MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Wednesday, 14 October 2020

BEYOND THE PAIN SEHEMU YA 6


 SEHEMU YA 6

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA ?Beka najua unachokiongea lakini kumbuka Emmy bado ni mke wangu wa ndoa na kama tulivyoelezwa siku tunakula kiapo cha ndoa kuwa kilichofungwa duniani kimefungwa na mbinguni.Hilo ndilo tatizo kubwa linalonifanya nisite kuchukua maamuzi.Nitawezaje kutengua ndoa hii? ? Nikasema huku nikishika kichwa. ?Hivi Wayne huyu mwanamke amekupa kitu gani? Kuna dawa amekulisha wewe si bure.Haiwezekani ugundue mtu amekufanyia kitendo kama hiki halafu bado unamruhusu kulala ndani ya chumba chako.? Beka akasema kwa hasira ?hahahaha Beka achana na mambo ya dawa.Unajua mimi huwa sipendi kuchukua maamuzi ya haraka haraka.Hili ni jambo zito linahitaji utulivu na busara ya hali ya juu kulitatua.usiwe na wasi wasi rafiki yangu suala hili litakwisha.Suala kama hili ni lazima washirikishwe wazee,viongozi wa dini n.kTwende tuendelee na safari tutaongea zaidi tukifika.? Beka akawasha gari tukaendelea na safari ya kurudi Arusha huku akionyesha dhahiri kuchukizwa na msimamo wangu.

ENDELEA???????? Jumapili jioni nikiwa nimepumzika bustanini nikitafakari Emmy akarudi.Baraka aliposikia niko bustanini akaja mbio akanikumbatia na kunisalimu.Emmy naye akaja bustanini haraka .Nilipomuona tu nikahisi hasira kali moyoni.Picha ya Chris ikanijia tena.Nikabadilika ghafla.Emmy akanibusu shavuni .Nilitamani nimkate shingo kwa hasira nilizokuwa nazo.Alionyesha mapenzi mazito kumbe ulikuwa ni unafiki mtupu.Huku akinipapasa kifuani akamwamuru Baraka aende ndani akapumzike .Nadhani hii ilikwa ni janja yake ili nisiweze kumuuliza Baraka kuhusu safari yao. ?Honey habari ya toka juzi? Akasema kwa sauti laini ya kimahaba. ?Nzuri .Pole kwa safari? Nikasema ?Safari nzuri.Jamani honey I missed you so much.? Akasema na kunibusu tena. ?Unajua kukaa mbali nawe hata kwa siku moja naumia sana.Nilipata wakati mgumu mno kwa kuwa mbali nawe.? Akasema huku moyoni akinizidishia hasira. ?Mwanamke shetani huyu..? Nikasema moyoni kwa hasira. ?baby are you ok? Akauliza baada ya kuniona nimekaa kimya ?yah I?m ok? Nikajibu kwa kifupi.Akainua kichwa na kunitazama usoni halafu akakilaza kifuani kwangu.Sikuwa na msisimko wowote kama alivytarajia.Laiti angejua kilichokuwa moyoni mwangu katu asingethubutu kunisogelea karibu. Baada ya mlo wa usiku nikamuaga baraka na kumtaka aende akalale ili kesho asichelewe shule.Haikuwa kawaida yangu kuingia chumbani kulala mapema vile.Dakika chache baadae Emmy akanifuata.Akavaa nguo za kulalia na kuja kujilaza pembeni yangu. ?baba baraka una tatizo gani? Akauliza Nilimtazama kwa makini usoni nikaona jinsi alivyokuwa na wasi wasi. ?Sina tatizo lolote ? Nikajibu

