MATANGAZ0 YETU 



Breaking

Saturday, 10 October 2020

BEYOND THE PAIN SEHEMU (3)


 SEHEMU YA 3

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA Maneno yale machache yakampa Emmy faraja kubwa na kumfanya ainuke na kunikumbatia kwa furaha.Sebule yangu ikageuka sehemu ya furaha kubwa.Watu tukashikana mikono na kupongezana.Lilikuwa nitukio kubwa na la kihistioria katika maisha yangu.Vinywaji vikaletwa tukaendelea kuburudika hadi ilipotimu saa mbili za usiku tukaagana wakaondoka.Walipoondoka nikabaki mwenyewe nikitafakari juu ya kilichotokea.Pamoja na kumsamehe Emmy lakini bado roho yangu haikuwa ikimtazama kama nilivyokuwa nikimtazama hapo zamani. ?Hivi ni kweli roho yangu imekubali kwa dhati kumsamehe Emmy kwa kitu alichonifanya?? Nikajiuliza tena kwa mara ya pili.Saa chache zilizopita sikutamanai kkumuona tena Emmy katika maisha yangu kuokana na kitendo kile lakini sasa nimeaua kumsamehe. ?Kwa vile nimamua kumsamehe acha tu nimamehe.Nahisi amekiri toka moyoni

mwake.?Nikajisemea mwenyewe. Maisha mapya yakaanza tena.Penzi letu likaonekana kama vile limechipua upya.Upendo ukaongezeka mara dufu.Enmmy alionekana kubadilika sana na hiyo ikanihakikishia kuwa hawezi kurudia tena kosa alilolifanya. Taratibu jeraha lililokuwa moyoni mwangu likaanza kufutika.Nikaanza kusahau yote yaliyokuwa yamepita.

ENDELEA????????..

Ni siku yetu ya kufunga ndoa.Sikuweza kupata usingizi usiku mzima.Nilikuwa nikiwaza kama ni kweli baada ya kupitia msuko suko mkubwa hatimaye ninakwenda kufunga ndoa.Ilikuwa ni kama ndoto. Asubuhi nilikuwa ni mtu mwenye mawazo na wasi mwingi.Mpambe wangu aliliona hilo ,akajaribu kunitoa wasi wasi na kunifanya nichangamke.Kwa mara nyingine tena nikajikuta niukijiuliza kama ninalokwena kulifanya leo hii ni sahihi na nina uhakika nalo.Baada ya tafakari ya kina nikaona hakuna haja ya kuendelea kujiuliza maswali mengi.Maji nimekwisha yavulia nguo hivyo sina budi kuyaoga. ?mwenzangu,pokea pete hii iwe ishara ya upendo na uaminifu kwako.Kwa jina la baba nan mwana na la roho mtakatifu.Amina? Nilitamka maneno haya huku nikimvisha pete ya Ndoa emmy kama mke wangu halali mbele ya kanisa lililofurika watu wakiwa kama mashahidi.Wakati nayatamka maneno haya bado ndnai ya nafsi yangu kuna kitu kilikuwa kikiniuliza ?Wayne are you sure with what you are doing? Sauti ile ilikuwa ikiniuliza kama ninayatamka manenoyale kwa dhati toka moyoni mwangu..Sikuijali sana sauti ile ,kwa sababu nilijua nimekubali kwa dhatiya moyo wangu kufunga ndoa na Emmy.Niliamini mwangwi ule ulitokana na tukio lililotokea na ambalo bado jeraha lake halijapona sawa sawa..Tukio ambalo kusema ukweli haliwezi kufutioka kiurahisi. Baada ya kumalizika kwa shughuli za kanisanii,shghuli kubwa ikafanyika ukumbini.Ilikuwa ni sherehe ya aina yake na kila mmoja aliyehudhuria alisuuzika moyo.Saa sita za usiku tukaondoka ukumbini na kuwaacha bado watu wakishereheka,tukaenda katika hoteli tuliyoandaliwa maalum kwa ajili ya kulala kwa usiku huo kabla ya kuelekea katika fungate letu tuliloamua kwenda Zanzibar. Huo ukawa ni usiku wetu wa kwanza kama mke na mume.Ni usiku huo ambao naweza nikasema kuwa maisha yangu yalianza upya.

