MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Monday, 12 October 2020

BEYOND THE PAIN SEHEMU YA 4


 SEHEMU YA 4

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA MY SPECIAL ONE: Jumamosi ya wiki ijayo.Anza kuandaa tararibu mazingira ili Mumeo asiweze kugundua chochote. EMMY: Nitajitahidi darling MY SPECIAL ONE: Vipi weekend hii una ratiba gani? MY SPECIAL ONE: BUZZ BUZZ BUZZ BUZZ MY SPECIAL ONE : ?Vipi Darling mbona kimya? Are you there???

BUZZ BUZZ BUZZ

Mawasiliano yakaishia hapa.nadhani ni wakati huu Emmy alipopata taarifa ya ugonjwa wa jirani yetu na kumfanya aondoke ghafla bila hata kukumbuka kuizima kompyuta yake.Ilikuwa ni kama ndoto ya mchana.Sikuamini nilichokuwa nimekisoma,nikakaa vizuri na kurudia tena na tena .Nikafungua archive na kukuta kumbukumbu ya mawasiliano kati ya Emmy na my special one.Jasho lilikuwa likinitiririka,mapigo ya moyo yakaanza kwenda kwa kasi isiyoelezeka.Nikakaa kitandani huku nikihisi kuishiwa nguvu taratibu.

ENDELEA??????.. ?No this must be a joke.Its not true? Nikasema mwenyewe huku nikijifuta jasho ?Emmy cant do to me something like this? Nikasimama na kuzunguka zunguka mle chumbani ,nikapata wazo.Nikachukua flash disk yangu nikaichomeka katika ile kompyuta ya Emmy na kurekodi kumbukumbu zote za mawasiliano baina yake na huyo special one.baad ya hapo nikaiacha kompyuta ile kama ilivyokuwa .Sikutaka Emmy aje agundue kuwa nilikuwa nimezisoma meseji zake.Mambo yakle niliyoyasoma amabayo nilihisi ni kama utani vile ni makubwa na yalihitaji uchunghuzio wa hali ya juu.Nilipohakikisha kuwa hataweza kugundua kitu chochote nikatoka,na kwenda kukaa sebuleni.Sikuwa na nguvu hata za kuendesha gari.Nikaanza kutafakari yale niliyoyasoma. ?MY SPECIAL ONE? Who is my special one? Nilihitaji kumfahamu huyo aliyeandikwa kama my special one. ?I need to find out the truth.I?ll find out the truth.And if its true,you?ll cause me another pain ? this will be BEYOND PAIN? Nikasema mwenyewe huku nikiuma meno kwa uchungu. Sikumbuki usingizi ulinipitia saa ngapi ila nilistuka kwa busu zito nililopigwa katika paji la uso.kwa haraka nikafumbua macho ,kumbe alikuwa ni mke wangu Emmy amerudi toka hospitali.Moyo ukastuka sana nilipomuona.Ghafla kumbukumbu ya nilichokisoma katika kompyuta yake ikaja kwa kasi .Hasira ikanipanda kwa ghafla sana lakini nikajikaza kiume na kuonyesha sura ya tabasamu ili kumfanya asiwe na wasi wasi.Sikutaka kupeleka mambo kwa haraka hadi pale nitakapokuwa na uhakika wa kutosha kama yale niliyoyasoma ni mambo ya kweli au si kweli ?hello darling? Nikasema kwa sauti ya chini na ya uchovu ?Ouh my love,mbona umenyong?onyea hivyo ,unaumwa? Akauliza emmy huku amekaa karibu yangu na kunishika kichwa. ?Siumwi kitu honey ni uchovu tu unanisumbua? Niliumia tena moyoni kutamka neno honey.lakini kwa kuwa nimeshaamua kuliendea suala hili taratibu sikuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kuonyesha mapenzi kwa Emmy ili asije kung?amua kama ninafahamu lolote kuhusu siri zake. ?Baba baraka kwa nini hujaenda kulala chumbani ?.Toka umerudi umelala hapa kwenye kochi ? Akauliza emmy ?Kuna kipindi nilikuwa naangalia katika Tv nikajikuta nimepitiwa na usingizi.Vipi mgonjwa anaendelaje? Mbona mmewahi kurudi namna hiyo? Nikauliza na kumfanya Emmy ajibu kwa wasi wasi kidogo ?Tumemfikisha hospitali ,nimeacha anashughulikiwa mimi nikaondoka? ?Yaani mama baraka unaondoka na kuwaacha wenzako hospitali bila hata kujua mgonjwa anaendeleaje? ?baba Baraka nilikuwa nakuwahi wewe,nilijua ungekuwa mwenyewe ungeboreka sana? Nilitabasamu baada ya kujua kuwa ananidangaya.Nafikiri alipofika hospitali alikumbuka kuwa hakuizima kompyuta yake na ndio maana akarudi haraka namna ile.

