MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Saturday, 17 October 2020

BEYOND THE PAIN SEHEMU YA 8


 SEHEMU YA 8.

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA ?Kama tulivyoapa siku ya ndoa yetu na padri akatamka kwamba kilichofungwa duniani kimefungwa pia mbinguni kwa maana hiyo ndoa yangu mimi na Emmy haitaweza kuvunjika hadi pale kifo kitakapotutenganisha.Pamoja na yote aliyonitendea lakini bado Emmy ni mke wangu na siku zote sintalisahau hilo.Pamoja na hayo lakini yeye kwa upande wake amelisahau hilo na kutamka wazi kwamba hajisikii tena kuwa na mimi mume wake wa ndoa na kwamba anahitaji kwenda kuishi na mwanaume mwingine ili walee mtoto wao.Natamka wazi kwamba yuko huru kwenda huko atakako kwenda.siwezi kumzuia kufanya atakavyo hata kama tunafungwa na ahadi ya ndoa.Kwa hiyo Emmy mimi nakuruhusu uende huko unakotaka kwenda,ukaishi kwa amani.Inaniuma sana lakini sina namna nyingine ya kufanya.Naamini mateso haya uliyonisababishia Mungu anayaona na iko siku atanipa faraja.Kwa hiyo mama uko huru kwenda unakotaka kwenda.Una ruhusa ya kuchukua chochote ukitakacho humu ndani.Mimi ya kwangu ni hayo tu? Nikasema na kuinama.Nilihisi maumivu makali ya moyo.

ENDELEA?????????..

Wote wakakaa kimya ni baba mkwe pekee aliyethubutu kufungua kinywa chake na kusema ?Wayne tumeyasikia mawazo na maamuzi yako.Wote tulikuwa tukisubiri kusikia kauli yako ya mwisho kwa sababu wewe ndiye mwenye mke na sisi ni washauri tu.Wayne najua ni maumivu kiasi gani uliyoyapata kwa kitendo hiki alichokufanyia mwenzio.najua umeumia kupita kiasi japokuwa ni wewe mwenyewe unayejua ni kiasi gani umeumia.Pamoja na hayo yote Wayne napenda nipendekeze jambo moja kwamba bado kuwe na fursa ya majadiliano na kusameheana.Sisi sote ni binadamu na sote tunakosea.Baba wa mbinguni anaagiza kwamba mara zote tuishi kwa kusameheana hata pale ambapo mioyo yetu inakuwa migumu kusamehe.Sijui wenzangu mnalionaje suala hili? Baba mkwe akauliza Mwalimu wangu wa dini akasema kwa haraka ?Mzee hata mimi nakuuunga mkono kwa hilo.Japokuwa masuala haya bado ni magumu na yanaumiza moyo lakini bado tunapaswa kusameheana kwa kila jambo.Hata mimi napendekeza hivyo kwamba tupate fursa ya kulijadili suala hili kwa undani na kusameheana ili maisha yaendelee na mtoto asiweze kuathiriwa na haya yaliyotokea kwani yeye ndiye atakayekuwa muathirika mkubwa? Mawazo yao yalikuwa mazuri lakini moyoni sikuwa hata na hamu ya kumuona tena Emmy.Nikainua kichwa na kusema kwa haraka. ?wazee wangu mna wazo zuri lakini naomba niweke wazi kwamba mimi nilikwisha msamehe Emmy siku nyingi.Najua aliteleza kitu ambacho kila binadamu kinaweza kumtokea.Pamoja

