SEHEMU YA 2 ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
? Haloo? Nikasema ?Wayne umelala?? ?Ndiyo nilikuwa nimelala? ?Ok .Sasa wayne naomba uwe na moyo mgumu na usihamaki tafadhali.Ni kwamba Emmy amenifuata na hapa nilipo niko naye na ni yeye ndiye alinisisitiza nikupigie simu hii.? ?Unasemaje Chris????? ?Nikasema kwa ukali.Sikutegemea kusikia kitu kama kile. ?Wayne niko na Emmy hapa.amenitafuta na kuomba nafasi ya kuongea na wewe? ?Chris????..?Nilidakia,sikutaka aendelee tana kunipa habari za yule baradhuli ?Chris tafadhali.Kama na wewe unataka tukosane hamna shida ila tafadhali naomba usinipe habari zozote kuhusu huyu mwanamke.? Nikakata simu.Mwili wote ulikuwa unanichemka kwa hasira.Sikutaka kumsikia tena emmy katika maisha yangu.Nilikuwa na hasira mbaya mno kwa kitendo alichonifanyia na kama angekuwa karibu yangu sijui hata ningemfanya kitu gani.
ENDELEA?????????.
?Hana haya mwanamke huyu.Kwa hiki kitu alichokifanya halafu leo anataka kuongea na mimi!! Aongee na mimi kitu gani? Kwanza si ana nguo zake humu .Zote nazipiga moto.Sitaki kumuona tena machoni mwangu huyu mwanamke.Amenifanyia kitendo cha kikatili sana.? Nikalifungua kabati kwa hasira na kuanza kutoa ngo zote za Emmy.Nyingi nilimnunulia mimi mwenyewe na ni nguo za thamani kubwa. ?Nguo zote hizi nimegharamia hela nyingi kumbe alikuwa akiniona mimi mjinga namna hii??.? Nikazikusanya zote na kwa hasira nikaenda nazo katika shimo la taka taka na kuzichoma moto.Sikuondoka mpaka nikahakikisha zimeteketea kabisa . Nikarudi sebuleni na kuangalia kama kuna kitu chochote kinachoweza kumuhusu Emmy,nikaiskia geti linagongwa.haraka haaka nikafuta uso na kujiweka vizuri ili mtu asije gundua nilivyosawajika. Nilifungua geti na kukuta ni rafiki yangu anaitwa Erasto. ?karibu Erasto ?ilijilazimisha kuchangamka. ?Ahsante sana wayne? ?Nimekuja kukujulia hali ,niliambiwa na akina mangi jana ulipata matatizo ukalazwa hospitali? Akasema Erasto tukiwa tumekaa sebuleni ?Ndiyo,jana nilipatwa na matatizo ya mstuko nikaanguka na kupoteza fahamu.Ni mambo ya uchovu.Si unajua tena ,mambo yamekuwa mengi sana.? Nikadanganya.Sikutaka mtu yeyote agundue kilichotokea kati yangu na Emmy ?Du! Pole sana.lakini hivi sasa unaendeleaje? ?Kwa sasa naendelea vizuri.Madaktari wamenipima na hakuna tatizo lolote,wameniomba niongeze muda wa kupumzika.? Nilishukuru kwa erasto kuja kunitazama kwani kidogo kichwa changu kilitulia.Tuliongea na kucheka nikaona kichwa kinakuwa chepesi.Mida ya kama saa nane hivi Chris naye akaja akiwa amefungasha chakula,tukajumuika wote kula.Kwa masaa haya machache nilifarijika sana na kujiona kama vile sina matatizo. Ilipata saa kumi na moja jioni tukiwa katika maongezi na rafiki zangu ,geti langu likagogwa.Nikainuka na kwend akumuona mgongaji.Nilistushwa na ujio usio wa kawaida wa