?Ngoja nikabadili nguo nioge,pengine nitajisikia vizuri ?Nikainuka kuelekea chumbani kwangu na kumuacha mama Baraka akiwa kwene sofa akionekana mwingi wa mawazo.Chumbani sikuikuta ile kompyuta yake kitandani ,alikuwa ameishaitoa na kuizima kabisa halafu akaifungia katika kabati lake.Nikatabasamu nikavua nguo na kwenda kuoga kisha nikarudi na kijilaza kitandani.Mlango ukafunguliwa Emmy akaingia,akanifuata pale kitandani nilikokuwa nimelala akanikumbatia na kunibusu. ?Honey nikupikie chakula gani leo? Akauliza ?Chochote utakachopika mi nitakula tu? Nikajibu huku nikitabsamu ?Ok honey nitakupikia chakula kitamu ajabu.Halafu honey kuna jambo nataka tuongee? ?Jambo gani hilo ? Nikauliza Emmy akakaa kimya akafikiri kwa sekunde kadhaa na kusema ?unajua kuna rafiki yangu mmoja tuko naye ofisi.moja ana harusi ya mdogo wake jumamosi ijayo na inafanyikia nyumbani kwao Same .Ameniomba nimsindikize .Sijampa jibu lolote nikaona ni bora nije nikuombe ruhusa wewe..? Emmy akasema. Nusura chozi linidondoke baada ya kusikia maneno yale.Nilianza kuamini kile nilichokisoma .Emmy na mu aliyemwandika kama my special one walikuwa wamepanga kwenda nyumbani kwa huyo special one kumtambulisha Baraka kwa babu zake yaani baba na mama yake huyo special one.Iliniuma kupita kiasi.Nikakaa kimya nikifikiri nini cha kusema. ?Darling niambie basi,utaniruhusu kwenda?? akasema Emmy Sikujibu kitu nikaendelea kufikiri ?Honey say yes please? akanibembeleza Emmy. ?hakuna shida ,waweza kwenda?nikajibu kwa ufupi. ?Ouh honey thank you..mwaaahh? akasema na kunibusu mdomoni.akatoka na kuelekea jikoni ?Ee Mungu kwa nini mambo haya yananikuta mimi? Nikawaza kwa uchungu huku machozi yakinilenga lenga.Nilikuwa nimejilaza kitandani ikanilazimu niinuke na kukaa. Kichwa nikaanza kukiona kizito mno.Mateso na maumivu niliyoyapata miaka kadhaa iliyopita yamerudi tena. ?Daddy !!?.?Nikastuliwa na sauti ya Baraka aliyekuwa amerudi toka shuleni ?Ouh Baraka.umerudi ! Nikasema. ?Ndiyo baba.pole na kazi?Akasema ?ahsante mwanangu.Habari ya shule? ?Nzuri baba? Mtoto hyu akaniongezea tena machungu.Nilimpenda Baraka kupita kitu chochote kile katika maisha yangu. ? This cant be.Baraka is my son? Nikasema kimoyo moyo. ?daddy mbona unalia? Akaniuliza Baraka na kunifanya nistuke.Nilikuwa nimeshindwa kujizuia kutokwa na machozi nilipomuona baraka. ?macho yananisumbua sana leo? Nikajibu na kujilazimisha kutabasamu. ?Haya Baraka nataka nipumzike,nenda kabadili nguo halafu baadae uje unionyeshe umejifunza nini shuleni leo? ?Ok Daddy? baraka akasema na kutoka mle chumbani.Nilimsindikiza kwa macho mtoto yule mzuri mwenye akili nyingi ,niliyemkuza katika adabu na tabia njema kiasi cha kumfanya kuwa mfano wa kuigwa mtaani na hata shuleni kwao. ?Kwa nini Emmy anifanyie mimi mambo haya?Kwa nini anitese namna hii? Nikawaza. ?.Ni lazima nifanye utafiti nigundue ukweli uko wapi..halafu huyu mtu anayemuita special one?Ni nani? Lazima nimfahamu mtu huyu? Mawazo yakawa mengi nikaona ni bora nikakae sebuleni .Nikaanza kutazama televisheni lakini hakuna kitu nilichokuwa nikielewa.Bado mawazo yangu yote yalikuwa katika suala zito linaloniumiza kichwa.Muda wa chakula ulipofika tukakaa mezani,tukala chakula huku

