MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Monday, 29 October 2018

WANAFUNZI 2,397 WAPATA MIKOPO AWAMU YA PILI 2018-19

Wanafunzi wapatao 2,397 wamepangiwa mikopo katika awamu ya pili ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019.

Idadi hiyo inafanya jumla ya Wanafunzi wa elimu ya juu wapatao 27,929 kati ya wanafunzi 40,000 wa mwaka wa kwanza kupangiwa mikopo hadi leo.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Abdul-Razaq Badru imesema kuwa idadi ya wanafunzi waliobaki wapatao 12,071 watapangiwa mikopo katika awamu inayofuata ili kukamilisha idadi iliyopangwa.

Orodha ya majina ya wanafunzi hao  27,929 waliokwishapangiwa mikopo inapatikana kwenye tovuti hii  na itatumwa kwenye vyuo husika kwa ajili ya hatua zaidi za kukamilisha malipo ya mikopo hiyo.

Kuona orodha ya waliopangiwa mkopo awamu ya pili 2018/2019 bonyeza hapa

Imetolewa na:

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

No comments:

Post a Comment