MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Wednesday, 14 October 2020

BEYOND THE PAIN SEHEMU (7)

 


SEHEMU YA 7

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA Baadae nikagundua kuwa kulikuwa na message za kimapenzi walizokuwa wakitumiana.Nikabaini kuwa Emmy ana uhusiano na mtu huyu wa kimapenzi kwa sababu kwa mujibu wa meseji wanazotumiana walikuwa wakikumbushana juu ya siku za nyuma wanazokutana katika mahoteli makubwa na kufanya mapenzi.Si mara moja Emmy huwa ananiaga kuwa anakwenda semina au katika makomngamano au kikazi nje ya mji kumbe huwa anautumia muda huo kukutana na huyo mtu wake muhimu.Ushahidi wa meseji zote hizo ninao toka walipoanza kuwasiliana.? Mama mkwe akainama chini kwa aibu .Baba mkwe yeye akatoa kitambaa na kufuta jasho lililoanza kumtoka.Kila mmoja mle sebuleni sura yake ikabadilika.Sikutaka kumung?unya maneno,nikaendelea. ?Niliumia sana baada ya kuligundua hilo lakini nashindwa hata kuelezea maumivu niliyoyapata baada ya kugundua kuwa ???.? Kabla sijaendelea mbele mlango ukagongwa.Nikaomba samahani na kwenda kuangalia ni nani aliyekuwa akigonga.Alikuwa ni jirani yetu mama Mwantumu.Mama yule akaniambia kuwa Emmy alikuwa akihitaji kuonana na mimi nje ya nyumba.Amegoma kuinia ndani baada ya kuliona gari la baba yake liko mle ndani.Nikaingia ndani na kumwita mama mkwe nje.

ENDELEA????????. ?Mama samahani,Emmy amekuja yuko nje lakini amegoma kuingia humu ndani baada ya kuliona gari la baba.Ninaomba ukamshawishi aingie ndani kwa sababu kama nikienda mimi