na kufanya hayo yote aliyoyafanya , bado Emmy ndiye aliyekuwa wa kwanza kuondoka hapa nyumbani bila kufukuzwa.Kwa maana hiyo ni kwamba hata tukikesha usiku na mchana tunajadili tayari mwenzangu hana mpango wa kuwa na mimi tena.Angekuwa ni mtu mwenye busara na mwenye kulitambua kosa lake angeweza kuomba msamaha lakini mpaka leo hajafanya hivyo.Ninyi wenyewe mmekuwa mashuhuda wa majibu anayoyatoa hapa mbele yenu.Mzee tusipoteze muda yeye aende tu anakotaka kwenda.? Nikasema huku hasira tayari ikianza kunipanda.Baba mkwe akamgeukia Emmy ?Emmy umeyasikia aliyoyasema mwenzako? Baba mkwe akauliza .Emmy kwa sauti ndogo akajibu. ?baba mimi nimekwisha sema siwezi tena kuishi na Wayne.hakuna haja ya kupoteza wakati kwa usuluhishi.Yeye amekwishanipa ruhusa niende kwa hiyo hakuna kitu cha kuendelea kujadili hapa.hata mkisema nini mimi siwezi kurudiana na Wayne.? Emmy akasema kwa kiburi. Baba mkwe akatafakari kwa sekunde chache halafu akasema ?sawa Emmy tumekusikia.Tumekuelewa unataka kitu gani.nenda unakotaka kwenda lakini ukumbuke kwamba hii ni dunia.mambo uliyomfanyia mwenzio leo na wewe yatakukuta kesho.Siku zote asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na dunia.nakutakia kila la kheri huko uendako.? Baba mkwe akasema kwa hasira Baada ya kama dakika moja hivi ya ukimya baba mkwe akasema. ? Wayne vipi kuhusu mtoto Baraka.Kuna utaratibu gani kuhusu yeye? ?Baraka ana haki ya kumfahamu baba yake mzazi.Haitakuwa jambo la busara kama tutamficha ukweli mtoto.Ni jambo zuri ikiwa atafahamu mapema kwamba baba yake si mimi.Iwapo tutamficha na akaja kufahamu tayari akiwa amekuwa mkubwa sana itamuumiza mno.Mimi naona ni bora kama tutafanya utaratibu ili aweze kufahamishwa na kwa baba yake.Hata kama nikiendela kumlea lakini awe akifahamu kwamba mimi si baba yake mzazi.Bado nampenda sana Baraka.Na endapo wazazi wake watakubali wanaweza wakamuacha hapa mimi nikaendelea kumlea??? Sikumaliza sentensi yangu emmy akajibu kwa haraka ?Siwezi kumuacha mtoto wangu hapa.Ninapoondoka hapa leo ninaondoka na mwangu.Siwezi kuruhusu mwanangu aje kulelewa na mwanamke mwingine.Mwanangu nitamlea mimi mwenyewe.? Emmy alisema kwa ukali halafu akainuka na kuelekea chumbani kwa baraka.Kila mmoja alikuwa akishangaa ?Wayne hivi huyu mwenzio amepatwa na matatizo gani? Kwa sababu naona si yule Emmy niliyemlea mimi.Amebadilika ghafla? Baba mke akauliza ?baba hata mimi mwenyewe ninashangaa kwa mabadiliko haya .? Wakati tukiendelea kujadiliana kule sebuleni nikasikia Baraka akipiga kele chumbani kwake.Nikainuka na kuelekea chumbani kwa Baraka Emmy alikuwa akipakia nguo na vitu vya Baraka katika begi huku Baraka akilia kwa nguvu. ?Baraka kuna nini ? Nikauliza baada ya kumkuta Baraka akigalagala chini. Aliponiona akakimbia na kunikumbatia. ?Daddy ,mama anasema eti leo tunahama mimi na yeye tunakuacha peke yako.Halafu anasema eti anataka kunipeleka kwa baba yangu? Nilimuonea huruma malaika yule asiye na kosa. Nikambembeleza akanyamaza kulia halafu nikamwambia. ?Baraka ni kweli mama yako anakupeleka ukamfahamu baba yako mzazi.Hatukukutaarifu toka mapema kwamba mimi si baba yako mzazi.Kwa hiyo B??.? kabla sijamalizia sentensi yangu baraka akachoropoka na kukimbia akajifungia bafuni akilia. Nikamfuata na kukuta tayari amekwisha ufunga mlango kwa ndani.Alikuwa akilia kwa nguvu ?Baraka fungua mlango..Nikasema. ?Sifungui mlango hadi uniambie wewe ndiye baba yangu.?