mwalimu wangu wa dini.katekista Nzomola ndiye mwalimu wetu aliyetufundisha mafundishoya ndoa mimi Emmy na watu wengine kama nane hivi. ?Ouh Mwalimu,Shikamoo? Nikamsalimia kwa furaha,sikutaka kuonyesha aina yoyote ya mstuko kwa ujio wake.hajawahi kuja nyumbani kwangu hata mara moja. ?Marahaba Wayne.Habari za Jumapili? ?Nzuri katekista.? ?Leo sijakuona kanisani,hata mwenzio naye sikumuona ? ?Leo sikuwa najisikia vizuri ndio maana sikuja.Si unajua mwalimu nyakati hizi mambo yanakuwa mengi ? Katekista akatabasamu.nikamkaribisha ndani.Nikamtambulisha kwa Chris na Erasto amabo baada ya kuona nimepata mgeni wakaaga na kuondoka. ?Ndio mwalimu karibu sana.hapa ndio nyumbani kwangu.? ?Ahsante nimeshakaribia.? Kimya kikapita cha kama dakika moja hivi ,katekista akaanzisha maongezi ?Wayne nimekuja hapa ili tuzungumze juu ya matatizo yaliyotokea? Kauli ile inanistua. ?Matatizo?? yapi hayo? ikauliza ?yaliyotokea kati yako na mwenzako? ?nani kakwambia kuna matatizo? Nikauliza tena ?Mwanzako amenifuata nyumbani .Tangu saa saba mpaka mida hii ndio tumeachana.Amekuja analia na kutaka tukae tuyaongee masuala haya? Nilimtazama mwalimu yule kwa hasira mpaka akaogopa. ?Mzee Nzomola nakuheshimu mno kama mzee wangu,umenijenga sana kiroho.Lakini kwa hili lililotokea naomba usiingilie kabisa.Hakuna kitu tunachoweza kuongea hapa.Halafu mpaka hapa nilipo kichwa changu bado hakijatulia,bado nina hasira na hatuwezi kuongea lolote na tukafikia muafaka .Mzee wangu naomba uniache kwanza nitulie halafu kwa heshima yako nitakuita mimi mwenyewe tutakaa ,tutaongea.Usione kama nimekudharau mzee wangu ,hali niliyonayo sasa hatuwezi kuongea tukafikia muafaka.Niachie siku mbili tatu,kichwa kitulie halafu nitakutafuta mimi mwenyewe.Nakuahidi hivyo.? Nashukuru mzee Nzomola alinielewa na akaondoka. Jumatatu sikwenda kazini,nilituma taarifa kwa wakuu wangu wa kazi kuwa ninaumwa.Mida ya kama saa tano nikiwa nimepumzika sofani nikitafakari simu yangu inalia.Nikaangalia mpigaji alikuwa ni baba mkwe yaani baba yake na Emmy.Niliiangalia simu ile ikiita na kukata ,ikaanza kuita tena.Nilikuwa na hasira na sikutaka kusikia lolote juu ya Emmy.Mwishowe nikakata shauri niipokee tu. ?Haloo mzee shikamoo? ?Nzuri baba hujambo?? ?Sijambo mzee wangu ,sijui nyie mnaendeleaje? ?Sie huku wazima.Vipi ali yako kwa sasa unaendeleaje? ?Naendelea vizuri tu mzee.Nashukuru Mungu? Kimya kikapita cha sekunde kadhaa ,halafu akasema. ?sasa Wayne nimekupigia simu hii nilikuwa na maongezi na wewe ya muhimu sana.Tafadhali ni muhimu mno.Uko kazini? Nikasita kujibu ,nilijua hakuna kingine kinachoongelewa hapa zaidi ya suala la Emmy. ?Niko nyumbani mzee? Nikajibu kwa ufupi. ?Ok vizuri .Basi nitakuja mida ya saa kumi za jioni ili tuongee mwanangu.Tafadhali naomba unisubiri? ?Sawa mzee wangu nitakusubiri hapa hapa nyumbani? Nikakata simu na kuirushia katika kiti.Nadhani hata huyu mzee aligundua kuwa sikuwa katika hali yangu ya kawaida.
