mkoa wa njombe na mwenyekiti wa jumuiya wazi willaya ya ludewa na wageni mbalimbali
pichani na aliyeshika kipaza sauti ni Ndugu NYANDA Ambaye ni katibu mkuu wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa NJOMBE naye akiwa anatoa ya kwake kwa vijana na wazazi na kuwaomba wazazi wazidi kufanya maboresho katika shule hiyo ili kufikia malengo ya kutoa elimu bora ambayo ndiyo dhumuni kuu la kunzisha shule za wazazi
katibu wa jumuiya ya wazazi mkoa w njombe ndugu NYANDA akiwa anamwelekeza katibu mwenezi wa ccm mkoa wa njombe mambo kadhaa baada ya kumaliza hotuba yake fupi siku ya mahafali
SABINUS HAULE (DIGALA) alipata nafasi naye hukusita kutoa nasaha kwa wazazi na vijana juu ya umuhimu na lengo la elimu kwa silaha pekee ya kujikwamua katika maisha
Mgeni rasmi ndugu ERASTO NGOLE akiwa anatoa vyeti kwa wahitmu wa kidato cha nne siku ya mahafali
Aliyeshika kipaza sauti (mike) ni ndugu NYANDA Akiwa anateta jambo na katibu mwenezi ccm mkoa wa njombe siku ya mahafali
Mgeni rasmi akiwa anaendelea kugawa vyeti kwa wahitimu kama pongezi kwa kufikia hatua hiyo na kuhimiza wasibweteke na hapo walipo fika lazima wakazane ili kifikia malengo yao
Katikati ni MWENYEKITI jumuiya ya wazazi wilaya ya Ludewa , Kulia kwake ERASTO NGOLE KATIBU MWENEZI MKOA WA NJOMBE kushoto kwake ni ndugu SABNUS HAULE wakiwa wana angalia miundombinu katika shule hiyo ya wazazi
PICHA ZOTE KWA NIABA NA HISANI YA
CHENGULA BLOG
BURUDIKA NA HABARI
No comments:
Post a Comment