Nikakosa jibu la kumpa.Roho ikaniuma sana kwa malaika yule kuteseka bila kosa. ?Fungua mlango Baraka? Nikasema tena . ?daddy sifungui mlango hadi uniambie wewe ndiye baba yangu.Mimi simtaki baba mwingine zaidi yako???.? Nilichomwa na maneno yale ya Baraka nikasimama na kuuma meno kwa hasira ?Kwa nini Emmy unafanya hivi? Nikajisemea moyoni. .Kwa jinsi nilivyokuwa ninampenda mtoto yule sikutazamia kama itakuja tokea siku ambayo ataumia kama hivi.Nilisimama pale mlangoni nikiwa na hasira huku Baraka akiendelea kulia mle ndani bafuni. ?Baraka fungua mlango ,nataka kuongea na wewe.Fungua mlango mwanangu? Nikaendelea kumbembeleza Baraka afungue mlango.Bado aliendelea kulia. ?Baraka mwanangu nyamaza kulia na ufungue mlango.? Nikasema tena ?baba sifungui hadi uniambie kwamba hautanipeleka huko mama anakotaka kunipeleka.Simtaki baba mwingine.wewe ndiye baba yangu? Baraka akasema. Wakati nikiendelea kumbembeleza baraka afungue mlango wa bafuni baba mkwe akatokea. ?Wayne nini kinaendelea huku? Akauliza baba mkwe. ?Mzee,Baraka amekimbia na kujifungia huku bafuni.Hataki kwenda sehemu yoyote ile.Nimejaribu kumbembeleza afungue mlango lakini amekataa hadi nitakapomuhakikishia kwamba mimi ni baba yake? baba mkwe akainama na kufikiri kwa sekunde kadhaa halafu akasema ?Emmy amesababisha mambo makubwa mno.Sikutegemea kama itakuja tokea siku Emmy atakuja fanya mambo kama haya.? Baba mkwe akanong?ona. Kwa muda wa kama dakika moja tulikuwa tumesimama pale mlangoni huku Baraka akiendelea kulia mle bafuni. ?Kwa hiyo umeamua nini Wayne? Baba mkwe akauliza. ?Ni kama tulivyoamua pale sebuleni.Emmy ataondoka na Baraka na kwenda kumkabidhi mtoto kwa baba yake mzazi,halafu taratibu nyingine za kisheria na kikanisa zitafuata baadae.lakini kwanza baraka amfahamu baba yake?Nikasema ?Sawa Wayne mimi siwezi kupingana na uamuzi wako japokuwa Emmy ni mwanangu lakini kwa dharau aliyoionyesha leo kwetu sisi wazazi wake na kwako wewe mume wake wa ndoa sina budi kukubali uamuzi wako huo kwamba aende anakotaka kwenda lakini ni dunia ndiyo itakayomfundisha.Mpaka umefikia uamuzi huu nina imani atakuwa amekufanyia mambo mengi ambayo huwezi kuyaweka wazi.lakini pamoja na hayo nina wazo moja.? ?wazo gani baba?Nikauliza ?Nataka nimpeleke Emmy huko anakotaka kwenda.Nataka nikamkabidhi kwa huyo mume wake mpya ambaye yeye ametamka mbele yetu kwamba ndiye anayemfaa kuishi naye.Kwa sababu yeye ameamua kuachana na kiapo chake cha ndoa alichoapa mbele ya mwenyezi Mungu,nitampeleka kwa huyo mwanaume ambaye yeye anamuona ni wa muhimu kwake .Inaniuma sana kufanya hivyo kama mzazi ambaye nilipaswa kuhakikisha mambo haya yanakwisha na mnakuwa pamoja tena lakini hata kama tukijaribu kuyaweka sawa mambo haya ili muishi pamoja Emmy atakuumiza sana na anaweza hata kukutoa uhai wako.Wayne acha tu niende nikamkabidhi huko halafu nitanawa mikono.Huyo Chris ndiye atakayekuwa ni baba na mama yake.? Baba mkwe akasema Nikakaa kimya kwa muda halafu nikasema ?Baba tutakwenda sote? ?Hapana Wayne nadhani ingekuwa vizuri kama ungebaki hapa halafu mimi na huyu mzee wa kanisa tutampeleka Emmy huko anakotaka kwenda.? ?Nalijua hilo baba.Lakini ninaomba niongozane na ninyi .Hakuna chochite kitakachoharibika.Chris alikuwa rafiki yangu mkubwa sana.Sintamweleza chochote isipokuwa nataka aione sura yangu ili aendelee kuikumbuka katika maisha yake yote.?

