ndugu msomaji naomba ufatilie mkasa huu mtamu na wa kusisimua sana wenye vipande vingi sana naomba usiache kuandika email yako kwenye sehemu iliyoandikwa jaza email ili kila kipande kinapopanda hewani kije moja kwa moja lakin pia follow blog yangu kwa kila kinachokuja hewani ukipate kwa muda
BEYOND PAIN SEHEMU YA 1
Ni saa kumi jioni nikiwa maeneo ya Kimandolu nikielekea Usa river katika baa iliyotulia ya Roterdam garden mahala panapofanyika vikao vya harusi yangu.Wanakamati ya maandalizi walichagua mahala hapa kutokana na utulivu wake kwani kuna bustani nzuri na hata huduma zake ni nzuri sana.Nikiwa maeneo haya ya Kimandolu gari ikienda taratibu kutokana na magari mengi kukaa pembeni ya bara bara kwa muda mrefu kwa kupisha misafara ya viongozi wa jumuia ya Afrika mashariki waliokuwa na kikao chao hapa Arusha.Siku zote kunapokuwa na mikutano ya namna hii jijini Arusha huwa kunakuwa na adha kubwa kwa watumiaji wa bara bara hii ya Moshi - Arusha kwa sababu ndiyo bara bara kuu waitumiayo viongozi hawa wakitokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).Mara simu yangu ikaita nikaitazama na kukuta ni Mr Cheleo mmoja kati ya wanakamati. ?Haloo kaka? nikasema ?Haloo ,uko wapi? Sisi tumeshafika tunakusubiri wewe tu.? ?Niko njiani kaka si unajua leo njia ilikuwa imefungwa viongozi walikuwa wanaondoka.Ndani ya dakika kumi nitakuwa nimefika hapo Usa river.? ?Ok kaka tunakusubiri? Hiki kilikuwa ni mojawapo ya kikao cha maandalizi ya harusi yangu inayotarajiwa kufanyika muda wa kama mwezi mmoja ujao.Harusi ambayo kila mmoja wa rafiki zangu alikuwa akiisubiri kwa hamu sana.Nimekuwa mchangiaji mzuri wa harusi za rafiki zangu na kuhakikisha zinafana safari hii walikuwa wamepania sana kufanya sherehe ya harusi yangu kuwa ya kihistoria. Tulipofika maeneo ya madukani gari zikaanza kwenda kasi na dakika tano baadae nikawasili usa river katika baa tulivu ya Roterdam.Nikapaki gari na kuelekea bustanini.Nikawasalimia wanakamati na kuwaomba radhi kwa kuchelewa kisha kikao kikaendelea.Kilikuwa ni kikao kirefu . Wakati kikao kikiendelea nikachukua simu na kumtumia mpenzi wangu Emmy ujumbe mfupi.Kwa siku tatu nilikuwa na shughuli nyingi na sikupata hata muda wa kuonana naye.Kwa sasa emmy anasoma digrii ya sheria katika chuo kikuu cha Tumaini makumira.Kila jioni huwa ana desturi ya kupita kwangu na hata kama sipo kwa kuwa ana ufunguo wa nyumbani kwangu huwa ananisubiri mpaka nikirudi tunakaa wote kisha namrudisha kwake.
?Hallow sunshine,niko kwenye kikao hapa roterdam.Baada ya kutoka hapa nitapita kwako.Missing you soooo much.? Huu ndio ujumbe mfupi niliomtumia Emmy kipenzi cha moyo wangu.