* * * *
Saa Tisa kama na nusu hivi za jioni nikasikia honi ikipigwa nje ya geti langu.Nilikuwa nimejilaza chumbani nikaamka na kwenda kufungua mlango.Ilikuwa ni gari ya baba yake Emmy pamoja na gari nyingine mbili jumla gari tatu.Nikawakaribisha ndani.Sikutegemea kama kungekuwa na ujumbe mkubwa vile.Watu zaidi ya kumi.Wengine nilikuwa nawafahamu kama shangazi yake zake Emmy na baba zake wadongo lakini wengine ikawa ni mara yangu ya kwanza kuwaona.Kwa picha ile ya ule ugeni nilielewa dhahiri kuwa hapa linaloongelewa ni suala langu na Emmy hakuna lingine. Katika friji kulikuwa na vinywaji,hivyo nikamkirimu ila mmoja na kinywaji alichohitaji. Nilisikia wakiongea kichaga,kana kwamba walikuwa wakielekezana jambo.Halafu mzee mmoja mwenye mvi na kitambi akakohoa kidogo na kusema. ?Bwana Wayne tunashukuru sana kwa ukarimu wako na kwa jinsi ulivyotupokea.hatukutegema kabisa kama ungeweza kutukirimu kwa upendo namna hii.Unaowaona hapa mbele yako ni baba,mama ,mashangazi na wajomba wa mchumba wako emmy? Alipotaja neno ?mchumba wako Emmy? nikauma meno kwa hasira,nikainama chini.Nafikiri hata wao waligundua kitu. ?Bwana wayne kwa ufupi tumekuja hapa sisi kama wazazi wa emmy ili kujaribu kuweka sawa mambo yaliyotokea.Hatukuwa tunajua nini kinaendela.Sisi tulikuwa katika maandalizi ya harusi.hatukujua kilichojificha nyuma ya pazia.Jana usiku ndio baba yake akatupigia simu na kutukusanya na kutueleza kuwa kuna tatizo limetokea.Emmy alitueleza yote mwanzo hadi mwisho bila kuficha hata kitu kimoja.Kwa kweli tulistuka sana sana.mama yake presha ikapanda ikabidi apelekwe hospitali.Tunashukuru Mungu hali yake imeendelea vizuri na mpaka sasa tunaye hapa.Kwa kweli kwanza sisi kama wazazi na wanafamilia ya Emmy tunakupa pole sana kwa yaliyotokea na vile vile tunakupongeza kwa ujasiri na uvumilivu wako.Umeonyesha uvumilivu na busara ya hali ya juu sana.Angekuwa ni mtu mwingine sijui tungekuwa tunaongea nini saa hizi.Ni wazi angefanya mambo ya ajabu sana.? Akatulia akakohoa kidogo halafu akaendelea. ? Wayne narudia tena kuwa hata sisi suala hili limetuuma mno.hatukutegemea kama tungepata aibu ya namna hii.Hii ni aibu kubwa na hata kuja kukuona na kuongea na wewe leo hii ni kwa sababu hatuna jinsi.Lengo letu kubwa la kuja hapa sisi ni kujaribu kuona nini tufanye ili kuweza kuokoa kile ambacho tumekwisha kianza.pamoja na kuwa inauma na bado una hasira lakini najua ndani kabisa ya moyo wako bado kuna kiasi Fulani cha upendo kwa emmy.Emmy Amelia sana na kuomba msamaha mno na kuahidi kuwa amekwisha achana na yule mtu wake aliyemsababishia haya yote.Amelia sana na ametutuma tuje sisi kama wazee tuombe msamaha kwa niaba yake .pamoja na shetani aliyepita kutaka kuvuruga mipango mizuri ya mbeleni ya maisha yenu lakini nina tumaini kuwa bado kuna kila dalili ya upendo wa kweli kati yenu.Suala la nyumba ni gumu na mambo kama haya huwa yanatokea.hakuna nyumba inayokosa majaribu na misuko suko.Na mnapojaribiwa ni wazi yupo atakayeanguka au mkaanguka wote.lakini sikuzote upendo wa kweli husimama panapo majaribu na hata mkijaribiwa mwisho wa siku mtabaki mnapendana na kusimama imara.Sikuzote wapendanao kweli hata kama wakianguka hushikana mikono ,wakasimama na kusonga