nikijilazimisha kutabasamu na kucheka ili kumfanya emmy asihisi lolote. ?baraka kesho ni weekend,siku ya mapumziko,right? Nikamuuliza baraka mara tulipomaliza kula chakula cha usiku. ?Yes daddy ,kesho ni jumamosi? Akajibu ?Ok pretty boy,now take you guitar.We?re going to play out in the moon and have fun? Nilikuwa nimemfundisha Baraka kupiga gitaa.Naye kama mimi alikuwa mpenzi sana wa nyimbo za country.Kila mara tupatapo wasaa huwa tunakaa bustanini na kupiga magita yetu . Tukaelekea bustanini,mimi ,Baraka emmy na mbwa wetu aitwaye Chesa. ?Daddy leo tunapiga wimbo gani? Baraka akauliza ?Leo tunaimba I believe in you wa Don Williams.This song is special for your mother ,the love of my life.I want to show your mother how much I do believe in her? Nikasema na kumfanya Emmy atabasamu lakini nikagundua tabasamu lake lilikuwa na uoga ndani yake. ?One,two,three?.Tukaanza kupiga huku nikiimba.Nilikuwa mpigaji mzuri sana wa gitaa ?I don't believe in superstars, Organic food and foreign cars. I don't believe the price of gold; The certainty of growing old. That right is right and left is wrong, That north and south can't get along. That east is east and west is west. And being first is always best.

But I believe in love. I believe in babies. I believe in Mom and Dad. And I believe in you.

Well, I don't believe that heaven waits, For only those who congregate. I like to think of God as love: He's down below, He's up above. He's watching people everywhere. He knows who does and doesn't care. And I'm an ordinary man, Sometimes I wonder who I am.

But I believe in love. I believe in music. I believe in magic. And I believe in you.

I know with all my certainty, What's going on with you and me, Is a good thing. It's true, I believe in you.

I believe in Mom and Dad. And I believe in you??????? ?Honey its enough.This song is so touching.? Emmy akanikatisha nisiendelee kuimba.Nilikuwa ninaimba kwa hisia kali sana huku machozi yakinitoka.Nilipomtazama

Emmy naye alikuwa akifuta machozi.Nadhani hata yeye wimbo ule ulimgusa. Usiku ule ulikuwa ni moja kati ya usiku mrefu ambao sikuwahi kuupata katika maisha yangu.Sikuweza kupata usingizi.Kichwa changu kilikuwa kimejaa mawazo.Hostoria ya maumivu yaliyonipata miaka kadhaa ya nyuma yakanirudia tena. TUKUTANE SEHEMU IJAYO???????.. ;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;

No comments:

Post a Comment