* * * *

Maisha ya ndoa yalikuwa mazuri na yenye furaha.Nilionyesha kila aina ya upendo kwa Emmy.naye hali kadhalika alionyesha upendo wa kila namna kwangu ilimradi ilikuwa ni furaha na mashamsham kila siku.Kila asubuhi ni kama penzi letu lilianza upya.Miezi hii sita ya kwanza sikuona kitu chochote kibaya cha kunikwaza na ambacho kingenifanya niseme ule msemo uliozoeleka wa ndoa ndoano.Sikuyaona magumu ya ndoa.Niliwashangaa wale wote wanaodai kuumizwa na ndoa zao.Sikuelewa ni kwa nini wengine hawakutaka kabisa kusikia kitu ndoa.Kwa furaha niliyokuwa nayo nikwa ndani ya ndoa sikuweza kufikiri kama iko siku ninaweza kutembea nje ya ndoa.Niliwashangaa wale watu ambao wamekuwa na wapenzi nje ya ndoa zao.Sikuhitaji mpenzi wa nje kwa sababu nilipata kila kitu nilichohitaji toka kwa mke wangu Emmy.Kwa muda huu mfupi nikanawiri na kuvutia zaidi.Nikawa mshauri maarufu wa kuwashauri vijana wenzangu ambao bado walikua wakisita na kuogopa ,kufanya maamuziya kufunga ndoa kwa sababu ndoa ni tamu ajabu. .Nilitolea mfano wa raha nizipatazo mimi . Mwezi wa saba toka tufunge ndoa Emmy akanitaarifu kuwa tayari alikuwa mjamzito.Hii ikaongeza furaha na upendo mara dufu ndani ya familia yetu.

Furaha hii haikuwa tu baina yetu bali hata kwa ndugu na jamaa zetu.Nilimshukuru Mungu kwa kunipa mke kama Emmy.Nilimpenda mno mke wangu na hasa katika kipindi hiki cha ujauzito.Siku zikazidi kusonga na hatimaye siku ya kujifungua ikafika na Emmy akafanikiwa kujifungua mtoto mzuri wa kiume aliyekuwa na afya bora.Nilifurahi kupita kiasi kwa zawadi ile ya mtoto.Ndugu ,jamaa na marafiki wakaungana nasi katika furaha ile kubwa ya kupata mtoto.Kwa furaha niliyokuwa nayo nilimzawadia Emmy zawadi ya gari jipya kabisa kama shukrani zangu kwake kwa kumleta duniani mtoto wetu mpendwa ambaye nilipendekeza aitwe Baraka.niliamini mtoto yule alikuwa ni baraka za mweneyezi Mungu kwetu.Emmy akafurahi mno kwa zawadi le niliyompa. Ukurasa mpya wa malezi ukaanza nikiwa baba na Emmy akiwa mama.Nilifurahi kushirikiana na mke wangu katika malezi ya mwanetu Baraka.Muda wa mapumziko ya uzazi ulipokwisha ikatyulazimu kumtafuta msaidizi atakayetusaidia kumlea mtoto wakati tukiwa kazini.Tulifanikiwa kumpata msaidizi kwa msaada wa jiani yetu. Siku zilikatika kama mvua na ikafika miezi sita.Tukajadili tukaona kuwa huo ndio muda unaofaa kwa ajili ya kumbatiza mwanetu.maandalizi yakafanywa na hatimaye tukafanikiwa kumbatiza mwanetu kwa jina la baraka.Mtoto akaendelaa kukua akiwa na afya njema mno.