?hapana mume wangu .nakufahamu vizuri una tatizo.Kuna kitu kinakusumbua.Hebu nieleze mume wangu.haipendezi kama una kitu kinakuumiza halafu hutaki kukisema.Mimi ndiye mke wako sasa usiponiambia mimi utamwambia nani tena? Nilitamani kucheka kwa jinsi alivyokuwa akijibalaguza pale kitandani. ?Ni kweli nina tatizo.? Nikasema. ?tatizo gani hilo mume wangu? Akauliza huku akinishika kichwa. Nilikaa kimya kwa sekunde kadhaa nikatafakari kisha nikasema ?Jumamosi ijayo tunasafari ya kwenda dar es salaam.nataka tukafanye DNA test? Emmy akastuka kama vile ameona jini.Akainuka kwa kasi na kukaa huku kijasho kikianza kumtoka usoni.Akaniangalia kwa macho makali. ?DNA test? Akauliza kwa ukali. ?Yes DNA test.Nataka nijue Baraka ni mwanangu au si mwanangu? Nikasema ?Unajua bado sijakuelewa baba Baraka.Unamaanisha nini unaposema unataka ujue Baraka ni mwanao au si mwanao? ?Kwani kuna tatizo gani la kutaka kuwa na uhakika wa mwanao? Nikauliza ?baba Baraka hivi umepatwa na kitu gani? Iweje ukampime mwanao wa kumzaa ? Ina maana umefikia mahala pa kutokuniamini hata mimi mkeo wa ndoa? ?si hivyo mama baraka.Ni katika kujiridhisha tu.Nakuamini sana mke wangu lakini kwa hili utanisamehe kwa sababu nahitaji kufahamu kama Baraka ni mwanangu au si mwanangu? Emmy akakaa kimya.akainuka pale kitandani akasimama na kuanza kuzunguka mle chumbani.Ghafla akageuka huku uso wake umejaa machozi. ?Nasema hivi kama mimi ni mke wako wa ndoa hufanyi hiyo test.Hivi mimi nitakuwa mjinga kiasi gani nikudanganye kuwa Baraka ni mwanao wakati si mwanao?Nasema baraka ni mwanao na hiyo Test haifanyiki? ?na mimi nasema hivi ,kama mimi ni mumeo wa ndoa nitafanya hiyo Test.Lazima nijue Baraka ni mwanangu au si mwanangu?Nikasema kwa ukali. ?Kitu gani kinachokupa wasi wasi kuwa Baraka anaweza kuwa si mwanao? Emmy akauliza. ?Hakuna kitu chochote Emmy nimeamua tu nifanye hivyo ili niwe na uhakika? Emmy akaanza kulia kwa kwikwi huku akilalama kuwa nimevuka mipaka kwa kumuona yeye ni msaliti wa ndoa yetu.Sikumjali nikavuta shuka nikajifunika na kulala.

* * * *

Ni wiki ambayo naweza kusema ilikuwa ni nyeusi ndani ya nyumba yangu.Maongezi na vile vicheko vilivyozoeleka vilikuwa nadra sana kusikika.Emmy hakutaka maongezi na mimi kwani muda mwingi alipotoka kazini alikuwa analala chumbani kwa kisingizio cha kazi nyingi.Sikuijali hali hiyo ,ila nilikuwa makini sana ili hali kama ile isije kumuathiri Baraka..Mtoto hakuwa na kosa na hakutakiwa kusulubishwa kwa makosa ya wazazi wake.Nilijitahidi kuwa naye karibu,kumsaidia kazi za shuleni zilizomshinda,na wakati mwingine tulikwenda bustanini kupiga magitaa yetu.Sikutaka aone kama kuna tofauti yoyote imetokea kati ya wazazi wake.Siku ya ijumaa usiku tukiwa mezani tunapata chakula nikakumbushai juu ya safari ya Dar es salaam kesho yake na kuuliza kama kila kitu kiko tayari.. ?Kila kitu umekwisha kiweka tayari kwa safari? Nikauliza Emmy hakujibu kitu akaniangalia kwa jicho kali . ?Hivi ni kweli umemaanisha kwenda kufanya hiyo DNA test au unanitania? Emmy akauliza ?mama baraka sikutanii.Kesho tunasafri kwenda Dar kwa ajili ya DNA.It?s a serious issue.?Nikasema ?Kama unakwenda nenda mwenyewe.Mimi wala mwanangu Baraka hatutakwenda? Emmy akasema kwa kiburi