?sawa wayne kama umesisitiza basi hakuna shida.Sasa tunafanyaje kuhusu huyu mtoto aliyejifungia humu bafuni? Muda unazidi kusonga.?Baba mkwe akauliza ?Nimekumbuka kuna ufunguo wa akiba.Ngoja nikauchukue ? Kwa haraka nikaelekea chumbani nikauchukua ufunguo wa akiba .Emmy bado alikuwa akikusanya nguo pamoja na vitu vyake vidogo vidogo.Sikusumbuka kumsemesha nikatoka chumbani na kurudi kule bafuni alikokuwa amejifungia Baraka.Nikachomeka ufunguo na kuufungua mlango.Baraka alikuwa amejikunyata katika pembe ya bafu akilia.Nilimuonea huruma sana mtoto yule lakini sikuwa na namna nyingine ya kufanya. Nilimfuata pale chini alipokuwa amekaa nikapiga magoti na kumfuta machozi. ?baba naomba usinipeleke huko mahala mama anakotaka kunipeleka.? Baraka akasema ?Nyamaza kwanza kulia baraka? Nikambembeleza ?Baba mimi sitaki kuwa na baba mwingine.wewe ndiye baba yangu? Baraka akasisitiza ?Nalijua hilo Baraka ,lakini huko mama yako anakotaka muende ni muhimu sana.Ila usijali tutakwenda wote.Mimi pia ninakwenda.? ?na wewe unakwenda baba? Akauliza Baraka ?Ndiyo Baraka.hata mimi ninakwenda huko.Inuka basi twende ukajiandae? Baraka akakubali ,akainuka nikamshika mkono na kumuongoza kwenda chumbani kwake.Nguo zake pamoja na vitu vyake vilikuwa tayari vimepakiwa katika masanduku .Niliumia sana moyoni .Sikutegemea kama ingetokea siku ningeachana na mtoto huyu niliyempenda kupita kitu chochote.Machozi yalikuwa yakinilenga lakini nikajikaza ili baraka asigundue chochote.Alipokuwa tayari nikamfuata mama yake kule chumbani. ?baraka yuko tayari.Vipi uko tayari? Nikamuuliza Emmy lakini hakunijibu kitu. ?kama kuna vitu vitabaki kesho nitamtuma dereva akuletee kila kitu unachohitaji? Nikasema ?Sihitaji kitu chochote toka kwako Wayne.Nilichokuwa nikihitaji nimeshakipata.Nilikuwa nahitaji kuondoka tu hapa ndani.na tafadhali wayne nakuomba nikitoa mguu ndani ya nyumba hii usiendelee kunifuata wala kunipigia simu.Forget if I exist.Na wala usimfuate fuate Chris.hana kosa lolote mimi ndiye niliyemchagua? Emmy akasema huku amenikazia macho.Sikutaka kuendelea kubisha naye.Nikainua mabegi yake mawili nikaanza kuyatoa nje na kuyafungia katika gari lake.Mama yake aliyekuwa amekaa ndani ya gari baada ya kutolewa mle sebuleni kutokana na hali yake kuanza kubadilika alianza kulia aliponiona nikitoka na mabegi na kuyapakia katika gari la Emmy.nadhani alifahamu fika kwamba mambo yalikwisha haribika. ?wayne baba usijali Mungu atakulipia.Mambo aliyokufanyia huyu mwenzio ni mambo mabaya sana? Akasema mama mkwe. ?usijali mama hii ndiyo dunia na hii ni mitihani ambayo hatuna budi kuishinda.Nitakuwa salama mama usijali? Nikasema huku nikipiga hatua kurudi tena ndani.Nilijitahidi kutokuonesha hali yoyote ya huzuni japokuwa nilikuwa na maumivu makubwa ndani ya moyo.Nikachukua mabegi ya Baraka na kuyapakia pia ndani ya gari ya Emmy. ?baba naona kila kitu kiko tayari.nadhani tunaweza kuondoka sasa? Nikamwambia baba mkwe. ?Emmy tunakwenda wote hadi kwa huyo mume wako mpya.Tunataka tukakukabidhi huko? baba mkwe akamwambia Emmy aliyekuwa amesimama mlangoni akiwa na Baraka. ?baba mimi nakwenda peke yangu.Sitaki mtu yeyote anifuate? Emmy akasema na kumfanya baba mkwe akunje uso kwa hasira ?Emmy nakuonya kwa mara ya mwisho kwamba sintaendelea kuvumilia dharau zako kwetu.Umetudhalilisha kiasi ambacho wewe huwezi jua,lakini kama haitoshi bado unaendelea kutudharau.Nakwambia sintavumilia zaidi dharau zako.Kuanzia sasa nataka unisikilize mimi kama baba yako.Nakuonya usiendelee kunijaribu tena?? baba mkwe akasema kwa hasira huku akitoa kitambaa na kujifuta jasho. ?wayne kama hakuna tunachokisubiri tena ,funga nyumba twendeni ? baba mkwe

