MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Tuesday, 13 November 2018

Swali la Kwanza La Dr Tizeba Bungeni Baada ya Rais Magufuli Kumtumbua

Wabunge wamemshangilia kwa makofi kwa muda wa takriban dakika moja Waziri wa zamani wa Kilimo, Dk Charles Tizeba ikiwa ni mara ya kwanza kuingia bungeni na kuuliza swali la nyongeza tangu uteuzi wake utenguliwe na Rais John Magufuli Jumamosi iliyopita  Novemba 10, 2018.

Makofi hayo yalipigwa na wabunge wa pande zote za upinzani na CCM yaliyokwenda sambamba na vigelegele hali iliyomfanya Dk Tizeba kusimama kabla ya kusubiri hadi wamalize ili kuanza kuzungumza.

Hayo yamejiri leo Jumanne Novemba 13, 2018 wakati Dk Tizeba ambaye ni mbunge wa Buchosa alipopewa fursa ya kuuliza swali la nyongeza.

Dk Tizeba ameanza kwa kushukuru Rais Magufuli kwa kumpa fursa ya kulitumikia Taifa na pia kumshukuru Spika Job Ndugai na  Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kwa ushirikiano walioutoa kwake katika kipindi chote cha uwaziri.

Katika swali lake la nyongeza, Dk Tizeba amesema katika jimbo lake kuna visiwa 28, lakini kuna vivuko viwili  kimoja kikiwa kimepitwa na wakati na hivyo wakati mwingine kuwafanya watu kuwa na hofu kutokana na kujaa.

Amehoji ni lini Serikali itapeleka vivuko vingine kutatua tatizo hilo.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Atashasta Nditiye amesema kuna timu imekwenda kutembelea katika eneo hilo ili kuangalia namna ya kuboresha ambayo ilikuta watu wakipigana hadi ngumi kutokana na hali ya usafiri ilivyo.

Amesema wataendelea kuboresha usafiri wa majini Tanzania

No comments:

Post a Comment