Tukaendelea na kikao.Baada ya kama robo saa hivi tangu niutume ule ujumbe mfupi wa maandishi kwa mpenzi wangu Emmy simu yangu inaita kuangalia zilikuwa ni namba za emmy.Nikainuka na kwenda mbali kidogo ili niweze kuongea naye. ?Halloo Darling ?Nikasema kimahaba.kwani ndivyo tulivyozoea wakati tunaongea simuni. Nusura moyo unipasuke kwa mstuko pale nilipoisikia sauti nzito ya kiume ikijibu. ?Mwanaharamu wewe,mpenda wake za watu.Huna haya unamwita nani Darling? Kumbe ndio mchezo wako huo wa kudandia wanawake wa watu.Leo nimekupata.? Nilibaki nimeduwaa kwa sekunde kadhaa nisijue nini cha kusema.sikuelewa yule jamaa alikuwa akimaanisha nini.Huku nikitabasamu nikauliza ?Mbona sikuelewi wewe.Unasemaje? samahani kama simu zimeingiliana? ?Simu hazijaingiliana we juha.We si ndio Wayne? Wayne mkotela?. ?yah ndio mimi? Nikajibu huku mapigo ya moyo yakinienda kwa kasi baada ya yule jamaa kulitamka jina langu ? Wewe si ndio umemtumia Sarafina ujumbe wa maandishi sasa hivi ukisema unakuja kumuona ukitoka kwenye kikao? ?Mimi nimemtumia ujumbe Emmy na sio sarafina? ?sasa sikiliza wewe mjinga?.?Nilihamaki baada ya kuitwa vile lakini nikavumilia nimsikie alichotaka kusema ?Iwe ni huyo Sara au Emmy kama unavyojua lakini nakwambia kuwa huyu ni mke wa mtu na mimi ndio bwana wake.?.. ?Unasemaje wewe??..Nikauliza kwa hamaki ?Hebu mpe Emmy simu yake haraka.Mpuuzi wewe? Nikasema tena kwa hasira ?Mpumbavu wewe ! hivi nikwambie mara ngapi Hakuna Emmy hapa?Huyu anaitwa Sarafina.Kama alikwambia anaitwa Emmy alikudanganya.Huyu ni sarafina na mimi ndio mumewe,mimi ndio ninayemlipia hii nyumba anayoishi na ni mimi ndio niliyemtafutia kazi pale AICC na baadae nikamtafutia nafasi ya masomo pale Makumira.Mimi ndiye ninayemlipia ada na kila kitu.Mimi ndiye ninayemuweka mjini.Nilikuwa nje ya nchi nilikuwa napata taarifa kuwa kuna mtu anatembea na mke wangu nikajua ni utani.Leo ndio nimegundua kuwa ni kweli? akasema Yule jamaa. ?Mjinga mkubwa wewe,huna haya mimi ndie ninayemlipia Emmy ada zote za masomo na hata nyumba anayokaa mimi ndiye ninayelipa.Na kwa taarifa yako mpumbavu wewe,sasa hivi tuko katika maandalizi ya harusi yetu na kesho jumapili kanisani wanasoma tangazo la kwanza la ndoa yetu.Hivyo nakuomba usijaribu kwa namna yoyote ile kuleta upumbavu wako ? Tayari hasira ilikwisha nipanda nikatamka maneno yale kwa hasira. ?Sikiliza we mjinga yaani pamoja na kukueleza kote huku bado hunielewi sasa Emmy huyu hapa hebu ongea naye? Nikasikia akimpa mtu simu na kumlazimisha ?Hebu ongea na huyu mbwa mwenzako mweleze ukweli mimi ni nani na mkanye akome kuanzia leo kukufuata fuata la sivyo nitamfanyia kitu kibaya sana ,hanijui mimi ni nani mjinga huyu? maneno haya nikayasikia kwa mbali.Mara nikasikia kitu ambacho sikukitegemea kukisikia maishani mwangu.Niliomba ardhi ipasuke niingie ndani.Nilitamani nijimalize pale pale.sikuona thamani tena ya kuendelea kuishi katika dunia hii. Niliisikia sauti ile tamu na nyororo iliyozoea kuniburudisha kila siku na kunifanya nione kama niko peponi,sauti ambayo niliamini ni sauti nzuri kuliko zote duniani,sauti ya mpenzi wangu,bibi harusi mtarajiwa Emmy.Huku akilia kwa kwikwi akatamka maneno ambayo yalinifanya niichukie dunia na watu wake na hasa wanawake.