hatakubali kuingia ndani? Mama mkwe akakubali na akaenda nje ya nyumba kuonana na Emmy. ?Wayne vipi,uko salama? Kuna tatizo lolote? Akauliza baba mkwe baada ya kuniona nimerudi ndani na kukaa kimya kimya ?Hapana mzee.Ni mambo ya kawaida ,mama anayashughulikia? Nikasema Baada ya dakika tano hvi mlango unafunguliwa,mama mkwe akiwa ameongozana na Emmy wanaingia ndani.Emmy akiwa ni mwenye sura ya aibu akamsalimu baba yake na mwalimu wa dini halafu akakaa sofani huku amekiinamisha kichwa chake chini.hakutaka kumuangalia mtu yeyote usoni. ?Nadhani tunaweza kuendelea.? Nikasema na kuwatazama watu wote mle ndani.Baba mkwe alikuwa akimuangalia Emmy kwa jicho la hasira mpaka nikaogopa . ?Endelea Wayne? Akasema baba mkwe. ?Kabla hatujasimama nilikuwa nasema kwamba,niliumia sana baada ya kugundua kuwa mwenzangu alikuwa akitoka nje ya ndoa yetu.Mwenzangu hakuwa mwaminifu hata kidogo.Kikubwa zaidi ya yote ni kwamba niligundua kuwa mtoto Baraka hakuwa mwanangu wa damu.Alikuwa na baba yake??? ?Yarabi toba?.? Mama mkwe akasema kwa sauti kubwa huku ameshika kichwa chake.baba mkwe akamshika mkono na kumtoa nje.Mama mkwe ana matatizo ya shinikizo la damu.Baba mkwe aliamua kumtoa nje baada ya kuona hali yake inanza kubadilika. Baada ya dakika kadhaa,baba mkwe akarudi ndani. ?Tuendelee?mama yenu huwa ana matatizo ya shinikizo la damu na habari kama hizi huwa zinamstua sana ndiyo maana nimemtoa nje apumzike.? ?Mwanzoni sikuamini hata kidogo kuwa ni kweli Baraka anaweza kuwa si mwanangu.Kwa mujibu wa meseji nilizozipata ,walizokuwa wakitumiana Emmy na My special one ni kwamba kwa kuwa Baraka tayari amekwisha kuwa mkubwa, anapaswa kuanza kuwafahamu ndugu zake na kwa kuanzia walipanga waanze kumpeleka kwa babu zake huko Same.Ni kweli siku hiyo kama walivyokuwa wamepanga Emmy aliniomba ruhusa kuwa anamsindikiza rafikiye kwenye sherehe ya ndugu yake.Nilimfuatilia bila ya yeye kujua mpaka Same ndipo nilipogundua kuwa huyo mtu aliyemuita kama special one alikuwa ni rafiki yangu wa siku nyingi sana aitwaye Chris.Nilipolitambua hilo nikataka nipate uhakika zaidi nikamuomba emmy tuende tukapime DNA ili tuwe na uhakika mtoto ni wangu au si wangu.Emmy alikataa kata kata ikanilazimu kuondoka mimi na Baraka hadi Dar es salaam na kufanya kipimo hicho cha DNA na majibu ylidhihirisha kuwa ni kweli Baraka si mwanangu.Niliporudi toka dar es salaam nikiwa na majibu ya vipimo vya DNA Emmy tayari alikwisha ondoka nyumbani na nilipompigia simu ni kwa nini aliondoka nyumbani bila ruhusa yangu akaniambia kwamba kwa sasa sina nguvu yoyote ya kuweza kumzuia,na akaenda mbele zaidi kwa kunitaka nisiendelee kumfuatilia.Nilimuelewa lakini nikamuomba aje katika kikao hiki cha jioni ya leo kwa ajili ya kujadili kuhusu suala la mtoto.Kwa ufupi hayo ndiyo niliyowaitia jioni hii ya leo na imekuwa vyema mhusika mkuu naye amefika? Nikamaliza na kuwatazama watu wote mle ndani.Kila mmoja alikuwa kimya .Ukimya mkuu ukatanda mle sebuleni halafu babamkwe akasema kwa hasira. ?Emmy ,japokuwa umechelewa ,lakini umeyasikia yote aliyoyaongea mwenzio.Je una lolote la kuongea? Emmy hakujibu kitu akakaa kimya huku machozi yakimtoka ?nakuuliza tena Emmy una lolote la kuongea kutokana na haya aliyoyasema mwenzio? Naomba usikae kimya nijibu haraka? baba mkwe akasema kwa ukali Emmy akiwa ameuficha uso wake kwa viganja vya mikono akasema ?Yote aliyoyasema ni kweli baba? Baba mkwe akashika kichwa kwa mstuko. .Alipatwa na mstuko wa ghafla.Kila mtu mle ndani alikuwa amepigwa na butwaa.baba mkwe