?Mama Baraka ,mimi ndiye mwenye kauli ya mwisho katika nyumba hii na ndiye mwenye kuamua nini kifanyike na nini kisifanyike.Kwa maana hiyo basi nasema kuwa kesho alfajiri na mapema wote tunakwenda Dar es salaam.Hili halina kipingamizi na wala sihitaji mjadala tena? Nikasema kwa sauti iliyoashiria hasira ndani yake .Nilifahamu ni kwa nini Emmy hakutaka kwenda kufanya kipimo cha vinasaba.Nina uhakika mkubwa kuwa Baraka hakuwa mwanangu wa damu lakini nilikuwa nataka kuwa na ushahidi mkubwa zaidi wa kibaolojia. ?Kama mnakwenda nyie nendeni lakini mimi sintakwenda Dar es salaam.Mimi ndiye mwenye ukweli wote na hata kama ukienda kupima bado ukweli hautabadilika ?Emmy akasema huku akiubetua mdomo wake kwa dharau akakiweka kijiko chini na kuondoka mezani kwa hasira.Niliumia sana moyoni kwa majibu yake ya kiburi namna ile lakini sikutaka kuonyesha mbele ya mtoto.

* * * *

Siku ya jumanne nilirejea toka jijini Dar es salaam nilikokuwa nimekwenda kwa ajili ya kufanya kipimo cha vinasaba ili kubaini kuwa Baraka ni mwanangu au si mwanangu.Emmy alikataa kata kata kuungana nasi kwenda Dar kwa ajli ya vipimo hivyo ikanuilazimu kwenda mimi na Baraka.Majibu niliyopewa yalinitoa machozi kwani yalionyesha dhahiri kuwa Baraka hakuwa mwanangu wa damu.Japokuwa nilikuwa naelewa kabla kuwa Baraka hakuwa mwanangu lakini sikuwa na uhakika sana hadi majibu haya yaliponidhihirishia wazi .Majibu haya yalinifanya nifikie hatua ya mwisho ya kuutafuta ukweli kama Baraka ni mwanangu au sivyo.Kila nilipomuangali mtoto yule niliyempenda kuliko kitu chochote kile roho iliniuma sana.Emmy alinifanyia unyama mkubwa sana.Ni bora Emmy angenieleza toka mapema nikafahamu kuwa yule si mwanangu.Ameuficha ukweli miaka hii yote na kwa sasa Baraka amekwisha kuwa mkubwa na ana akili za kutosha na hivyo kuambiwa ukweli kuwa mimi si baba yake ni kitendo ambacho kitamchanganya akili na kumuathiri kisaikolojia. Saa moja za za jioni tukawasili Arusha na kuelekea moja kwa moja nyumbani.Nyumbani alikuwepo mtumishi wa ndani peke yake.Nikamuuliza alikoenda Emmy akasema kuwa siku tulipoondoka kwenda Dar es salaam na yeye akaondoka na hajarudi tena hadi leo hii na wala hakusema anaelekea wapi.Sikushangaa wala kuumia rohoni kwa kitendo kile kwa sababu kuendelea kumuona Emmy machoni pangu kungeniongezea hasira.Nikaingia chumbani na kukuta baadhi ya vitu vyake havipo.Nadhani alitambua kuwa kwenda kwangu Dar es salaam kungeweka ukweli wa mambo kuwa baraka hakuwa mwanangu na kwa maana hiyo akaamua kuondoka mapema kabla sijarudi ili kuepusha matatizo.. Nilikaa kitandani nikitafakari kwa kina juu ya maisha yangu na matatizo ambayo Emmy amenisababishia.Toka nimegundua uchafu alionifanyia Emmy nimekuwa nikijipa ujasiri mkubwa kuwa haya ni masuala madogo ambayo katu hayawezi kuniumiza kichwa lakini nikiwa pale kitandani kwa mara ya kwanza nikahisi kitu kama kisu kikali kikiupenya moyo wangu .Nilihisi maumivu makali ya moyo.pamoja na ujasiri wangu wote nilioahidi kuwa nao lakini nilishindwa kuyazuia machozi kunitoka.Hayakuwa maumivu ya kawaida.Ilikuwa ni zaidi ya maumivu.. Kesho yake nikadamka asubuhi na mapema na kujiandaa kumpeleka Baraka shule.Emmy hakurejea na wala sikusumbuka kumtafuta katika simu na kumuuliza yuko wapi ingawa nilipaswa kujua aliko akiwa kama mke wangu.Kwa hasira niliyokuwa nayo moyoni sikuwa tayari kumuona tena akitia mguu nyumbani kwangu.Macho yalikuwa yamevimba na mekundu kwa kukosa usingizi .Baraka alipokuwa tayari akaingia garini nikampeleka shule halafu nikaelekea ofisini.Japokuwa nilijitahidi kuuficha ukweli kuwa kuna jambo linanisumbua lakini wafanyakazi wenzangu walihisi sikuwa sawasawa.Nikiwa ofisini niliegemea kitini na kuanza kutafakari kwa kina juu ya maisha ya furaha niliyoishi na Emmy kumbe nyuma yake kumejaa usaliti na uchafu wa hali ya juu mno.Niliufikiria pia urafiki kati