?Wayne I?m sorry mimi ni mke wa mtu,na ninaomba usiendelee tena kumtukana mume wangu? Ilikuwa ni kama niko ndotoni nikazubaa kwa sekunde kadhaa kisha nikajikaza kiume na kuuliza tena. ?Emmy is that you????. ?Yes Wayne please leave me alone.Usinipigie simu tena.Mimi nina bwana wangu? Machozi yalianza kunitoka.Sikuamini kile nilichokisikia. ?Please Emmy tell me its not true ? Nikasema tena huku machozi yakinitoka. ?My name is not Emmy?..Akashindwa kuendelea alikuwa akilia.Yule jamaa akachukua tena simu ?Sasa umeamini we kijana.Tafadhali usiendelee kumfuata fuata sarafina.Kitakachokupata usije kumlaumu mtu???..?Akamalizia kwa tusi zito na kukata simu Nikahisi miguu ikiisha nguvu nikaakaa chini. Christopher rafiki yangu mkubwa alihisi lazima nitakuwa na tatizo akanifuata .Akastuka baada ya kunikuta nimekaa chini. ?Wayne.. ?Akaita nikamuangalia sikuwa na nguvu za kujibu. ?Wayne una tatizo gani? Akawaita wanakamati wote wakaja mbio na kuanza kunipepea.Nikaletewa maji nikanywa.Dakika kama tano hivi baadae nikaweza kuongea ?Take me home? Nikamwambia Chris ?Wayne una tatizo gani.Twende hospitali? Akasema Chris ?No ! take me home? Nikasema huku nikijaribu kuinuka.Wakanisaidia kutembea hadi garini kisha Chris akawasha gari na kuondoka kunipeleka nyumbani. Picha mbali mbali zikawa zinakuja na kupotea.Nilihisi kama vile niko ndotoni .Chris aliendesha kwa kasi bila kunisemesha.Tulipofika maeneo ya sanawari nikafungua mdomo na kumwambia Chris. ?Nipeleke kwa Emmy? Chris alikuwa akipafahamu anapoishi Emmy hivyo tulipofika maeneo ya Ilboru akakata kushoto na moja kwa moja akaelekea nyumbani kwa Emmy. Alisimamisha gari nje ya nyumba ya Emmy.Sikuongea kitu nikafungua mlango nikashuka garini.Mlinzi wa kimasai wa nyumba ya Emmy alinifahamu hivyo aliponiona akanisalimia nikapita zangu hadi ndani.Chris naye alikuwa akinifuata kwa nyuma.Nilisimama mlangoni na kusikia watu wakinong?ona kwa ndani.Nilikuwa na funguo ya mlango nikaufungua bila kugonga na kuingia ndani.Sebuleni nilimshuhudia Emmy akiwa kifuani kwa baba mmoja mnene wakiwa katika mahaba mazito.Nikaanguka na kupoteza fahamu.