akainama akatafakari kwa sekunde kadhaa halafu akainua kichwa na kusema ?Emmy naomba urudie tena,haya aliyoyatamka mwenzako ni mambo ya kweli? Huku akifuta machozi akiwa ameinama chini akasema bila kusita ?Ni ya kweli baba? Ghafla baba mkwe akainuka kwa kasi ya ajabu na kutaka kumvaa Emmy kwa kipigo,nashukuru mwalimu wa dini alikuwa karibu akawahi kumshika na kumketisha chini. ?Mtoto una laana wewe.Unawezaje kufanya upuuzi kama huu ? Baba mkwe akasema kwa hasira ?Mzee.Punguza hasira tuyaongee haya mambo kiutu uzima tuyamalize.Najua inauma kama mzazi lakini jitahidi kujizuia mzee wangu ili tuyamalize mambo haya magumu kwa amani?Mwalimu wa dini akasema taratibu akijaribu kumtuliza baba mkwe aliyekuwa amewaka kwa hasira. ?Mwalimu hebu niachieni nafasi nimshikishe adabu baradhuli huyu .Amenitia aibu kubwa .Tutaziweka wapi sura zetu sisi? ..Ouh My God?..? Akasema kwa hasira baba mkwe. ?Aibu hii si yako peke yako.Suala hili limetugusa sisi sote.Wote tunaumia mioyoni mwetu.lakini tunajitahidi kujizuia .Nakuomba mzee wangu tuliza hasira tuyaongee mambo haya na kuwasaidia hawa vijana.? Baba mkwe akatulia lakini alikuwa akihema kwa hasira.Emmy uso ulikuwa umejaa machozi.Mambo haya mimi niliyaona kama ya kawaida kwa sababu nilikwisha yazoea tayari.Nilikwisha umia vya kutosha kwa hiyo sikuwa mgeni wa maumivu haya.Wote tulikuwa kimya tukisubiri kusikia baba mkwe atasema kitu gani. ?Emmy nataka uniambie.Ni kitu gani kimepelekea wewe ukafanya uchafu wa namna hii.Nataka uwe wazi ili tujue na tuone jinsi gani tunaweza kulimaliza suala hili? Emmy alikuwa ameinama akilia.Hakuweza kuinua uso wake kwa aibu.Sebule yote ikawa kimya ikimsubiri yeye aweze kujibu swali aliloulizwa na baba yake. ?Emy nimekuuliza,na ninataka unijibu sasa hivi ni kitu gani kimepelekea wewe ukafanya uchafu wa namna hii ? Hii ni aibu kubwa kwetu kama familia,umetuumiza sana siwezi kukuficha na hasa mama yako ameumia mno.Umemuumiza mwenzako pia kiasi ambacho hakielezeki.Bado kuna mtoto Baraka ambaye ataumia kupita kiasi atakapoelezwa kuwa huyu si baba yake mzazi.Tafadhali usikae kimya hebu tueleze ni kwa nini ulifanya mambo kama haya? Baba mkwe akauliza tena huku hasira zikianza kumpanda. Emmy akafuta machozi kwa kitambaa chake halafu akainua sura yake na kusema kwa kwikwi. ? baba ?kusema ukweli..nilifanya hivi kwa sababu???? Emmy akashindwa kuendelea akaanza kulia. ?Emmy naomba tafadhali usipoteze muda wetu hapa.hebu tueleze ni kitu gani kimekufanya wewe ukamfanyia mwenzako namna hii? Baba mkwe akasema kwa sauti kali ?baba ..niliamua kutoka nje ya ndoa kwa sababu sikuwa naridhika?.Wayne haniridhishi??. Kauli ile inanifanya nihisi kama vile moyo wangu unataka kupasuka kwa jinsi ulivyoyabadilisha mapigo yake na kuanza kwenda kasi.Katika maisha yangu sikuwa nimetegemea kama iko siku Emmy atakuja kutamka kitu kama kile.Nilijitahidi kwa kila niwezavyo kumridhisha kwa kila kitu alichokihitaji bila kujali gharama yake.na hata katika mapenzi ya kitandani nilikuwa mjuvi wa mambo na kila tulipofanya mapenzi siku zote hunisifia na kuniita kidume huku akiapa na kuwatukana wanaume wengine kuwa hawana hadhi ya kumgusa mtu kama yeye kutokana na raha ninazompatia.Sasa iweje tena leo mbele ya wazee atamke kuwa sikuwa namridhisha?Baada ya tafakari fupi nikagundua kuwa alisema vile kama utetezi wake.Uongo ule ukaniuma sana.baba mkwe akamtazama Emmy kwa hasira na kuuliza. ?Emmy unadai kuwa ulifanya uchafu huu kwa sababu mumeo hakuwa akikuridhisha,je kuna siku yoyote uliwahi kukaa naye na ukamueleza kuhusu suala hilo? Emmy hakujibu kitu akakaa kimya.Nilijua alikuwa akiongopa ndiyo maana hakuwa na