akaamuru.tayari alikuwa amekasirika .Nilimsifu sana baba huyu kwa ustahimilivu wake mkubwa kwa dharau za mtoto wake wa kumzaa.Dharau za Emmy hazikuwa zikimithirika.Sikujua sababu ya mabadiliko yale ya tabia ya Emmy. Nilifunga milango ya nyumba yangu huku roho ikiniuma kila nikimfikira baraka.Mimi na Beka pamoja na wale wasimamizi wetu wa ndoa tukaingia katika gari la Beka,halafu mzee wa kanisa akapanda gari moja na baba na mma mkwe ,Emmy akapanda gari lake akiwa na Baraka.Safari ikaanza ya kuelekea Njiro mahala anakoishi Chris. Usiku huu hakukuwa na msongamano mkuwa wa magari katika barabara iendayo Njiro.Kwa wakazi wa Arusha wanaufahamu msongamano mkubwa wa magari uliopo siku hizi katika barabara za jiji hili linalokua kwa kasi. Haikutuchukua muda mrefu sana toka maeneo ya Majengo ninakoishi mimi hadi maeneo ya Njiro. Safari yetu ilikuwa ni ya kimya kimya.Kila mtu alikuwa akiwaza lake.Tulikuwa tukilifuata gari la Emmy ambaye ndiye aliyekuwa akituongoza njia.Hatimaye gari ya Emmy ikasimama nje nyumba moja yenye geti kubwa jeusi.Akafungua mlango na kushuka garini.Baba mkwe naye akashuka garini.Kuona hivyo na sisi ikatubidi tushuke. ?nadhani ni hapa? baba mkwe akasema.Nilipatazama mahala pale nikapatambua kwamba pale hapakuwa kwa Chris. ?Mzee hapa si nyumbani kwa Chris.Ninapafahamu nyumbani kwake.Emmy anataka kutuchezea mchezo? Nikasema.Ni wazi pale hapakuwa nyumbani kwa Chris.Haraka haraka baba mkwe akamwita Emmy ambaye alikuwa getini akisubiri geti lifunguliwe. ?Emmy nilikuonya toka mwanzo kwamba sintavumiia tena dharau na michezo yako ya kijinga.Hebu niambie hapa ndipo nyumbani kwa Chris? Babamkwe akauliza.Emmy hakujibu kitu akabaki kimya.Tukiwa hatuna hili wala lile tulitahamaki baba mkwe akimchapa Emmy kofi kali la shavuni linalompeleka Emmy chini.Alitaka kumfuata tena pale pale chini ili aendelee kumuadhibu lakini kwa jitihada zangu na Beka tukafanikiwa kumtuliza. ?Haya ingia garini sasa hivi tunaelekea kwa Chris.Wayne ongoza njia kwenda kwa huyo mshenzi mwingine? baba mkwe akatamka kwa hasira.Emmy akasimama huku akilia akaingia garini na kuligeuza gari lake.Mimi nikatangulia mbele halafu gari la Emmy likafuatia na mwisho lilikuwa ni gari la baba mkwe.Dakika chache baadae tukawasili katika nyumba ya Chris.Gari zikasimama nikashuka na kumfuata baba mkwe. ?baba ,Chris anakaa hapa? Nikasema ?una uhakika Wayne? Baba mkwe akauliza ?Nina ukakika baba? Nikajibu.Baba mkwe akashuka na kumfuata Emmy ambaye alikuwa ameuinamia usukani akilia ?Hebu tuambie hapa ndipo nyumbani kwa Chris? Baba mkwe akauliza kwa ukali ?Ndiyo .Ni hapa? Akajibu huku akijifuta machozi. ?haya wapigie simu ndani watufungulie mlango? Sekunde chache geti likafunguliwa tukaingiza magari ndani.Baada tu ya kushuka ndani ya Gari Baraka akaja na kuung?angania mkono wangu.hakutaka kuniachia.Emmy akatuongoza na kuelekea sebuleni.Mara tu tulipoingia sebuleni nilipatwa na kitu ambacho siwezi kukielezea kama ni hasira au ni nini baada ya kumuona aliyekuwa rafiki yangu mkubwa Chris akiwa amekaa sofani akiangalia luninga huku mezani kukiwa na chupa kubwa ya mvinyo. Mapigo ya moyo yalibadilika na kuanza kwenda kwa kasi ya ajabu.Nikahisi jasho likilowanisha shati langu jepesi.Kichwa kiliwaka moto kwa hasira.Chris aliponiona nimesimama alipatwa na mstuko mkubwa akainuka na kusimama huku akiwa na wasi wasi mwingi.Niliushuhudia uso wake ukivuja jasho jingi. ?Hallow?W..way.ne..? Akasema kwa sauti yenye kutetemeka.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO?????????

No comments:

Post a Comment