yangu na Christopher ulivyokuwa wa karibu.Tulikuwa ni marafiki tulioshibana sana na tuliishi kama ndugu.Ni Christopher ndiye aliyesaidia mpaka mimi na Emmy tukarudiana tena baada ya Emmy kunifanyia usaliti miaka ya nyuma kabla hatujaoana.Leo mke wangu wa ndoa anadiriki kuzaa na rafiki yangu wa karibu.Sikuwa tayari kuendelea kuteseka na kuumia moyo kwa ajili yao tena.Nikaamua kuliweka wazi suala hili.Nikachukua simu na kumpigia baba mkwe wangu yaani baba yake Emmy na kumuomba kama ana nafasi nionane naye jioni yeye pamoja na mama.Hakuwa na tatizo mzee yule ,halafu nikampigia tena simu rafiki yangu Beka na kumuomba aje nyumbani kwangu jioni kwa ajili ya maongezi mafupi , nikampigia pia simu mwalimu wa dini ambaye amekuwa karibu nasi na kutulea kiroho kwa muda mrefu.Niliwataarifu vile vile wasimamizi wetu wa ndoa kuwa wafike jioni hiyo kuna masuala muhimu ya kuongea.Nilihitaji na Emmy awepo katika kikao cha jioni hiyo wakati nikiusema ukweli mbele ya wazee na mashahidi lakini sikuwa na hamu hata ya kuongea naye simuni.Baada ya kufikiri mara kadhaa nikaamua kumpigia simu japokuwa moyo ulikuwa hautaki . ?Unasemaje wewe? Akauliza kwa ukali mara tu alipoipokea simu.Nilistushwa na ukali ule na kauli ile ya dharau kwani hakutaka hata kunisalimu.Nilisita kidogo kuongea kutokana na hasira zilizonipanda ghafla.Leo emmy amefikia hatua ya kuniita mimi ?wewe? ?Sema unachokitaka kama husemi nitakata simu? Akasema tena kwa ukali baada ya kuona nimekaa kimya. ?nakuhitaji nyumbani jioni? Nikasema ?Nije kufanya nini? Hivyo vipimo ulivyoenda kufanya si vimeshakupa ukweli sasa unataka nije kwako kufanya nini tena? ?nataka uje tuongee? ?Tuongee nini tena? Hatuna cha kuongea wayne.tayari ukweli unaufahamu kwa hiyo sioni kama kuna kitu tunatakiwa kuongea mimi na wewe.Umeshatambua Baraka siyo mwanao kwa hiyo hata mimi si mkeo.Sifikirii tena kuishi na wewe .Nimechoka mimi maisha ya kubanwa banwa na kufugwa fugwa ndani kama njiwa.Nahitahi maisha ya uhuru,maisha ya kufanya nitakacho.Naomba uniache Wayne.Mimi sifai kuwa mkeo.Unahitaji mwanamke bora wa kuishi naye na si mimi.? Nilivuta pumzi ndefu baada ya maneno yale mazito.Sikutegemea Emmy mwanamke niliyempenda na mbele ya mashahidi kanisani akala kiapo cha kuwa nami katika maisha yote mpaka kufa lakini leo ananitamkia maneno kama haya.Ni shetani gani amemwingia mwanamke huyu hadi akabadilika na kuwa namna hii? ?Emmy mimi sina ugomvi na wewe na hata kama ukitaka kuondoka kwangu mimi sikuzuii kwani ni uamuzi wako.Ninaujua ukweli wote.Ninafahamu Baraka si mwanangu wa damu.Ninafahamu Baba yake ni nani kwa hiyo ninachotaka tukae chini tuongelee suala la huyu mtoto .Tukilimaliza hilo mimi sina tatizo na wewe hata kidogo.You can do anything you want? Nikasema huku moyo ukiniuma kupita maelezo. ?Ok kama nitapata muda nitakuja.? Emmy akajibu kwa dharau na kukata simu.Nilihisi kama dunia inazunguka .sikuwa nimetegemea kama itatokea siku mimi na Emmy tungefikia mwisho wa namna hii.

