SEHEMU YA 9
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA ?baba ,Chris anakaa hapa? Nikasema ?una uhakika Wayne? Baba mkwe akauliza ?Nina ukakika baba? Nikajibu.Baba mkwe akashuka na kumfuata Emmy ambaye alikuwa ameuinamia usukani akilia ?Hebu tuambie hapa ndipo nyumbani kwa Chris? Baba mkwe akauliza kwa ukali ?Ndiyo .Ni hapa? Akajibu huku akijifuta machozi. ?haya wapigie simu ndani watufungulie mlango? Sekunde chache geti likafunguliwa tukaingiza magari ndani.Baada tu ya kushuka ndani ya Gari Baraka akaja na kuung?angania mkono wangu.hakutaka kuniachia.Emmy akatuongoza na kuelekea sebuleni.Mara tu tulipoingia sebuleni nilipatwa na kitu ambacho siwezi kukielezea kama ni hasira au ni nini baada ya kumuona aliyekuwa rafiki yangu mkubwa Chris akiwa amekaa sofani akiangalia luninga huku mezani kukiwa na chupa kubwa ya mvinyo. Mapigo ya moyo yalibadilika na kuanza kwenda kwa kasi ya ajabu.Nikahisi jasho likilowanisha shati langu jepesi.Kichwa kiliwaka moto kwa hasira.Chris aliponiona nimesimama alipatwa na mstuko mkubwa akainuka na kusimama huku akiwa na wasi wasi mwingi.Niliushuhudia uso wake ukivuja jasho jingi. ?Hallow?W..way.ne..? Akasema kwa sauti yenye kutetemeka.
ENDELEA??????????.
?Karibu?.Kar?karibuni?? Akatamka Chris huku akionekana kuogopa kwa namna nilivyomuangalia.Skumjibu kitu nikaendelea kumtazama.Sikutazamia kama ningepatwa na hasira za namna ile baada ya kumuona mtu ambaye awali alikuwa ni rafiki yangu mkubwa .Beka alitambua kwa haraka jinsi nilivyopandwa na hasira akanishika mkono na kuniketisha sofani. Hakuna mtu aliyeitikia salamu ya Chris.Wote tukaingia sebuleni na kukaa kimya kimya.Emmy alikuwa ameinama hakutaka kututazama usoni. ?jamani karibuni sana..Chris akasema huku akiwa bado amesimama na mwenye wasi wasi mwingi. ?Mnatumia vinywaji gani? Chris akasema huku akiliendea friji ?Kijana hebu tulia na ukae chini.Hatujaja hapa kutumia vinywaji?
Baba mkwe akasema kwa ukali.Chris akaenda kuketi sofani karibu na Emmy halafu akazima kabisa luninga ile iliyokuwa mle sebuleni kukawa kimya.Baraka akaja na kusimama pembeni yangu.nadhani kuna kitu alikuwa amekihisi.Hakutaka kukaa mbali nami.Akanishika mkono kwa nguvu. ?Habari za siku nyingi wayne? Chris akasema baada ya kuona sebule iko kimya huku akijilazimisha kutabasamu.Sikumjibu kitu bali nikaendelea kumtazama.Baba mkwe akakohoa kidogo halafu akasema ?Kijana ,wewe ndiye Chris? Baba mkwe akauliza ?Ndiye mimi mzee? Chris akajibu ?Vizuri. Nadhani kabla hatujaendelea ningetoa utambulisho mfupi.Mimi ni baba yake mzazi Emmy.Yule pale ni mama yake mzazi Emmy.Yule mzee pale ni Mzee wa kanisa na mwalimu wa dini wa Emmy na Wayne.Yule pale anaitwa ndugu?nani jina lako ndugu? baba mkwe akamuuliza Beka. ?naitwa beka? ?Exactly.Anaitwa ndugu Beka ni rafiki wa Emmy na Wayne .Wale pale nadhani unawajua ni wasimamizi wa ndoa ya Wayne na Emmy.Wa mwisho sina haja ya kumtambulisha kwa sababu unamfahamu fika kwa sababu ni rafiki.. I mean alikuwa rafiki yako.Kwa kukumbusha jina lake anaitwa Wayne ni mume wa ndoa wa Emmy ? Baba mkwe akanyamaza kidogo halafu akaendelea. ?Chris nadhani mpaka hivi sasa umekwisha elewa ni kwa nini tuko hapa.Sina