mbele.Upendo wa kweli siku zote haushindwi na lolote.Ninaona picha ya upendo wa kweli ulio kati yenu.Ni upendo hu wa kweli ndio uliokuzuia kufanya lolote mpaka leo hii.Roho wa Mungu yuko pamoja nawe na ndiye anayekuongoza katika kufanya maamuzi haya yenye busara.kwa maana hiyo Wayne sisi wazee wako tumekuja rasmi kama wazazi kukuangukia na kuomba msamaha na kufuta kila kilichotokea ,tusimame pamoja tushikane mikono na tusonge mbele.Tumekosa sisi tunaomba utusamehe sisi.Emmy yuko tayari kuja kuomba msamaha mbele yetu sisi wazee wake.hatukuweza kuja naye mpaka tutakapoongea na wewe na tuone
kama utakuwa tayari kumsamehe mwenzako? Akamalizia mzee yule ambaye alikuwa akiongea kama mchungaji vile.Sijui wazee hawa walikuja na nini manake nilijisikia maneno yao yakiniingia moyoni na kujikuta licha ya hasira nilizokuwa nazo kutaka kumsamehe Emmy.Kuna wakati ulikuwa unakuja moyo wa kusamehe lakini papo hapo inakuja picha ya Emmy akiwa amekumbatiana na lile libaba.Ikija picha hii hasira zinarudi tena. Niliinua kichwa niliposikia baba yake Emmy akikohoa na kutaka kuongea machache. ?Wayne mwanangu,na mimi naona niongezee machache katika yale aliyoyasema mkubwa wangu.Kwa kweli pamoja na uzee wangu huu nilikuwa nimeishiwa maneno ya kusema ndio maan nikamuachia mkubwa wangu.Ameeleza kila kitu na sitaki kurudia yale aliyoyasema ila nata kusema machache kuwa Emmy ni binti niliyemlea katika maadili mazuri ya kiroho na kwa kweli alikuwa ni binti mwenye heshima kubwa.Sikutegemea kwa jinsi nilivyomlea aje afanye yale aliyoyafanya.Ndio maana hata mama yake aliposikia mambo haya presha ikapanda kwa sababu hatukumlea awe mtu wa namna hii.Nina imani tabia hii aliyoifanya ni mambo ya tamaa na kuiga.Tena ni baada ya kutoka nyumbani.Pale alipoanza maisha yake ya kujitegemea.Mwanzoni alipotaka kuhama nyumbani na kwenda kuishi mweneyewe nilikataa kwa kuhofia asije akaambukizwa kufanya mambo yasiyofaa katika jamii lakini aliomba sana kuwa anataka ajifunze maisha ya kuishi mwenyewe ndipo nikamruhusu.Hii si tabia yake hata kidogo.Hakuwa na tabia hizi.Ni tamaa tu ya kuwa na pesa na vitu vizuri vizuri.Toka akiwa mdogo nilimfundisha kutambua mara moja anapokosea na kuomba msamaha.Kweli amelitambua kosa alilolifanya na kuomba msamaha.Mimi kama baba yake nilikataa kabisa kabisa kuishughulisha tena na masuala yake baada ya kusikia aibu aliyoifanya.Aliniomba sana sana nimsamehe na nimsaidie kuomba msamaha kwako.Kwa macho yangu niliona katika macho yake kuwa alikuwa akimaanisha toba ya dhati.Ni hilo ndilo lilinisukuma mie nimsamehe na kunifanya nifike hapa leo pamoja na wenzangu hawa kuomba msamaha kwa niaba yake kwanza na baadae yeye mwenyewe atafika hapa na kuomba msamaha kwako mbele yetu.Wayne hatutaki katika hatua kubwa mliyofikia mshindwe kuendelea.Mkisameheana katika hili nina imani mtakuwa mmejenga kitu kikubwa sana na nyumba yenu itajengwa katika kusameheana hata likitokea kubwa la aina gani.Kwa hayo machache Wayne mimi kama baba yake naomba sana niko chini ya miguu yako msamehe mwenzio na muendelee na mipango yenu ya ndoa kama kawaida.? Baada ya baba yake Emmy kumaliza kuongea akafuata shangazi yake na baba zake wadogo.Du ! niliombwa kila aina ya msamaha.Kila aina