* * * *
Nilizinduka na kujikuta mahala nisipopafahamu.Nilikuwa katika chumba chenye harufu ya dawa.Ndani ya chumba hiki kulikuwa na watu kadhaa.Mtu wa kwanza kumtambua alikuwa Chris. ?Pole sana Wayne?.Akasema huku akinishika kichwa.?Tafadhali usiinuke , endelea kupumzika.? Muda huo huo akaja daktari akiwa ameongozana na wauguzi wawili,nikajua hapa nipo hospitali.daktari akanipima kisha akasema ?Kwa sasa unaendelea vizuri.Itabidi ulale hapa leo ili tuendelee kukuangalia zaidi? Sikuwa na ubishi ingawa sikuhisi kuumwa sehemu yoyote ile zaidi ya kichwa kuwa kizito mno.Daktari akatoa maelekezo kadhaa kwa wale wauguzi akaandika pia katika kijikadi kisha akatoka.Pale mlangoni nilisikia akiongea kama na kundi la watu.na dakika hiyo hiyo watu zaidi ya ishirini wakaingia mle chumbani.Walikuwa ni wanakamati ya maandalizi ya harusi yangu pamoja na baadhi ya rafiki zangu.Walinipa pole nami nikawahakikishia kuwa niko salama wakanitakia usiku mwema wakaondoka.pale hospitali nikabaki na Chris
?Chris nini kilitokea mpaka nikaletwa hapa? Chris akanitazama kisha akajibu ?Wayne ulianguka ukapoteza fahamu ,ikanibidi nikulete hapa katika hospitali hii .Usijali kila kitu kinakwenda vizuri.Daktari anasema kesho asubuhi atakuruhusu? Niliposikia kuanguka na kupoteza fahamu ,ndipo nikalikumbuka tukio zima lililotokea.Ghafla fahamu zikanipotea tena. Nilirejewa na fahamu baadae sikujua ni saa ngapi.Ukiacha yule daktari mmoja aliyekuwapo mida ile sasa walikuwapo watatu.hali hii iliniogopesha sana.Nikaogopa pengine hali yangu si nzuri.Daktari mmoja mzee mwenye miwani akanisogelea na kuniuliza ?Wayne unajisikiaje sasa hivi?? ?Najisikia safi ila kichwa ni kizito sana.Nahisi kama kizungu zungu kwa mbali? ?Ok sawa.Hali yako inaendelea vizuri,vipimo vyote vinaonyesha uko sawa ila unachotakiwa kwa sasa ni kujaribu kutokuwaza kitu chochote kinachoweza kukusababishia ukapoteza fahamu kwa mara nyingine.Jaribu kupata mapumziko ya kutosha na jitahidi sana kutokuwaza?..? Nilimtazama yule daktari sikuwa na jibu la kumpa.Nafikiri hakujua kitu gani kilichonipata.Hakuyaelewa maumivu yaliyokuwa moyoni mwangu. ?Ok dokta nitajitahidi?.Nilisema huku machozi yakinilenga. Madaktari na wauguzi wakatoka na kuniacha chumbani mimi na Chris.hawakutaka Chris aniache peke yangu kwa kuwa waliogopa pengine ningeweza kujidhuru. Niliinuka na kukaa kitandani.Chris akanisaidia nikakaa sawa. ?Chris I hate the world?Nikasema kwa sauti ndogo Chris akanitazama akasema. ?Wayne jitahidi upumzike.Usiwaze lolote kwa sasa.Everything will be ok? ?No Chris.Nothing is ok.Emmy lied to me????????Nikasema huku machozi yakinitoka. ?Don?t cry buddy,be strong? akasema chris huku akinipiga piga mgongoni ? I loved her .I loved her Chris more than I love myself.Lakini ona kitu alichonifanyia?..Nitauweka wapi uso wangu mimi?.?.Uso wote ulijaa machozi.Iliniuma kupita kiasi. ?Wayne lala kwanza.Tutaongea asubuhi? Akasisitiza Chris. ?No Chris siwezi lala wakati mwanamke niliyempenda amenisaliti?.why me????? Why this pain???? ?Ok brother let it out??let it out?.?Akasema