haja ya kutoa maelezo marefu sana kwa sababu hivi unavyotuona tumetoka katika kikao kizito na mambo mengi tayari tumekwisha yaongea huko.kwa ufupi ni kwamba tulipigiwa simu na wayne akatuomba tuonane jioni.Jioni ya leo kama alivyokuwa ametuomba tumeitika wito tukakusanyika bila kufahamu ni jambo gani alilokuwa akituitia.Baadae alitueleza jambo alilotuitia ,jambo ambalo kwa mtu mwenye moyo mwepesi unaweza ukaanguka na kufariki mara tu ukihadithiwa.Ni jambo lenye kuumiza na kusikitisha sana.Kwa mujibu wa maelezo ya wayne ni kwamba wewe na mkewe Emmy mna mahusiano ya kimapenzi.Wewe uliwahi kuwa rafiki mkubwa wa wayne na hata kulipotokea matatizo kati ya wayne na Emmy mara ya kwanza ni wewe ndiye uliyekuwa mstari wa mbele katika kutafuta suluhu.Baada ya Emmy na wayne kuelewana ni wewe ndiye uliyekuwa kiongozi wa jopo lililofanikisha sherehe za harusi yao.Sielewi ni shetani gani alikuingia hadi ukaamua kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa rafiki yako.si tu rafiki yako bali rafiki yako mkubwa na wa karibu.Hilo lilikuwa dogo,kubwa zaidi ikabainika kwamba katika mahusiano hayo baina yako na Emmy mlipata mtoto ambaye Wayne alijua ni wa kwake kumbe mtoto huyu ni wako wewe .Hili ni jambo baya sana na halivumiliki.Umemtendea vibaya sana rafiki yako na vile vile umemtendea vibaya sana mwanao Baraka.Nadhani akiwa mkubwa na kuufahamu ukweli kiundani atakuchukia katika maisha yake yote kwa kitendo ulichokifanya.Baada ya kuligundua hilo Wayne alimtaka Emmy wakafanye kipimo cha DNA ili kubaini kama ni kweli Baraka ni mwanae au si mwanae.kwa ujeuri kabisa Emmy alikataa kata kata.Wayne alifunga safari hadi dar es salaam na kufanya kipimo hicho ambapo ilidhihirika kwamba ni kweli Baraka hakuwa mwanae wa damu.Hebu pata picha ni maumivu kiasi gani aliyoyapata mwenzio baada ya kugundua kwamba mtoto aliyemlea na kumpenda na kumthamini kuliko kitu chochote kumbe si mwanae wa damu.Namshukuru sana wayne kwa sababu ni kijana mwenye roho ya ujasiri sana ambaye siku zote anaongozwa na mwenyezi Mungu kutokufanya maamuzi mabaya.Kama si kwa maongozi ya mwenyezi Mungu hivi sasa tungekuwa tukiongea mambo mengine kabisa.Lakini kama hiyo haitoshi bado Emmy aliamua kuondoka nyumbani na kuja kuishi kwako kwa kiburi bila ruhusa ya mumewe.Linaumiza sana jambo hili.Wayne alivumilia mwishowe akaona hataweza kuvumilia suala hili zaidi ya hapa lilipofikia hivyo akatuita na kuamua kuliweka wazi suala hili ikiwa ni pamoja na maamuzi yake.Katika kikao tulichokaa,mbele ya wazazi wake,mume wake,mzee wa kanisa pamoja na mashahidi wao wa
ndoa emmy alitamka kwa ulimi wake kwamba hataki tena kuishi na Wayne na kwamba wewe Chris ndiye mwanaume wa maisha yake.Anataka aishi na wewe ili mumlee mtoto wenu Baraka.Kama mzazi nilipaswa kuhakikisha kwamba watoto hawa wanamaliza tofauti zao na kuendelea kuishi kwa amani na kujenga familia iliyo bora.Sikuweza kulifanya hilo kwa sababu Emmy kwa kiburi kabisa alisema kwamba hana haja na masuluhisho ya namna yoyote ile.yeye anachohitaji ni kupewa nafasi ya kuishi na wewe.Niliyatazama macho yake na nikabaini kwamba hakuwa hata na chembe ya mapenzi kwa Wayne tena kwa hiyo hata kama