Mo Dewji, bilionea Mtanzania aliyetekwa na watu wasiojulikana Alhamisi wiki iliyopita, amerejea nyumbani salama.
Katika
ujumbe ulioandikwa kwenye ukurasa wa Twitter wa kampuni yake, amesema:
"Namshukuru Mwenyezi Mungu nimerudi salama nyumbani. Nawashukuru
Watanzania wenzangu na watu wote kote duniani kwa dua na sala zao.
Nashukuru mamlaka zote, ikiwemo Jeshi la Polisi, zilizofanya kazi ya
kuhakikisha narudi salama."Ujumbe huo umeandikwa saa tisa na robo alfajiri, na umeelekezwa kwamba umeandikwa kutoka Dar es Salaam.
- Gari alilotekewa Mo Dewji limesajiliwa Msumbiji
- Wasifu wa Mo Dewji, Mtanzania bilionea wa umri mdogo zaidi Afrika
- Visa 10 vya utekaji nyara vilivyoishangaza dunia
BONYEZA LINK ⇰https://twitter.com/MeTL_Group
No comments:
Post a Comment