Chris. ?Emmy amenidanganya muda wote huu kumbe ni mke wa mtu?.? ?what!!!!!!!!? Akahamaki Chris ?Yah! ana bwana wake.Ndiye yule tuliyemkuta amelala naye kwenye sofa pale sebuleni kwake.Kwa mdomo wake mwenyewe ameniambia nisimsumbue yeye ana mume wake ? Chris akainuka na kuanza kuzunguka mle chumbani huku ameshika kichwa. ?Is this true brother?Akauliza ?Yah..kwa mdomo wake amenitamkia maneno haya?.It hurt Chris it hurt so much.? ?Mwanaharamu huyu??.?Akasema Chris kwa hasira ?Kesho ndoa yetu inatangazwa kanisani kwa mara ya kwanza??.nikashindwa kuendelea.Nilishindwa kujizuia kuangusha machozi. ?Wayne its gonna be ok.Jitahidi ulale kesho tutayaongea mambo haya.Usiwaze sana kilichotokea.Hii ni mitihani tu ya maisha? Chris alijaribu kwa kila njia kunibembeleza ili niweze kuwa katika hali yangu ya kawaida lakini kwa hali halisi jinsi ilivyo ni ngumu sana. Ni Jumatano ya wiki hii tumetoka kuandikisha ndoa kanisani na kesho tangazo la kwanza linaanza kusomwa.tayari maandalizi yote ya harusi yamekamilika .Nitauweka wapi uso wangu mimi.Nitawaeleza nini watu wanaoisubiri harusi yangu??Nitawaleleza nini wazazi na
ndugu zangu? Simlaumu mtu.Emmy nilimchagua mwenyewe.Hakunichagulia mtu yeyote.Iwapo ningechaguliwa na wazazi au mtu mwingine , ningekuwa na kila sababu ya kuwatupia mzigo wa lawama wao kwa uchaguzi wao usiofaa.Lakini hili lilikuwa ni chaguo langu mwenyewe..Huu ni mzigo wangu na inanibidi nisimame kidete niukabili.Nilijilaza kitandani na sijui hata saa ngapi nilipata usingizi. Saa tano asubuhi tayari nilikuwa nyumbani kwangu maeneo ya majengo.Nilikuwa najisikia mzima wa afya isipokuwa kichwa kilikuwa kikiniuma kwa mbali.Chris ndiye aliyenichukua hospitali na kunirudisha nyumbani. Mpaka sasa hivi hakuna mtu mwingine aliyekuwa akijua nini kilichotokea na kupelekea kupoteza fahamu na kulazwa hospitali zaidi yangu na Chris.Sikutaka kuharakisha kuliweka wazi jambo hili gumu.Nilitaka kuacha kwanza akili yangu itulie.Nilikaa kidogo sebuleni ,halafu nikamwambia Chris aniache nikapumzike. ?Brother naomba nikapumzike,halafu tutaongea jioni.Ila tafadhali naomba usimwambie mtu yeyote nini kilichotokea..? ?Ok wayne nenda kampumzike ila tafadhali don?t do anything stupid?Akasema Chris huku akitoa tahadhari kwani madaktari walimuonya asikubali kuniacha peke yangu kwa kuhofia pengine ninaweza kujidhuru. ?C?mon Chris,I?m not a kid.Haya ni mambo ya kawaida katika maisha.Let me have a rest then I?ll know what to do next.? ?Ok wayne..nitapita mchana kukuangalia.Nikuletee chakula gani mchana? ?Nothing Chris.Usiniletee chochote.I don?t feel like eating anything.? ?Unatakiwa ule Wayne.unatakiwa uwe na nguvu.? Sikumjibu kitu nikamtazama na kuondoka kuelekea chumbani kwangu. Nilikaa kitandani,nikalifungua kabati langu na kutoa albamu kubwa la picha.Humu kuna picha nyingi ambazo nimepiga na emmy tangu tulipoanza mapenzi yetu .Picha yetu ya kwanza mimi na yeye ikanikumbusha tulikwenda picnic Ziwa Duluti.Ni siku tuliyofurahi sana.Siwezi kuisahau siku hii.Nikaendelea na kuzifunua picha nyingine.Wakati nikiendelea na