tungewasuluhisha ingekuwa ni kumuongezea matatizo wayne.? Baba mkwe akanyamaza kidogo akatutazama wote halafu akasema ?bwana Chris,nimekuja hapa mimi kama baba wa Emmy nikiwa na mama yake Emmy na mashahidi wao Nataka mbele yao utamke wazi kwamba ni kweli Baraka ni mtoto ambaye umezaa na emmy halafu masuala mengine yafuate.? Baba mkwe akasema huku amemkazia macho Chris. ambaye alikuwa ameinama asijue afanye nini.Jasho lilikuwa likimtiririka.Nilikumbuka jinsi urafiki wetu ulivyokuwa mkubwa na wala sikutegemea kama ingetokea siku angenifanyia kitu kama hiki.Ni wazi ulimi ulikuwa mzito kutamka lolote. ?Chris tunakusubiri wewe.hebu ongea haraka bado tuna mambo mengi ya kuongea? Usoni kwa Chris kulikuwa na michirizi ya machozi ambayo sikujua kama alikuwa akilia kwa kulijutia kosa lake au yalikuwa ni machozi ya uongo. ?baba..na mama naombeni mnisamehe..Nimek?..? Alisema Chris lakini kabla hajaendelea mbele zaidi baba mkwe akadakia ?Chris usipoteze wakati wetu.Ninachotaka kusikia ni kauli yako kwamba ni kweli umezaa na Emmy.Just short and clear? baba mkwe akasema kwa ukali ?baba ni kweli,nimezaa na Emmy? Chris akasema huku akitazama chini kwa aibu. Kwa fundo nililokuwa nalo moyoni nilitamani niichukue chupa ile ya mvinyo iliyokuwa mezani nimtwange nayo kichwani.Nilianza kujilaumu kwa kuamua kuja huku kwa sababu kuja kwangu huku kumeyaamsha upya mateso na maumivu yote aliyonisababishia Emmy.Awali nilijipa moyo kwamba maumivu yale ni ya kupita na tayari nimekwisha yazoea lakini kumbe nilikuwa najidanganya.maumivu yale hayakuwa yakizoeleka wala kuvumilika. ?Nadhani nyote mmmesikia kwa kauli yake kwamba ni kweli amezaa na emmy mtoto ambaye ni huyu Baraka.? Baba mkwe akasema halafu akanyamaza na kumkazia macho Emmy halafu akamtazama Baraka aliyekuwa amesimama pembeni yangu amenishika mkono.Hakutaka kuuachia mkono wangu. ?Chris ,baada ya kukiri wewe mwenyewe kwa ulimi wako kwamba Baraka ni mwanao ,kitu cha kwanza tunachokifanya hapa usiku huu ni kukukabidhi mtoto wako baraka ili umtunze na kumlea kama baba yake mzazi .Baadae taratibu za kisheria na kidini zitafuata ili tuone ni jinsi gani tunaweza kulibadilisha jina la mtoto ili liweze kuendana na jina la baba yake mzazi.Tungeweza kumzuia mtoto huyu abaki kwa Wayne na asikutambue wewe kama baba yake,lakini kwa kufanya hivyo tungekuwa bado hatumtendei haki mtoto mdogo kama huyu ambaye ana haki ya kumfahamu baba yake mzazi.Kwa hiyo kuanzia usiku huu utakuwa na mwanao Baraka na utamtunza na kumlea kwa jinsi unavyoona inafaa kama baba yake.Tunasikitika sana kwa sababu mateso anayoyapata mtoto huyu kwa hivi sasa ni makubwa .?baba mkwe akasema Baraka ambaye alikuwa amesimama pembeni yangu amenishika mkono kwa nguvu akawa akitokwa na machozi na kuniambia kwa sauti ndogo ?Baba mimi sitaki kubaki hapa.Tunaondoka wote? Sebule nzima ikawa kimya wote wakimtazama Baraka na kumuonea huruma malaika yule anayeteseka bila sababu.Iliniuma sana kumpoteza mtoto kama yule niliyekuwa nikimpenda kupita maelezo.Sikuwa na jinsi zaidi ya kumuachia aende kwa baba yake mzazi.Nilihisi kama vile nilikuwa naadhibiwa kwa kosa ambalo silijui kwa maumivu yaliyokuwa ndani ya moyo.