ya ushawishi ilitumika ili niweze kumsamehe Emmy.Kwa kweli sijui wazee hawa walikuwa na kitu gani manake niliwasikiliza na kujikuta ninakuwa na moyo mweupe tena wa kumsamehe Emmy.Pamoja na kwamba zile picha mbaya zilikuwa bado zikinijia nilijawa na moyo wa kusamehe.Hatimaye ikaja zamu yangu kuongea.Kila mmoja akatulia kutaka kunisikiliza nitasema nini. ?wazee wangu nimewasikilza vizuri.Ujio wenu leo umenipa faraja sana.Sijui mmekuja na kitu gani lakini kwa kweli najiona mwepesi na mwenye furaha sana.Mmenisaidia kuutua mzigo mzito niliokuwa nimeubeba.Ahsanteni sana.Wazee wangu kwa kweli lililotokea ni pigo kubwa kwa moyo wangu.Nimeumia sana.Kwa kweli sikutegemea jambo kama lile kutokea kwa mtu kama Emmy tena kwa wakati kama huu.kama mzee pale alivyosema ni kwa maongozi ya Mungu niliamua kutumia busara zaidi katika suala hili.Sijamueleza mtu yeyote zaidi ya rafiki yangu wa karibu.Sikuwa na haraka ya kutaka kuutangazia ulimwengu nini Emmy kafanya.Sikutaka dunia imchukie.naamini kama mzee alivyosema ni tamaa za pesa ,mali na vitu vizuri vizuri ndio ilmponza.Iwapo ningeamua kumdhalilisha Emmy kwa kutangaza aliyoyafanya ,nisingekuwa nafanya hivyo kwake tu bali hata kwa wazee wake waliomlea katika madili mema,ndugu zake,ndugu zangu na hata wazazi wangu.Pamoja na yote yaliyotokea,machungu yote niliyoyapata,maumivu ya ndani na nje,bado ninathubutu kusimama nakutamka mbele yenu wazee wangu kuwa nimemsamehe Emmy na niko tayari
kurudiana naye tena na mipango ya ndoa yetu kuendelea kama kawaida? Hawakuamini ,wakanitaka nirudie tena kauli yangu.Nikarudia tena na kuwahakikishia kuwa Emmy nimemsamehe kwa moyo mmoja na wala sina kinyongo naye tena. Wazee wakainuka na kuja kunipongeza.Kilikuwa ni kipindi cha furaha sana.Baada ya kupongezana baba yake mkubwa Emmy akasimama na kusema. ?Wayne wewe ni kijana wa ajabu .Katika kuishi kwangu mpaka nimefika uzee huu sijawahi kuona mtu mwenye moyo wa ajabu kama wako Wayne.laiti dunia ingekuwa na vijana 100 kama wewe basi pangekuwa ni sehemu nzuri sana kwa kuishi.Mimi binafsi sijui hata niseme kitu gani.Sijui hata nikushukuru vipi kwa ujasiri wa kumsamehe mwenzako.Narudia tena kijana unaongozwa na roho wa Mungu.Kwa ulimwengu wa sasa si rahisi mtu kumsamehe mwenzake aliyemfanyia kitendo kama alichokufanyia emmy.Ahsante sana kijana.ahsante sana wayne? akanishika mkono tena.Akawageukia wazee wengine na kuwaambia kuwa ni wakati muafaka kwa Emmy kuitwa .Ikapigwa simu na baada ya kama dakika kumi hivi Emmy akaingia ndani.Moyo wangu ukastuka tena baada ya kuiona sura ya Emmy ikiwa na macho mekundu yaliyovimba ikiashiria jisni alivyokuwa akilia.hakutaka kuniangalia usoni.Uso wake alikuwa kuinamisha chini.Nilishindwa kuwa na hasira nikamuonea huruma. Baba mkubwa wa Emmy akasimama na kuongea machache. ?Kijana wetu Wayne,na ndugu wote ambao mko hapa leo,napenda kuchukua nafasi hii kuongea machache kwa sababu mengi yamekwisha semwa na nisingependa kuyarudia tena.Tumemsikia kijana wetu alivyosema.Toka ndani ya moyo wake amekubali kumsamehe Emmy .Kwa kuwa kijana wetu Wayne si mtenda kosa basi hatuna budi sasa kumpa nafasi mtenda kosa yeye mwenyewe kwa mdomo wake akiri kosa na kuomba msamaha kwa mchumba wake,wazazi wake na