MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Monday, 22 October 2018

Ndalichako atoa agizo kuhusu Wanafunzi 682 waliofutiwa udahili katika chuo kikuu cha UDSM

Kuna Breaking News inayotembea kwenye Whatsapp ikieleza kwamba Wanafunzi 682 wamefutiwa usajili wao kwenye Chuo Kikuu cha Dar es salaam na kwamba kama una Mtu wako alichaguliwa inabidi aangalie account yake.
Baada ya hayo, leo Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako amekutana na Waandishi wa habari na kueleza yafuatayo …….. “TCU ndiyo ambayo inaratibu zoezi la udahili wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na kilichotokea ni kwamba katika baadhi ya programu Chuo Kikuu cha DSM kilikua kimepeleka idadi ambayo ni ndogo kuliko idadi halisi ya Wanafunzi ambao wanawahitaji
Waziri Ndalichako ameendelea kwa kusema “Sasa kwa mujibu wa huo mfumo wa TCU inapokua idadi imezidi kile kiwango kilichowekwa kwenye mfumo, Wanafunzi wote wanaondolewa….. siku ya Jumamosi niliongea na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania Profesa Kihampa nikamwambia haiwezekani Wanafunzi wanaopenda Chuo Kikuu cha DSM washindwe kupata nafasi kwaajili tu ya mambo ya kikarani kwamba mtu alikosea takwimu”
Kwahiyo nikamwambia akae na Profesa Rangisi ambae ndio Mkuu wa Chuo Kikuu cha DSM, kwahiyo zile nafasi ambazo Mkuu wa Chuo anampatia ahakikishe kwamba Wanafunzi wote ambao walikua wanaondolewa warudishwe, na leo saa nane nina mkutano kwenda kuangalia utekelezaji wa maagizo yangu” – Profesa Ndalichako

No comments:

Post a Comment