jibu.Alipoona Emmy amekaa kimya hana jibu baba mkwe akanigeukia mimi ?wayne hebu tuelze.Kua siku yoyote mkeo alikwisha wahi kukueleza kuwa humridhishi? ?Hapana baba hakuna hata siku moja aliyowahi kuneieleza kuwa haridhiki.Kinachonishangaza ni kwamba mara zote amekuwa akinisifia kuwa hajawahi ona mwanaume kama mimi ,kwa maana hiyo ni kwamaba alikuwa akiridhika saa iweje leo atamke kwamba hakuwa akiridhika? Zaidi ya yote hakuna kitu alichowahi kukitaka mke wangu akakosa hata cha gharama gani.Kuna siku nyingine akiwa nyumbani huwa ananipigia simu na kunieleza kuwa ananihitaji,kwa kumridhisha huwa natoroka kazini na kuja kukaa naye.Hebu muulizeni kama ninasema uongo? ?Emmy umemsikia mwenzio alivyosema.Ni kweli? Emmy hakujibu kitu.Baba mkwe akawagekia wasimamizi wa ndoa yetu na kuwaliza. ?Au alikuwa kushitaki kwenu wasimamizi? ?hapana baba.Hakuna hata siku moja Emmy amewahi kuja kushitaki kwetu kuhusu jambo lolote lile linalohusiana na masuala ya ndani ya ndoa yao? baba mkwe akatafakari kwa muda na kusema ?Inaonekana Emmy umeamua kutunga uongoHuna sababu yoyote ya msingi iliyopelekea wewe kuamua kutoka nje ya ndoa yako,na hata kufikia hatua ya kuzaa nje ya ndoa na kumdanganya mumeo.Mara ya kwanza mwenzio alikufuma na mwanaume akakusamehe na mkafunga ndoa.Niliamini kuwa ulijifunza na ukabadilika .Siku zote hizi umekuwa ukiishi kama mke mwema kumbe ni chui ndai ya ngozi ya kondoo.Inaonekana hii tabia ya umalaya imekwisha kuingia ndani ya damu yako na hautaweza kuiacha.Sasa nakuambia hivi kwa kosa hili ulilolifanya mimi sintakuwa na kusema .Nitamuachia wayne yeye ndiye atakaye amua afanye nini.? Baba mkwe akasema kwa ukali.mwalimu wa dini ambaye alikuwa amekaa kimya muda wote akakohoa kidogo na kusema. ?Jamani naomba na mimi niseme kidogo.Nakubali kuwa Emmy amefanya kosa kubwa sana.Amemkosea mwenzake na hata kuvunja ahadi ya ndoa aliyoiweka mbele ya altare ya bwana.Lakini kama Mungu anavyotuagiza kwamba tusiwe na mipaka katika kusamehe kama yeye anavyowasamehe hata wale wanaomkosea kupita kiasi.kwa maana hiyo kabla hatujaendelea mbele na kikao hiki ningeomba kwanza tujenge mazingira ya kusameheana.Ni kwa njia hiyo pekee tunaweza kuyamaliza mambo haya kwa amani.Halafu kitu kingine ni kwamba tunataka Emmy atueleze nani ni baba wa mtoto ili tuone ni vipi tutafanya kuhusu mtoto huyu.? Mwalimu wa dini akasema lakini kabla hajaendelea zaidi baba mkwe akadakia ?Mwalimu,nafahamu wewe ni mtu wa Mungu na siku zote kazi yenu ni kuhubiri upendo na kusameheana.Lakini nadhani wewe hujaguswa na jambo hili.maumivu ya kufanyiwa kitu kama hiki hayapimiki..Suala la kusameheana naona tumuachie Wayne yeye ndiye atakayeamua kama atamsamehe huyu mke wake au vipi.Tuendelee na kikao chetu.Emmy hebu tueleze huyu mtoto Baraka baba yake ni nani? Kwa upande Fulani nilimuunga mkono baba mkwe kwa kauli yake.Kumsamehe Emmy ilihitaji moyo wa ajabu sana.haikuwa rahisi kusamehe .Emmy hakuwa tayari kusema nani alikuwa ni baba wa Baraka.ote tukakaa kimya tukimsubiri. ?Emmy tunakusubiri wewe ,hebu tueleze ni nani baba wa mtoto ? Emmy hakuwa tayari kusema lolote kuhusiana na mtu aliyezaa naye.Kwa kuwa nilikuwa nikimfahamu ni nani baba wa Baraka nikaona ni bora niwe wazi. ? Baba mkwe hawezi kutujibu huyu.Lakini tayari ninamfahamu baba wa mtoto.? ?unamfahamu baba wa mtoto? Baba mkwe akauliza kwa mshangao ?Ndiyo tayari ninamfahamu? Nikajibu ?Hebu tutajie ni nani huyo? ?Ni rafiki yangu Chris? Kimya kikatanda mle sebuleni.Kila mmoja hakuamini kama Emmy angeweza kuzaa na rafiki yangu. ?Yaani Emmy anadiriki kuzaa na rafiki yako? Baba mkwe akauliza.

