MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Tuesday, 4 December 2018

DC LUDEWA NDUGU TSERE AING'ARISHA LUDEWA KWA KUONGEZA KIWANGO CHA UFAULU KATIKA SEKTA YA ELIMU

MKUU WA WILAYA YA LUDEWA


Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe Mh:Andrew Tsere amefanikiwa kupandisha kiwango cha Elimu katika Wilaya ya Ludewa Baada ya Kuweka Mikakati ya pamoja na wadau wa Elimu wote wa shule za msingi na Sekondari Mwanzoni mwa Mwaka 2018 Ili kuongeza kiwango cha ufaulu
Mheshimiwa Tsere alibuni mbinu hiyo Mbadala baada ya kuona  Ludewa ipo nyuma ki elimu /katika Ufaulu kwa Miaka mingi kwani katika Mkoa wa Njombe ilikuwa inashika nafasi ya mwisho kwa mda mrefu mfululizo, Ndipo Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mh:Andrew Tsere alipoamua kujiwekea mikakati hiyo ya kuwakutanisha pamoja wadau wote wa elimu katika Wilaya hiyo Wakiwemo Maafisa elimu wote, Waratibu elimu kata wote, Walimu wakuu na, wakuu wa shule wote, Watendaji kata wote, Watendaji na wenyeviti wa serikali za vijiji wote, Pamoja na Waheshimiwa madiwani wote, mnamo Tarehe 24,February 2018  Mikakati iliyowekwa katika Mkutano huo wa wa dau ni pamoja na:
Kuhakikisha Shule zote za Msingi na Sekondari zinatoa Chakula cha mchana, Walimu wafundishe kwa bidii zote na atakaye zembea kuwajibishwa,
Walimu Wakuu na Wakuu wa Shule kusimamia nidhamu ya wanafunzi
  Lakini Pia Mheshimiwa Tsere alitoa agizo la kuwepo kwa Kambi za Taaluma kwa Kila Kata Mwezi wa Juni wakati wa likizo kwa wanafunzi wa madarasa ya Mitihani Ikiwemo Darasa la Saba,Kidato cha nne na,Kidato cha pili,
Aidha Mheshimiwa Tsere aliwataka kila mdau wa Elimu kufuatilia kwa ukaribu juu ya maendeleo ya elimu kadri ya nafasi yake inavyo mruhusu Chini ya usimamizi wa Mkuu wa Wilaya mwenyewe,
Ambapo Mikakati hiyo imefanikiwa kwa asilimia kubwa kuongeza kiwango cha ufaulu Ludewa Na hatimaye matokeo ya Mtihani wa  Darasa la Saba 2018 Mock  Mkoa Wilaya ya Ludewa ilishika nafasi ya 2 kati ya 6 na, Mtihani Taifa Wilaya ya Ludewa  ilishika nafasi ya3 Ki Mkoa  Na kushika nafasi ya 94 Kitaifa, Huku Ikiwa Ludewa Imepiga hatua zaidi ukilinganisha na mihula michache iliyopita, Ikiwa ni pamoja na shule za sekondari ambapo matokeo yake ya Kidato cha nne yakiwa bado hayajatoka Lakini kwenye mitihani ya Mock matokeo yalikuwa ni yakuridhisha,
  Mwishoni mwa Mwezi November 2018 Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa anekuwa akiendelea na ziara zake za kutembelea Kata na Vijiji pamoja na kukagua maendeleo ya Taaluma mashuleni Ameendelea kutoa maagizo kwa Walimu na wakuu wa shule  zote kuhakikisha wanaongeza bidii ya kuboresha taaluma mashuleni Mheshimiwa Tsere alitoa maagizo hayo alipo tembelea Kutoa maagizo kwa Wakuu na Walimu wakuu wa Shule ya Sekondari Ikovo Iliyopo kata ya Ludende na Shule za Msingi Ludende, Madindo na Maholong'wa katika kata ya Ludende Mheshimiwa Tsere alitoa maelekezo kuwa Walimu Wakuu na wakuu wa shule watakaoendelea kufanya vibaya watafutiwa ukuu wao wa Shule Tsere aliongeza kuwa wajitahidi kuhakikisha kuwa chakula shuleni wanafunzi wanapata cha kutosha hii ni kwa Wilaya yote ya Ludewa Tsere aliongeza kuwa hataki kufanya mchezo katika swala hilo la elimu,
  Athanasi Kibena ni Mratibu elimu kata ya Ludende katika Wilaya ya Ludewa ameshukuru sana uwepo wa DC Tsere Wilaya ya Ludewa hasa katika suala la elimu Bwana Kibena ameongeza kuwa amewaona wakuu wa Wilaya wengi waliokuwa wakifanya kazi Ludewa na walikuwa wachapakazi wazuri Lakini kwa Mkuu wa Wilaya Andrew Tsere  hakika ni wa aina yake amekuwa Mkuu wa Wilaya ambaye ni Mwalimu wa Wilaya nzima anayefundisha wa kuu wa idara ki uweledi zaidi hasa kwenye mikakati ya elimu Kibena hakusita kusema Bila Juhudi za Andrew Tsere ufaulu huu tulioupata mwaka huu 2018 ingekuwa ni Ndoto,
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ambaye pia ni Diwani wa kata ya Ibumi Mheshimiwa Edward Lezile Haule amesema anajivunia sana kuwa na Mkuu wa Wilaya mwenye uchungu na Maendeleo ya Ludewa katika Idara zote Afya, Miundombinu Elimu na n'k Mheshimiwa Edward Haule ameongeza kuwa Mheshimiwa Tsere amekuwa chachu nzuri sana kwa Ludewa na kama ni amri yake hakika angemwomba Mheshimiwa Rais asimhamishe kamwe Ludewa,
   Katika Hatua nyingine
   Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe Mh:Jassel Mwamwala alipokuwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo Inayotekelezwa kwa mjibu wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM katika Wilaya ya Ludewa Tarehe 28na 29 Novemba2018
  Amesifu na kufurahishwa na Uchapakazi mzuri wa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Andrew Tsere Mheshimiwa Mwamwala amempongeza sana Mheshimiwa Tsere kwa kuanzisha mikakati imara ya kuboresha Elimu Wilaya ya Ludewa katika Mkoa wa Njombe
  

No comments:

Post a Comment