kwa Mungu wake.Emmy uwanja ni wako ,waangukie wazazi wako uwaombe msamaha pamoja na mchumba wako? Kimya kikatanda mle sebuleni.Emmy huku akilia akainuka na kwenda kupiga magoti mbele ya baba yake na kulia akiomba kusamehewa.Baba yake akamshika kichwa na kumuombea kwa Mungu amsamehe na kumtangulia katika kila jambo alifanyalo,halafu akatangaza kuwa tayari amemsamhehe mwanae kwa kosa alilolifanya.Emmy akaenda tena kwa mama yake na kuomba msamaha kama alivyofanya kwa baba yake.Naye halikadhalika akamsamehe.Kazi ikawa kwangu.Akasita kuja kwangu pale tulipogonganisha macho.Nadhani ni nafsi yake ilikuwa ikimsuta kwa mambo aliyoyafanya.Wazee wake wakamuangalia kwa ukali hali iliyomlazimu kujikaza kisabuni na kunisogelea.akapiga magoti mbele yangu na kunishika miguu. ?Wayne, nakosa hata neno la kusema.Nashindwa nikwambie kitu gani cha kuweza kulifuta doa nililoliweka moyoni mwako kwa tamaa zangu.Nimekuumiza Wayne,na sistahili hata huruma yako.lakini pamoja na hayo yote niliyokufanyia naomba ufahamu kitu kimoja kuwa toka ndani ya moyo wangu bado nakupenda sana na ninaomba msamaha wa dhati kabisa .Naomba unisamehe na tuendelee na mipango yetu ya ndoa kama tulivyokuwa tumepanga.naahidi sintafanya tena kosa kama hili katika maisha yangu.nakuahidi kuwa mke mwema kama utanisamehe.naomba msamaha wako Wayne..? Emmy macho yalikuwa yamejaa machozi,akilia kwa kosa alilokuwa amelifanya.Hata mimi ilikuwa ikiniuma sana na nilikuwa nikijiuliza mara mbili mbili kama ni kweli nimeamua kwa dhati kumsamehe? Nikakubaliana na moyo wangu kuwa nikubali kumsamehe.Nikamshka mkono nikamuinua na kumtazama usoni. ?Emmy,nakubali ulinikosea.Lakini kama tunavyofundishwa kila siku nav iongozi wetu wa dini na kama maandiko yanavyosema kuhusu kusamehemana,mimi kwa moyo wangu wote nimekubali kukusamehe.Nakuombea kwa Mungu naye akusamehe na tuendelee na mipango yetu ya ndoa kama kawaida ? Maneno yale machache yakampa Emmy faraja kubwa na kumfanya ainuke na kunikumbatia
kwa furaha.Sebule yangu ikageuka sehemu ya furaha kubwa.Watu tukashikana mikono na kupongezana.Lilikuwa nitukio kubwa na la kihistioria katika maisha yangu.Vinywaji vikaletwa tukaendelea kuburudika hadi ilipotimu saa mbili za usiku tukaagana wakaondoka.Walipoondoka nikabaki mwenyewe nikitafakari juu ya kilichotokea.Pamoja na kumsamehe Emmy lakini bado roho yangu haikuwa ikimtazama kama nilivyokuwa nikimtazama hapo zamani. ?Hivi ni kweli roho yangu imekubali kwa dhati kumsamehe Emmy kwa kitu alichonifanya?? Nikajiuliza tena kwa mara ya pili.Saa chache zilizopita sikutamanai kkumuona tena Emmy katika maisha yangu kuokana na kitendo kile lakini sasa nimeamua kumsamehe. ?Kwa vile nimamua kumsamehe acha tu nimamehe.Nahisi amekiri toka moyoni mwake.?Nikajisemea mwenyewe. Maisha mapya yakaanza tena.Penzi letu likaonekana kama vile limechipua upya.Upendo ukaongezeka mara dufu.Enmmy alionekana kubadilika sana na hiyo ikanihakikishia kuwa hawezi kurudia tena kosa alilolifanya. Taratibu jeraha lililokuwa moyoni mwangu likaanza kufutika.Nikaanza kusahau yote yaliyokuwa yamepita.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO??????? ;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;
No comments:
Post a Comment