SEHEMU YA 5
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
I know with all my certainty, What's going on with you and me, Is a good thing. It's true, I believe in you.
I believe in Mom and Dad. And I believe in you??????? ?Honey its enough.This song is so touching.? Emmy akanikatisha nisiendelee kuimba.Nilikuwa ninaimba kwa hisia kali sana huku machozi yakinitoka.Nilipomtazama Emmy naye alikuwa akifuta machozi.Nadhani hata yeye wimbo ule ulimgusa. Usiku ule ulikuwa ni moja kati ya usiku mrefu ambao sikuwahi kuupata katika maisha yangu.Sikuweza kupata usingizi.Kichwa changu kilikuwa kimejaa mawazo.Hostoria ya maumivu yaliyonipata miaka kadhaa ya nyuma yakanirudia tena. ENDELEA?????????.. Siku iliyofuata ilikuwa jumamosi,niliamka asubuhi na mapema nikamuaga Emmy kuwa ninaenda ofisini kuna kazi nilitakiwa nikaifanye asubuhi hii na nisinge chelewa kurudi.Siku ya leo ni mapumziko hivyo ofisini nilikuwa mwenyewe.Nikaiwasha kompyuta yangu nikachomeka ile flash disk niliyokopi mawasiliano kati ya Emmy na my special one,mtu ambaye sikumjua ni nani.Nilianza kupitia tarehe moja baada ya nyingine,nikagundua kuwa mawasiliano yao yameanza muda mrefu.Kwa mujibu wa mawasiliano yao ilionesha kuwa walikuwa katika kipindi cha mapenzi mazito.Walikuwa wakiongea mambo mengi kuhusiana
na raha na starehe wanazopeana.Nikagundua kuwa huwa wanakutana katika mahoteli makubwa makubwa na kupeana maraha.Kumbe mara zote Emmy akiniaga kuwa wana semina au makongamano huwa anakwenda kuponda raha na huyo special one.Yote haya niliyagundua katika meseji walizokuwa wakiandikiana.Iliniuma mno siwezi ficha.Nilitamani kutokuendelea kuzisoma meseji zile lakini ilinibidi nizisome zote ili kuupata ukweli wote. Mpaka nilipomaliza kuzisoma chat history zote nikajikuta sina hata nguvu za kuinuka kweye kiti.Jasho lilikuwa likinitiririka. ?God where are you? Please help me? Nikasema kwa uchungu mwingi.
* * * * Wiki iliyofuata ilikuwa ni wiki ngumu kwangu kupita maelezo.Nilijitahidi kutokuonesha dalili zozote zile kuwa kuna jambo lolote linanisumbua kichwani kwangu.Kila nilipomuona Baraka furaha yote ikapotea.Masikini malaika yule hakuwa na kosa lolote,hakuwa akifahamu kilichokuwa kikiendelea.Alifahamu fika kuwa baba yake mzazi ni mimi.Hata mimi bado niliendelea kuamini hivyo bado sikuwana na uhakika wa kutosha kwa yale niliyoyanasa kati ya mke wangu emmy na my special one ni ya kweli.Nilihitaji ushahidi wa kutosha..Jumanne jioni baada ya kazi nikaenda kuonana na rafiki yangu mmoja aitwaye beka anayefanya biashara ya kuuza magari.Nilimuomba anisindikize kwenda Same siku ya jumammosi tukitumia gari lake.Japokuwa alitaka kufahamu kwa undani juu ya safari hiyo lakini sikumpa jibu la moja kwa moja.Kutokana na ukaribu wetu akakubali kunisindikiza Same kwa kutumia gari lake. Siku zikaenda kwa kasi na hatimaye ikafika siku ya Ijumaa.Usiku tukiwa kitandani Emmy huku akikichezea kifua changu bila kujua kama alikuwa akinikera kupita kiasi ,akasema ?darling ,kesho ndio ile safari niliyokwambia .Nasikitika kukuacha mwenyewe,utakuwa mpweke sana.? Nikatabasamu na kusema ?Ni kwa nini usimuache baraka ? ?hapana honey .Unajua Baraka kuna wakati anakuwa msumbufu sana.Acha tu niende naye asije akabaki akakusumbua .? ?Hawezi kusumbua.Yupo dada yake wa kazi atakuwa akimlea.?Nikajibu. ?Siku hizi Baraka amekuwa mtundu sana.Honey acha niende