* * * *

Miaka minne ilipita.Maisha yakiwa ni yenye furaha na upendo mkubwa.Mtoto wetu baraka alikuwa anasoma katika shule ya awali ya Maria Theresa academy.Baraka alikuwa akiendelea kukua kwa furaha na upendo mkubwa. Kwa muda wa miaka yote hiyo hali ya upendo ndani ya ndoa yetu ilikuwa kubwa na hii ilitufanya tuwe mfano wa kuigwa.Nilikwisha sahau yote yaliyotokea kipindi cha nyuma.Nilichokuwa nikiangalia kwa sasa ni malezi ya mtoto wetu na kumtengenezea maisha mazuri ya baadae. Ilikuwa siku ya Ijumaa siku ambayo sikuwa na shughuli nyngi za kufanya nikaamua kuwahi kurudi nyumbani ili kujumuika na famili na yangu .Siku zote huwa nikipata nafasi hupendelea kuwahi kurudi nyumbani na kuitumia nafasi hiyo nikiwa na familia yangu tukifurahi pamoja. Nikiwa mita kadhaa kabla ya kufika nyumbani kwangu nikaona geti likifunguliwa na gari ya mke wangu ikitoka.Tulipokutana akasimamamisha gari,akashusha kioo tukasalimiana. ?Hello Darling? akasema mama Baraka ?Hello honey? nikajibu ?Mbona leo mapema hivi kulikoni? Akauliza ?Nimeamua kuja kukaa na familia yangu.Sikuwa na kazi nyingi.Safari ya wapi tena? Nikauliza ?Kuna mama mmoja jirani yetu ni mjamzito sasa ameanguka ghafla ndio tunataka tumkimbize hospitali? ?Ouh ! basi wahini mara moja.? Nikajibu naye akaliondoa gari kwa kasi kumuwahi mgonjwa..Nikaingiza gari ndani nikasalimiana na mwanangu Baraka halafu nikamwacha akicheza mimi nikaelekea chumbani kwangu.Kitandani kulikuwa na kompyuta aina ya Laptop ya mke wangu.Kwa kuwa nilikuwa nikihitaji kupumzika nikaamua kuitoa na kuiweka pembeni.Kompyuta ile ilikuwa imechomekwa katika umeme na ilionyesha kuwa muda mfupi uliopita alikuwa akiitumia.Kwa haraka haraka nikaona kama alikuwa akiwasiliana na watu wake kwa kutumia Yahoo messenger.Kuna meseji ilikuwa ikikonyeza kuashiria kuwa haikuwa imesomwa,nikang?amua kuwa Mama Baraka alikuwa ameondoka ghafla na kumfanya asahau kuizima kompyuta yake.Nikaamua kufunga ile Yahoo messenger ili watu wale aliokuwa akiwasiliana nao wajue kuwa hayupo.Kabla sijaifunga kabisa ile Yahoo messenger,nikaliona jina moja limeandikwa My special one.nikapata udadisi Fulani.Nikafungua ule ukurasa waliokuwa wakiwasiliana nikaanza kuusoma .Meseji ya