kuzitazama picha simu yangu inalia.Alikuwa ni mama yangu. ?mama shikamoo? nikamsalimu ?Marahaba baba ,hamjambo? ?hatujambo mama,vipi mnaendeleaje? ?Huku wote wazima.Ni baba yako tu kichwa chake kile kinamsumbua sana lakini anaendelea vizuri? ?Mpe pole sana ?Nikajibu kwa ufupi. ?Vipi mkwe wangu hajambo? Nikasita kujibu. ?eenh jamani hajambo mama mkwe? Mama akauliza tena baada ya kuona sijamjibu ?Hajambo mama?Nikajibu huku nikiuma meno kwa hasira.Mwanamke huyu amewadanganya hadi wazazi wangu.Iliniuma sana. ?nashukuru kama ni mzima.Vipi mnaendeleaje na maandalizi ya harusi? ?mama maandalizi ni mazuri.Tunaendelea vizuri? ?sawa baba.Leo huku wamesoma Tangazo la kwanza..Hivi ninavyokwambia watu wanajiandaa isivyo kawaida,kila ndugu anataka aje kwenye harusi yako.? Sikuwa na cha kusema.Machozi yalikuwa yananitoka. ?Mama nashukuru.Nitakupigia baadae tutaongea vizuri zaidi? ?Sawa baba? Nilikata simu na kuitupia kitandani.hasira zikanipanda. ?Damn you Emmy?..? Nilizungunguka zunguka mle chumbani nikijaribu kuwaza na kuwazua bila kupata jibu.Nikatoka na kurudi sebuleni.Nikafungua kabati ninamoweka cd na kuchukua moja ya cd
niipendayo sana ya mmoja kati ya wanamuziki mahiri kwenye mziki wa bongo fleva,Hamis mwinjuma au Mwana F.A .Huu wimbo wake niliona ni kama vile alinitungia mimi kwa sababu ulinihusu mimi.Ubeti wa pili ndio uliniumiza zaidi ukanifanya niurudie tena na tena ?hata nikitaka kuoa niambie ntamuoa nani?/ watu wana watu wao wengine toka zamani/ ukiambiwa we ni boyfriend haimaanishi uko peke yako/ wadogo usoni wanahifadhi wazee wako/ sijui ni dhiki au tamaa tu??/ watoto wanaanika njaa tu/ hawafikirii mapenzi wanachoona wao ni mkwanja tu/? Maneno haya yalinichoma moyo.Kijana huyu aliimba vitu vya kweli kabisa na yote aliyoyaimba yamenikuta mimi. Nikarudi tena chumbani sikujua nini cha kufanya.Nilikuwa kama nimechanganyikiwa vile.Nikaona ni bora nijilaze kitandani na kijiusingizi kikanipitia. Nilistuka na mlio wa simu iliyokuwa kichwani kwangu,alikuwa ni Chris. ? Haloo? Nikasema ?Wayne umelala?? ?Ndiyo nilikuwa nimelala? ?Ok .Sasa wayne naomba uwe na moyo mgumu na usihamaki tafadhali.Ni kwamba Emmy amenifuata na hapa nilipo niko naye na ni yeye ndiye alinisisitiza nikupigie simu hii.? ?Unasemaje Chris????? ?Nikasema kwa ukali.Sikutegemea kusikia kitu kama kile. ?Wayne niko na Emmy hapa.amenitafuta na kuomba nafasi ya kuongea na wewe? ?Chris????..?Nilidakia,sikutaka aendelee tana kunipa habari za yule baradhuli ?Chris tafadhali.Kama na wewe unataka tukosane hamna shida ila tafadhali naomba usinipe habari zozote kuhusu huyu mwanamke.? Nikakata simu.Mwili wote ulikuwa unanichemka kwa hasira.Sikutaka kumsikia tena emmy katika maisha yangu.Nilikuwa na hasira mbaya mno kwa kitendo alichonifanyia na kama angekuwa karibu yangu sijui hata ningemfanya kitu gani.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO?????????.. ;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;
Story hii ya Mkasa wa mapenzi Kati ya Wayne na Emmy usiache hata kipande kimoja vipo vipande vya kutosha
ReplyDelete