naye.Siku mbili tu si nyingi .? ?Mtaondoka na usafiri gani? Nikauliza ?Mimi nitaondoka na gari yangu? Akajibu Emmy huku usoni akionesha dalili za kutopendezwa na jinsi nilivyokuwa nikinga?ngania Baraka abaki.Nilikuwa nikielewa kila kitu hivyo haikunipa shida yoyote. ?Ok nadhani hat mimi kesho nitaondoka asubuhi na mapema kuna kazi ninawahi kwenda kuifanya ? Nikasema ?Ok baby? Akajibu Emmy akanibusu na kulala.Alipogeuka upande wa pili nikafuta mdomo wangu mahala aliponibusu kwa kiganja cha mkono. Emmy hakujua kilichokuwa kikiendelea moyoni mwangu lakini ukweli nilikuwa namchukia kupita kiasi kwa mambo anayonifanyia.Pamoja na hayo niliendelea kujifanya mjinga ili niweze kupata ukweli wa mambo.Sikutaka kuyaendea haraka mambo haya mazito. Asubuhi na mapema,nikaamka ,nikaoga na kuagana na Emmy.Nikapanda gari langu na kuelekea nyumbani kwa Beka maeneo ya Sakina.Nilimkuta tayari amejiandaa ananisubiri. Hatukupoteza muda tukaingia katika gari lake na safari ikaanza. ?Beka najua bado unajiuliza maswali mengi toka nilipokwambia kuhusu safari hii.lakini ukweli ni kwamba kuna gari ambayo itabidi tuifuatilie inakwenda Same.? Nikasema ?Tunaifuatilia gari??Beka akauliza ?yes..kuna gari tunakwenda kuisubiri Bomang?ombe na tutaifuatilia mpaka Same.? Beka akakaa kimya akabadili gia na kulipita lori la mafuta halafu akanigeukia.
?Wayne whats going on? Toka nimekufahamu sijawahi hata siku moja kukuona ukiwa katika hali kama hii.Kuna kitu unanificha .Hebu kuwa muwazi kama kuna tatizo ili tusaidiane jinsi ya kulitatua. Wewe ni rafiki yangu na tatizo lako ni la kwangu? Ni kweli Beka alikuwa mmoja kati ya marafii wangu amabao naweza kusemea ni wa kweli.Sikuona sababu ya kumficha tatizo langu Nikatabasamu na kujibu ?beka,kusema ukweli nina tatizo kubwa lakini siwezi kukueleza kwa sasa hadi hapo nitakapokuwa na uhakika wa kutosha.Kwa sasa naomba tu unisaidie kulifuatilia hilo gali nitakalokuonesha.? Beka hakujibu kitu tena,akakubaliana nami.Akakanyaga mafuta hadi tulipofika eneo la Boma,tukasimamisha gari pembeni ya bara bara. Mpaka saa nne za asubuhi bado Emmy alikuwa hajapita ,nikawa na wasi wasi pengine anaweza akawa amepanda gari jingine,nikaamua kumpigia simu. ?hallow Emmy,umeshaondoka? ?yes? darling nimeondoka muda si mrefu,kwa sasa nelekea maeneo ya KIA?akasema Emmy. ?Unatumia usafiri gani,wa kwako au umepanda basi? Nikauliza ili kupata uhakika zaidi ?Ninatumia gari yangu? ?Ok honey Mimi ndio natoka kazini muda huu,msalimu baraka? Nikakata simu huku beka akiniangalia kwa jicho kali. ?unaongea na mkeo? ?yah ! ni mke wangu? Nikajibu ?Tunamfuatilia mke wako? Sikujibu kitu nikakaa kimya ?Wayne tell me please.Tunamfuatilia mke wako.? ?Yes Beka tunamfuatilia mke wangu.? ?ouh My God whats going on Wayne? Beka akauliza ?Nitakwambia Beka lakini sio sasa.Ni habari ndefu sana.? Beka akajua lazima liko tatizo kati yangu na Emmy.akawa na subira akisubiri muda ukifika nimueleze mimi mwenyewe kwa mdomo wangu nini kinaendelea.Tuliendelea kusubiri huku tukiburudishwa na muziki ,mara nikaliona gari la mke wangu mama baraka likija.Nikamstua Beka aliyekuwa nje akiongea na simu.Akaingia garini tukaanza kulifuatilia gari lile. Beka alilifuatilia gari lie kwa ustadi mkubwa ili tusije shukiwa kuwa tunawafuatilia.gari la Emmy likaongoza hadi katika hoteli moja mpya na ya kisasa sana ijulikanayo kama Uhuru white peak hotel.Hatukuweza