mwisho ilisema ?Vipi Darling mbona kimya? Are you there??? Baada ya meseji hiyo zikafuata BUZZ nyingi..Nilikuwa nimesimama nikaamua kukaa na kusoma sawa sawa.Nikaanza kuisoma tokea mwanzo.Kutokana na muda ilionyesha kuwa walikuwa wameanza kuwasiliana kama dakika ishirini zilizopita.Mfululizo wa mawasiliano yao ulikuwa hivi EMMY: Nimeshafika nyumbani dear MY SPECIAL ONE : Ouh ! good.Mimi bado niko ofisini EMMY: Unatoka saa ngapi leo MY SPECIAL ONE : Leo nitachelewa kutoka kidogo. EMMY: Ok poa Darl ,sasa hebu tuendelee kujadili lile suala la mtoto manake mimi linalipa wakati mgumu sana MY SPECIAL ONE: Darl ni kama nilivyokueleza kuwa mtoto ni lazima nikamtambulishe kwa babu zake.Nataka mtoto aanze kunizoea taratibu ili hata baadae akielezwa kuwa huyu ndiye baba yako mzazi asishangae.Nataka aanze taratibu kuwafahamu ndugu zake. EMMY: Darl unanipa wakati mgumu sana.Nashindwa hata nifanye nini MY SPECIAL ONE: Usiogope Darl.Unajua mtoto anakua kwa kasi na anazidi kupata akili.Kwa maana hiyo inabidi aanze kujua toka mapema ,nani baba yake nani siye.Nashukuru kwa ile safari ya mbuga za wanyama imeniweka karibu naye sana. EMMY: Yah hata mimi nimefurahi kwa hilo kwa sababu kila siku ni lazima akuulizie. MY SPECIAL ONE: Hivyo ndivyo ninataka.Jaribu kwa kadiri uwezavyo kumuweka karibu zaidi na mimi. EMMY: Nakubali Honey mtoto ni wako lakini siku huyu jamaa akigundua najua ataumia mno.Hujui ni jinsi gani anavyompenda Baraka MY SPECIAL ONE: Yah ! I now that.Ni wazi ataumia lakini hakuna jinsi.Ni lazima ifike mahala akubaliane na ukweli kuwa mtoto si wake.Na kwa kweli darling sitaki tuendelee kulificha hili kwa muda mrefu.nataka ifike wakati tuchukue uamuzi wa kumueleza ukweli kuwa mtoto si wake.Tukiendelea kukaa kimya tutakuwa hatumtendei haki mtoto. EMMY: Lakini darling ni wazi siku Wayne akiufahamu ukweli hakutakuwa na jingine zaidi ya kuachana.Niliwahi kumuumiza mara moja miaka kadhaa ya nyuma na nikamuahidi kuwa sintamuumiza tena.Sasa akigundua hili sijui nini kitatokea. MY SPECIAL ONE: Honey usijali kitu chochote.bado naendelea kuweka mazingira mazuri ili kama kutatokea la kutokea pindi utakapomueleza ukweli basi moja kwa moja unahamia kwangu na tunaanzisha familia,mimi ,wewe na mtoto wetu baraka. EMMY : (smiley) Are you sure darling? MY SPECIAL ONE :Yes baby I?m sure.Lengo langu mimi sikuzote limekuwa kuishi na wewe.Nataka kuishi na mwanangu.nataka mwanangu akasome Ulaya.Nataka siku moja sisi sote tukaishi Ulaya. EMMY : Ingawa nakupenda na niko tayari kufanya lolote kwa ajili yako lakini kila ninapomfikiria mume wangu nafsi inanisuta sana.Wayne ananipenda kupita maelezo. MY SPECIAL ONE: Usijidanganye baby kuwa mumeo anakupenda.Unachotakiwa ni kuangalia wapi unapata furaha ya maisha.Fuata moyo wako unavyokutuma. EMMY : Ok tuachane na hayo.Umepanga lini umpeleke mtoto kwa babu zake? MY SPECIAL ONE: Jumamosi ya wiki ijayo.Anza kuandaa tararibu mazingira ili Mumeo asiweze kugundua chochote. EMMY: Nitajitahidi darling MY SPECIAL ONE: Vipi weekend hii una ratiba gani? MY SPECIAL ONE: BUZZ BUZZ BUZZ

BUZZ MY SPECIAL ONE : ?Vipi Darling mbona kimya? Are you there??? BUZZ BUZZ BUZZ

Mawasiliano yakaishia hapa.nadhani ni wakati huu Emmy alipopata taarifa ya ugonjwa wa jirani yetu na kumfanya aondoke ghafla bila hata kukumbuka kuizima kompyuta yake.Ilikuwa ni kama ndoto ya mchana.Sikuamini nilichokuwa nimekisoma,nikakaa vizuri na kurudia tena na tena .Nikafungua archive na kukuta kumbukumbu ya mawasiliano kati ya Emmy na my special one.Jasho lilikuwa likinitiririka,mapigo ya moyo yakaanza kwenda kwa kasi isiyoelezeka.Nikakaa kitandani huku nikihisi kuishiwa nguvu taratibu.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO????????.. ;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;

No comments:

Post a Comment