* * * *

Saa kumi na moja za jioni Baba mkwe akiwa ameongozana na mkewe wakawasili nyumbani kwangu.Niliwakaribisha kwa furaha japokuwa nyuso zao zilikuwa na wasi wasi mwingi.Nadhani mwito ule wa dharura ulikuwa umewastua sana.Tayari Beka,mwalimu wangu wa dini na wasimamizi wetu wa ndoa walikuwa wamekwisha fika muda mrefu na waliokuwa wakisubiriwa ni wakwe.Zaidi ya Beka hakuna aliyekuwa akijua nini niliwaitia jioni ile,hali iliyowafanya wote wazidi kuwa na wasi wasi .Baada ya salamu na maongezi

mafupi,nikafanya utambulisho kwa wageni wote halafu nikafungua kikao. ?Baba na mama mkwe,kwanza kabisa ninapenda kuchukua nafasi hii kuwaomba samahani kwa kuwasumbua jioni hii.Najua mna majukumu mengine mengi ya kufanya .Nashukuru sana kwa kuitikia mwito wangu na kufika hapa.Nawashukuru pia wengine wote mliofika,rafiki yangu Beka,mwalimu wangu wa dini, na wasimamizi wetu wa ndoa.? Kabla sijaendelea mbele zaidi,baba mkwe akadakia. ?Samahani kwa kukukatisha Wayne.Mbona simuoni Emmy hapa? Swali lile linanipa wakati mgumu kidogo kulijibu.Nikafikiri kwa sekunde chache na kusema ? Emmy atakuja si muda mrefu.amepata dharura kidogo? Nikadanganya.Sikutaka kuharakisha mambo.Nilitaka kwanza niwape picha kamili ya mambo jinsi ilivyo.Nikawatazama wote na kila mmoja alikuwa na sura iliyoniashiria niendelee na maongezi. ?Nimewaiteni jioni hii ya leo kuna mambo muhimu ya kuongelea.Nadhani nyote mnafahamu kuwa ndani ya ndoa migongano,mikwaruzano huwa haikosekani.Kunapotokea mikwaruzano au migongano ndani ya ndoa na wanandoa mkashindwa kuisuluhisha basi hamna budi kuwashirkisha watu wa karibu kama wazazi na ndugu wengine wa karibu.Kwa ufupi ni kwamba ndani ya ndoa yetu kumetokea matatizo kidogo ambayo sisi kama wanandoa tumeshindwa kuyatatua ikanilazimu kuwaita na kuwashirikisha katika suala hili.? Nikanyamaza na kuwaangalia wote mle ndani ,kila mmoja alikuwa na hamu ya kutaka kujua nini kimetokea. ?nafikiri nyote mnakumbuka kuwa kipindi kifupu kabla ya ndoa yangu na Emmy kulitokea mtafaruku ambao ulichangiwa na mwenzangu kutokuwa mwaminifu katika uchumba wetu.Sitaki kurudia kulielezea hilo kwa sababu lilikwisha pita na limesahaulika,ila nimelisema tu ili kuweka kumbukumbu sawa.Baada ya usuluhishi wa wazazi na ndugu tulilimaliza suala lile na ndoa ikafungwa.Tumeishi vizuri na mwenzanguu hadi tukabahatika kupata mtoto mmoja.Maisha yetu yamekuwa ni ya furaha kubwa siku zote.? Nikanyamaza tena na kuvuta pumzi halafu nikaendelea ?Siku chache zilizopita,niligundua kuwa mwenzangu amekuwa si mwaminifu katika ndoa yetu.Labda kwa kuelezea tu ilimpate picha halisi ni nini ninakiongea ni kwamba kuna siku niliwahi kutoka kazini,sikuwa na kazi nyingi