?Si tu rafiki yangu,bal ni mtu aliyekuwa rafiki yangu wa karibu sana.Ni Chris ndiye aliyekuwa muandaaji mkuu wa harusi yangu na Emmy.Nilimwamini na kumuona kama ndugu.Sikujua kama iko siku anaweza akafanya kitu kama hiki alichokifanya.? Nikasema kwa uchungu.Ilikuwa inauma sana. ?mambo haya yanazidi kuwa magumu.Na huyo rafikiyako mmekwiha wasilia ana kwa siku za hivi karibuni? Aba mkwe akauliza ?Hapana baba.Ni kitambo kirefu sijawasiliana naye.Mawasilaiano baina yangu na yeye yalianza kufiifia na hatimaye kufa kabisa.Kwa sasa sina mawasilano naye yoyoite yale? Baba mkwe akamgeukia Emmy ?Emmy ni kweli umezaa na rafiki wa Wayne? Kwa sauti yenye kitetemeshi Emmy akajibu ?Ni kweli baba,nimezaa na Chris? jibu lile linampandisha baba mkwe hasira ?Mtoto una laana wewe.Unawezaje kuzaa na rafiki wa mumeo? ?baba Chris ninampenda .Sitaki kuendelea kuishi na Wayne.Nataka nikaishi na Chris tulee mtoto wetu.? Chumba chote kikawa kimya kwa kauli ile ya Emmy.Kila mmoja alikuwa amepatwa na mshangao mkubwa .Kwa wale waliokuwa pale sebuleni ilikuwa ni kama wanaangalia mchezo wa kuigiza lakini ilikuwa kweli. ?baba wewe una mawazo gani ? Baba mkwe akanigeukia na kuniuliza.Watu wote mle sebuleni macho yao yakanielekea mimi ili kunisikia ninatoa wazo gani.Kila mmoja alikuwa akikwepa kutoa hukumu kwa kesi ile ngumu.Nililitambua hilo na nikaamua kuweka wazi yaliyokuwa moyoni mwangu ?baba nadhani nyote mmesikia kwa kauli yake kuwa hana haja ya kuishi tena na mimi.Hili amelitamka mbele yako wewe baba ambaye ni mzazi wake na mbele ya mashahidi ambao walishuhudia ndoa yetu.Mpaka hapa ilipofika mimi nina imani huyu mke wangu amekwisha nichoka na hana mpango na mimi tena.hata kama tukiamua kuyamaliza mambo haya kwa kusameheana na kuanza maisha mapya ni wazi ndani ya nyumba hakutakuwa na amani yoyote wala upendo tena.Mimi kwa moyo mweupe mbele yenu ninyi wazazi na mashahidi ninapenda kuweka wazi lililo moyoni mwangu.? Nikatulia kidogo huku kila mmoja akisikiliza kwa makini sana ili kusikia nitaongea kitu gani ?Kama tulivyoapa siku ya ndoa yetu na padri akatamka kwamba kilichofungwa duniani kimefungwa pia mbinguni kwa maana hiyo ndoa yangu mimi na Emmy haitaweza kuvunjika hadi pale kifo kitakapotutenganisha.Pamoja na yote aliyonitendea lakini bado Emmy ni mke wangu na siku zote sintalisahau hilo.Pamoja na hayo lakini yeye kwa upande wake amelisahau hilo na kutamka wazi kwamba hajisikii tena kuwa na mimi mume wake wa ndoa na kwamba anahitaji kwenda kuishi na mwanaume mwingine ili walee mtoto wao.Natamka wazi kwamba yuko huru kwenda huko atakako kwenda.siwezi kumzuia kufanya atakavyo hata kama tunafungwa na ahadi ya ndoa.Kwa hiyo Emmy mimi nakuruhusu uende huko unakotaka kwenda,ukaishi kwa amani.Inaniuma sana lakini sina namna nyingine ya kufanya.Naamini mateso haya uliyonisababishia Mungu anayaona na iko siku atanipa faraja.Kwa hiyo mama uko huru kwenda unakotaka kwenda.Una ruhusa ya kuchukua chochote ukitakacho humu ndani.Mimi ya kwangu ni hayo tu? Nikasema na kuinama.Nilihisi maumivu makali ya moyo. TUKUTANE SEHEMU IJAYO?????????. ;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;

No comments:

Post a Comment