?baraka baba njoo hapa.? Baba mkwe akamwita Baraka ?Babu mi sitaki.mi sibaki hapa nitarudi kwetu na baba? Baraka akasema huku akilia. Baba mkwe akasimama,akamshika mkono Baraka na kwenda kukaa naye sofani. ?Baraka najua bado u mtoto mdogo lakini tayari una akili ya utambuzi.Nadhani mpaka sasa hivi unamfahamu baba yako ,si ndiyo? Baba mkwe akauliza na baraka akaitika kwa kichwa ?Good boy.baba yako anaitwa nani? Baba mkwe akauliza tena huku akitabasamu ?baba yangu anaitwa wayne? baraka akajibu ?Vizuri sana . Sasa Baraka kuna kitu kimoja ambacho tunataka ukifahamu Ni kwamba Wayne si baba yako mzazi.baba yako mzazi ni yule pale anaitwa Chris.Kwa hiyo kuanzia leo wewe utaishi hapa kwa baba yako mzazi pamoja na mama yako.Umesikia Baraka? Baba mkwe akasema na kumfanya Baraka akaangue kilio.Ikanibidi nimchukue na kumbembeleza. ?Sikia baraka utabaki hapa kwa baba,mama yako pia atabaki hapa.Nitakuwa nakuja kukuangalia na kukuletea zawadi kila jumamosi.? ?baba mimi sitaki kubaki hapa? Baraka akapiga kelele ?baraka utabaki na mama yako? ?Mimi simpendi mama.nakupenda wewe baba? Baraka akasema huku akilia na kuwaacha watu wote midomo wazi. Nilishindwa kuyazuia machozi kunitoka kwa kauli ile ya Baraka.Ni wazi aliufahamu ukatili wa mama yake . ?baba ,itakuwa ngumu sana kwa baraka kubaki hapa.naombeni mniruhusu nirudi naye nikaendelee kuishi naye ili hata kama ni kumkabidhi kwa baba yake basi tumfanyie maandalizi ya kutosha ya kisaikolojia lakini si hivi tunavyotaka kufanya.Tunamuumiza mtoto bure.? Nikasema Emmy akainuka pale sofani na kuja kumchukua Baraka kwa nguvu ?Nimeshasema mtoto wangu haendi popote.Hapa ni kwa baba yake na ataishi hapa atake asitake.? Emmy akanyanyua Baraka na kuondoka naye huku mtoto akipiga kelele nyingi. Baada ya muda akarejea bila baraka.nadhani alikuwa amekwenda kumfungia chumbani. Baba mkwe akaendelea baada ya Emmy kuirejea. ? Bwana Chris baada ya zoezi la kwanza kukamilika kitu kingine kinachofuata ni kukukabidhi rasmi Emmy? Chris akastuka sana kwa kauli ile ya baba mkwe akataka kuongea jambo baba mkwe akamuonyeshea ishara anyamaze. ?kaa kimya kabisa na sitaki unijibu chochote.Huna nafasi ya kunijibu lolote.? Baba mkwe akasema kwa ukali. ?Chris naomba usistuke kwa sababu Emmy kwa mdomo wake ametamka kwamba hataki kuendelea kuishi na Wayne na anataka kuja kuishi na wewe ili mumlee mtoto wenu baraka.Tokea mwanzo ulifahamu fika kwamba Emmy ni mke wa mtu tena mke wa rafiki yako wa karibu lakini ukadiriki kuwa na uhusiano naye na hatimaye mkazaa mtoto.Nina imani ulikwisha jiandaa kwa lolote litakalotokea.Ulikuwa ufahamu nini kitatokea baada ya mambo yote haya kuwekwa bayana.Niwazi ulitegemea ndoa ya Wayne na Emmy kuvunjika na wewe kupata nafasi ya kuwa na Emmy.Imetokea kama ulivyokuwa umekusudia.Ndoa kati ya Emmy na wayne naweza sema kwamba haipo tena.Sababu kubwa ya kutokuwepo kwa ndoa hii kati ya Wayne na Emmy ni wewe.Kwa hiyo Bwana Chris nimekuja hapa mimi pamoja na hawa wote unaowaona ili nikukabidhi rasmi Emmy.Kuanzia sasa chochote kitakachomtokea Emmy kitakuwa ni jukumu lako.Mimi kama baba mzazi wa Emmy pamoja na mama yake wote kwa pamoja tumekwisha nawa mikono,hatutahusika tena na jambo lolote linalomuhusu .Kwa sasa wewe ndiye utakuwa baba na mama yake.Kitendo mlichokifanya si kitendo cha kibinadamu na hakistahili kuvumilika.Tokea sasa Emmy yuko mikononi mwako.Mlee na kumtunza jinsi unavyotaka wewe Mimi nimemaliza.? Akasema Baba mkwe na taratibu nikauona uso wa Chris ulivyokuwa umelowa jasho.Hakuwa ametegemea mambo
