MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Tuesday, 23 October 2018

NECTA YATANGAZA MATOKEO DARASA LA SABA, YATAZAME HAPA

Baraza la Mitihani NECTA limetangaza matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi (darasa la saba) ambapo matokeo yanaonyesha ongezeko la ufaulu kwa asilimia 4.96% tofauti na ufaulu wa 2017 ambao ulikuwa asilimia 72.76%
Jumla ya wanafunzi 733,103 kati ya 943,318 waliofanya mtihani huo sawa na asilimia 77.72% wamefaulu. 
idadi hiyo ya wanafunzi waliofaulu imegawanyika kama ifuatavyo, wanafunzi 382,830 walikuwa wasichana na waliobaki 350,273 walikuwa wavulana.
Dk. Charles Msonde, amesema pia kiwango cha ufaulu wa somo la Kiingereza uko chini sana tofauti na masomo mengine.
Dk Msonde amemtangaza Ndemezo Rutakwa Lubonankebe kutoka shule ya msingi Kadama ya Geita kuwa ndiye Mwanafunzi Bora kwa Mwaka huu.


Baraza la Mitihani nchini limewafutia matokeo watahiniwa 357, waliobainika kufanya udanganyifu kwenye mitihani iliyofanyika mwaka huu 2018


"Baraza limezuia kutoka matokeo ya watahiniwa zaidi 100 kutokana na kuugua kipindi cha mtihani na kuwapa fursa ya kufanya mtihani huo mwaka 2019".


Kuona matokeo hayo | Fungua link zifuatazo


http://41.59.85.99/psle/psle.htm

https://www.necta.go.tz/results/2018/psle/psle.htm

No comments:

Post a Comment