za kufanya hivyo ikanibidi kuwahi kazini na kuja kukaa na familia yangu .Nilipofika getini nikakutana na mke wangu akitoka nikamuuliza alikokuwa akielekea kasema kuwa wanampeleka jirani yetu hospitali.Nikaingia ndani na kuikuta kompyuta yake iko kitandani,nikaona ni bora niizime.Kabla sijaizima nikagundua kuwa kabla hajatoka alikuwa akiwasiliana na mtu .Kwa kuligundua hilo nikaona ni bora mtu huyo aliyekuwa akiwasiliaana naye nimjibu kuwa asubiri hadi baadae.Nilipatwa na udadisi wa kusoma zaidi baada ya kuona jina la mtu aliyekuwa akiwasiliana mke wangu limeandikwa my special one.Nikajiuliza huyu my special one ni nani? Hata kama ungekuwa ni wewe ni lazima ungepatwa na udadisi wa kutaka kujua huyo special one ni nani.kwa sababu mimi kama mume mke wangu ndiye mtu wangu muhimu,ndiye my special one.Kwa mantiki hiyo hata mke wangu mimi ndiye special one wake kwa sababu aliamua kuwaacha wanaume wote na kuolewa na mimi.Sasa nikastuka baada ya kujua kuwa mwenzangu ana special one mwingine ambaye si mimi.? Nikatulia na kuwaangalia watu wote mle sebuleni.walikuwa kimya kabisa wakiniskiliza.mama yake Emmy alikuwa ameinama ameshika shavu .Nikaendelea. ?Baada ya uchunguzi nikagundua kwamba walikwisha anza kuwasiliana muda mrefu toka Emmy akiwa kazini,na aliporudi nyumbani wakaendelea tena kuwasiliana.Na hiyo haikuwa mara yao ya kwanza kuwasiliana.Baadae nikagundua kuwa kulikuwa na message za kimapenzi walizokuwa wakitumiana.Nikabaini kuwa Emmy ana uhusiano na mtu huyu wa kimapenzi kwa sababu kwa mujibu wa meseji wanazotumiana walikuwa wakikumbushana juu ya siku za nyuma wanazokutana katika mahoteli makubwa na kufanya mapenzi.Si mara moja Emmy huwa ananiaga kuwa anakwenda semina au katika makomngamano au kikazi nje

ya mji kumbe huwa anautumia muda huo kukutana na huyo mtu wake muhimu.Ushahidi wa meseji zote hizo ninao toka walipoanza kuwasiliana.? Mama mkwe akainama chini kwa aibu .Baba mkwe yeye akatoa kitambaa na kufuta jasho lililoanza kumtoka.Kila mmoja mle sebuleni sura yake ikabadilika.Sikutaka kumung?unya maneno,nikaendelea. ?Niliumia sana baada ya kuligundua hilo lakini nashindwa hata kuelezea maumivu niliyoyapata baada ya kugundua kuwa ???.? Kabla sijaendelea mbele mlango ukagongwa.Nikaomba samahani na kwenda kuangalia ni nani aliyekuwa akigonga.Alikuwa ni jirani yetu mama Mwantumu.Mama yule akaniambia kuwa Emmy alikuwa akihitaji kuonana na mimi nje ya nyumba.Amegoma kuinia ndani baada ya kuliona gari la baba yake liko mle ndani.Nikaingia ndani na kumwita mama mkwe nje.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO????????. ;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;

No comments:

Post a Comment