haya kufika hapa yalipokuwa yamefika.Nilimsikitikia sana Emmy kwa ujinga aliokuwa ameufanya kwa sababu Chris ninamfahamu fika kwamba hakuwa na lengo lolote naye.Chris tabia yake ndiyo hiyo ya kuchezea wanawake na kisha kuwatelekeza.Siwezi elezea uchungu unaonipata kila nikimuwaza mtoto Baraka.Ni wazi alikuwa katika wakati mgumu mno licha ya umri wake kuwa mdogo. ?Jamani kuna mtu ana jambo la kuongeza? Baba mkwe akauliza baada ya ukimya mkubwa kutanda mle ndani.Macho ya watu wote mle ndani yakanigeukia mimi .Wote walijua labda nilihitaji kusema machache.Nilikuwa na mengi ya kuongea lakini kila nilipojaribu kutaka kusema neno kuna kitu kilikuwa kimenikaba koo kiasi cha kushindwa kutamka neno.Fundo la hasira lilikuwa limenikaa.Niliutumia mkono wangu kuwafanyia ishara kwamba sina lolote la kuongea. ?Nadhani hakuna yeyote mwenye jambo la kuongea.Tunaweza kuondoka? Baba mkwe akaamuru.Wakati tukiinuka kwa ajili ya kuondoka Chris akasimama na kusema jambo ?Baba samahani naomba mkae kidogo .Hata mimi nina mambo ya kuongea.Mbona hamjanipa nafasi ya kuongea? Hivi mnavyonifanyia si vizuri.Haiwezekani mje mnimwagie mtu hapa ndani katika mfumo huu.Tafadhalini jamani naomba na mimi nisikilizwe japokuwa nimekosea..? Chris akasema huku akiwa ameifumbata mikono yake kifuani kwake na sauti yake ilikuwa ni yenye kukwama kwama. ?Tumekumwagia mtu? Baba mkwe akauliza kwa ukali ?Unadiriki kusema tumekumwagia mtu? Kweli kijana huna haya.Baada ya mambo yote haya uliyoyafanya bado unadiriki kusema kwamba una kitu cha kuongea? Huna nafasi wala kitu chochote cha kuongea baradhuli wewe.Ulitegemea nini baada ya kuivuruga ndoa ya rafikiyo? Ulichokuwa umekitegemea ndicho hicho umekipata.Emmy sasa ni mke wako halali.Na kwako Emmy,kwa kuwa umemkana mumeo wa ndoa mbele yetu na kutamka kwa ulimi wako kwamba hutaki kuishi naye tena,na sisi hatutaki kukuona tena nyumbani kwetu.na hatukutambua kama mwanetu.Lolote litakalokupata kuanzia sasa ,baba na mama yako ni huyu mwenzio ambaye leo hii amekuwa ni mtu wa maana sana kwako.Usitutambue kwa lolote lile.Na ninakwambia wazi wazi kwamba kitendo ulichomfanyia mwenzio na wewe kitakurudia.Utafanywa kama ulivyomfanyia mwenzio?. baba mkwe akafoka ?lakini baba?..? Chris akataka kusema jambo lakini kabla hajaendelea akazuiwa na Emmy. ?Chris usiseme chochote.kwa kuwa wamekwisha nikataa kuwa mimi si mtoto wao sasa ya nini uendelee kuwabembeleza? Achana nao Chris.Let them go.? Nilimtazama Emmy kwa hasira.Alikuwa akiongea kwa kiburi sana.Sikutegemea kama ni kweli Emmy niliyemfahamu leo hii anadiriki kutamka maneno yale kwa kiburi kikubwa na tena mbele ya wazazi wake.Baba mkwe hakutaka kuongea tena neno lolote akatuongoza tukatoka nje.Nilimuona Chris akiwa amesimama pale sebuleni akiwa haamini kilichokuwa kimetokea. ?Wayne baba, nenda nyumbani kapumzike.Tutaongea zaidi kesho.Ninachokuomba usiwaze sana kuhusu haya yaliyotokea.Hii ni mitihani ya dunia na huna budi kuishinda.Ninachokusihi jitahidi sana kuomba Mungu ili aweze kukupa nguvu ya kuweza kuyashinda majaribu haya.Muda si mrefu mambo haya yatakwisha na utasahau kabisa? baba mkwe akaniambia huku akinipiga piga mgongioni wakati tukijiandaa kuingia katika magari yetu .Sikujibu kitu nilikuwa nimeinama chini nikitafakari..Sikutegemea kama mwisho wangu na Emmy ungekuwa namna hii. TUKUTANE SEHEMU IJAYO????????.. ;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;
No comments:
Post a Comment