kuingia mle ndani ya ile hoteli kubwa ya kifahari tukabana sehemu tukiwasubiri watoke.Baada ya kama saa moja hivi wakatoka na safari ya kuelekea Same ikaanza.Nadhani walikuwa wameenda kupata mlo wa mchana Tulifika Same saa nane za mchana,.Pale hatukutaka kuendelea kulitumia gari letu hivyo ikatulazimu tulipaki mahala penye usalama tukakodisha gari aina ya Noah,tukaendelea kuifuatilia ile gari ya Emmy.Gari ya Emmy ikasimama nje ya nyumba moja kubwa yenye geti la kijani,na kupiga honi.Mara mlango ukafunguliwa na akashuka mwanaume mmoja ambaye sura yake haikuwa ngeni kwangu.Nikavua miwani myeusi niliyokuwa nimeivaa ili nimuangalie vizuri mtu yule .Sikutaka kuamini kuwa akili yangu ilikuwa sahihi.Sikutaka kuamini mtu niliyemuona toka ndani ya ile gari ni yeye kweli au wamefanana.Nilibaki mdomo wazi. ?No Its not true.Chris!!!! Nikasema kwa uchungu. Ndugu msomaji aliyeshuka toka ndani ya ile gari ya Emmy alikuwa ni rafiki yangu wa siku nyingi aitwaye Chris ambaye alifanya kazi kubwa katika kufanikisha harusi yangu mimi na emmy.Ni mmoja kati ya watu ambao mchango wao kwangu sina uwezo wa kuulipa.Chris mtu ambaye nilimhesabu kama mmoja wa ndugu zangu kabla ya uhusiano wetu kuanza kupungua taratibu kiasi cha kuweza kumaliza hata mwaka mzima hatujaonana. Nikiwa naendelea kushangaa nilichokiona,geti linafunguliwa na gari linaingia
ndani..Nilikuwa nimelowa jasho mwili mzima. ?Tuondoke eneo hili Wayne? akasema Beka Tuliondoka eneo lile na kurudi hadi mahala tulipoacha gari letu.Tukamlipa yule jamaa mwenye ile gari tuliyoitumia akaondoka zake ?Tunaelekea wapi baada ya hapa? Beka akauliza Sikujibu kwa haraka.Nilitafakari nini kifuate baada ya hapo.Niendelee kumfuatilia Emmy au nirudi nyumbani? Nikajiuliza mwenyewe na mwishowe nikaamua kurudi nyumbani. ?Twende turudi nyumbani Beka.tayari nimeshaujua ukweli? Nikasema huku Beka akiniangalia na kisha akaondoa gari. Safari yetu ilikuwa ya kimya kimya .Nilikuwa na mawazo mengi mno .Tulipofika maeneo ya kwa Sadala Beka akauvunja ukimya. ?Wayne najua si vizuri kuingilia mambo yasiyonihusu lakini wewe ni rafiki yangu na kama una jambo lolote linalokusumbua basi hata mimi linanihusu.Hebu niambie kuna tatizo gani? Sikuona sababu yoyote ya kumficha Beka juu ya tatizo linalonikabili.Nikaamua kumweleza ukweli wote ulivyo.Beka akasimamisha gari pembeni ya bara bara baada ya kuusikia ukweli.Hata yeye alistuka sana. ?Wayne ni ya kweli hayo unayonieleza? Beka akauliza ?kwa nini nikudanganye Beka.Haya yote ni ya kweli kabisa.?Nikasema.Beka akavuta pumzi ndefu na kusema kwa sauti ndogo ? I cant believe this.? Akanyamaza kidogo halafu akasema ?Kwa jinsi ninavyomfahamu mke wako niliamini ni mmoja kati ya wanawake waadilifu mno katika ndoa zao.? ?hata mimi nilikuwa naamini hivyo na sikujua kama anaweza akanifanyia kitu kama hiki.Namsikitikia mtoto kwa sababu hajui lolote.Ninampenda mno Baraka.Niliamini yeye ndiye mrithi wangu na ndiye furaha ya maisha yangu.baada ya kugundua kuwa si mwanangu sijui hata nifanye nini.Ninampenda mno mtoto yule Beka? Nikasema kwa uchungu. ?Kwa hiyo umepanga kufanya kitu gani? Beka akauliza.Swali hili kwangu lilikuwa moja kati ya maswali magumu kujibu.Sikuwa nimepanga kufanya chochote na wala sikujua ningefanya nini.Kwa kitendo alichokifanya Emmy sikuona hata adhabu gani inayomstahili. ?Beka sijapanga bado nifanye kitu gani.bado nahitaji ushahidi wa kutosha ili niweze kujiridhisha na hatua nitakazozichukua..I think I need more time? Nikasema ?More time??.Beka akauliza kwa mshangao. ?More time? Akarudia tena. ? Wayne naona kama unafanya utani na suala kama hili.Hili si suala dogo kama unavyolichukulia.Ni suala zito mno.Mkeo ameisaliti ndoa yenu na ushahidi wa uhakika unao.Umemfuatilia mkeo hadi Same na umegundua kuwa anaetembea na mkeo ni rafikiyo sasa ushahidi gani tena unaouhitaji? Hebu chukua hatua stahili mapema? Beka akasema kwa hasira.Beka alikuwa sahihi kwa upande Fulani lakini bado moyo wangu ulikuwa mzito kuchukua hatua za haraka.Beka alikuwa ameukunja uso kwa hasira.Kitendo kile ni wazi kilikuwa kimemuumiza mno. ?Beka uko sahihi kuwa ushahidi unajitosheleza kwa kiasi kikubwa.lakini bado nahitaji muda zaidi wa kufikiri nini cha kufanya.Sitaki suala hili limuumize baraka.Nataka suala hili niliendee taratibu? Nikasema ?Taratibu? Beka akauliza tena. ?Wayne sidhani kama suala hili linakuumiza.Naona unalifanyia mzaha.Taratibu wakati mkeo bado anaendelea kukudanganya ,bado anakuona hayawani,anatembea na rafiki zako halafu unasema unachukulia mambo taratibu..Be serious my friend? beka akasisitiza. ?nakuelewa Beka,lakini hizo hatua unazonisisitiza nichukue ni hatua zipi? Hebu nishauri? Nikasema
?Hakuna ushauri hapa.Fukuza tu aende kwa huyo hawara yake.? Beka akajibu kwa hasira kali. Nilishindwa kukasirika ikanibidi nicheke . ?sasa unacheka nini Wayne? Wanawake wa namna hii dawa yao ni kuwatimulia mbali ili wakafunzwe na dunia.Sipendi watu wasiokuwa na hisani? ?Huo ndio ujinga wa wanawake.kwa jinsi ninavyofahamu ni kwamba Chris ana mchumba wake na tayari amezaa naye mtoto mmoja.Kwa sasa binti huyo yuko nje ya nchi kimasomo.Kwa maana hiyo ahadi kwamba atamuoa Emmy na kwenda kuishi naye nje ya nchi ni uongo mtupu.Chris akisafiri na kwenda nje ya nchi huwa anakwenda kumtazama mchumba wake na si vinginevyo.Iwapo nikimtimua Emmy hatakuwa na mahala pa kwenda kwa sababu ninamfahamu vizuri Chris.Hii ndiyo tabia yake kuwahadaa wanawake.Ninayemuonea huruma hapa ni Baraka.? Beka bado hakuridhika na maelezo yangu ?Wayne mimi nakuonya ,mwanamke huyu si mzuri na hafai katu kuishi naye.Sikushauri uendelee kuishi naye.Mtimue haraka sana.? ?Beka najua unachokiongea lakini kumbuka Emmy bado ni mke wangu wa ndoa na kama tulivyoelezwa siku tunakula kiapo cha ndoa kuwa kilichofungwa duniani kimefungwa na mbinguni.Hilo ndilo tatizo kubwa linalonifanya nisite kuchukua maamuzi.Nitawezaje kutengua ndoa hii? ? Nikasema huku nikishika kichwa. ?Hivi Wayne huyu mwanamke amekupa kitu gani? Kuna dawa amekulisha wewe si bure.Haiwezekani ugundue mtu amekufanyia kitendo kama hiki halafu bado unamruhusu kulala ndani ya chumba chako.? Beka akasema kwa hasira ?hahahaha Beka achana na mambo ya dawa.Unajua mimi huwa sipendi kuchukua maamuzi ya haraka haraka.Hili ni jambo zito linahitaji utulivu na busara ya hali ya juu kulitatua.usiwe na wasi wasi rafiki yangu suala hili litakwisha.Suala kama hili ni lazima washirikishwe wazee,viongozi wa dini n.kTwende tuendelee na safari tutaongea zaidi tukifika.? Beka akawasha gari tukaendelea na safari ya kurudi Arusha huku akionyesha dhahiri kuchukizwa na msimamo wangu.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO??????? ;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;
No comments:
Post a Comment